Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza katika Mkutano na jumuiya ya Wafanyabiashara wa Austria jijini Vienna. |
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya uwekezaji Zanzibar Bw. Khamis Dunia akizungumza katika mkutano na wafanyabiashara wa Austria uliofanyika jijini Vienna tarehe 13 Juni, 2023 |
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya uwekezaji Zanzibar Bw. Khamis Dunia akizungumza katika mkutano na wafanyabiashara wa Austria uliofanyika jijini Vienna tarehe 13 Juni, 2023. |
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Bw. Gilead Teri akizungumza katika Mkutano na jumuiya ya Wafanyabiashara wa Austria uliofanyika jijini Vienna. |
Waziri
wa Mambo ya na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe Dkt. Stergomena Tax
amekutana na kuzungumza na jumuiya ya Wafanyabiashara wa Austria jijini
Vienna na kuwashawishi wafanyabiashara hao waje nchini kuwekeza, kufanya biashara na kutembelea vivutio vya utalii.
Dkt. Tax ameshiriki mkutano huo pamoja na Kituo cha Uwekezaji
Tanzania (TIC), Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) na Bodi ya Utalii
Tanzania (TTB) ambapo kwa pamoja walielezea jinsi serikali ilivyoboresha
mazingira ya kufanya biashara na uwekezaji nchini waliwashawishi kwamba Tanzania ni salama kwa mitaji yao na waje nchini pia kutembelea vivutio vya utalii
Wamewaelezea
Wafanyabiashara wa Austria juu ya faida zinazoweza kupatikana kupitia
uwekezaji au ubia na Serikali ya Tanzania au mtu binafsi kwamba hawatajuta kufanya hivyo.
Dkt.
Tax amewahakikishia Wafanyabiashara hao kuwa Tanzania ni nchi yenye
amani na usalama wake ni wa hali ya juu na hivyo ni kituo muafaka kwao kuwekeza mitaji yao na kufanya
biashara na ana hakika watapata soko, faida na kurejesha fedha zao watakazowekeza nchini.
"Tanzania ni nchi yenye amani na usalama, kiufupi Tanzania
ni njema na kwa hivyo mtakuwa na uhakika wa kurejesha fedha zenu mlizoweka kwa kuwa na soko la uhakika na faida pia mtapata kutokana na usalama wa mitaji yenu na kufanya
biashara,” alisema Mhe. Waziri.
Akizungumza katika mkutano huo
Mwakilishi wa Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) Bw. Khamis Dunia
alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imefungua milango ya uwekezaji na
kuwakaribisha wenye nia ya kuwekeza Zanzibar katika maeneo ya utalii na
miundombinu waje nchini kuwekeza na kujionea vivutio.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) amesema Serikali
imeunganisha mifumo ya taasisi za usajili na uwezeshaji biashara ili
kutoa huduma bora kwa wawekezaji. Taasisi hizo zinajumuisha TIC, NIDA,
TRA, BRELA, Uhamiaji na Idara ya Kazi.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Bodi
ya Utalii Tanzania (TTB) Bw. Damas Mfugale Ali waambie wafanyabiashara
hao kuwa eneo la utalii lina utalii wa aina nyingi ambazo wawekezaji
wanaweza kuja nchini na kutembelea maeneo hayo na kuwekeza.
Aliongeza
kuwa Wafanyabiashara hao wanaweza pia kuja nchini na kuwekeza mmoja
mmoja au kwa kuungana na serikali kwa njia ya ubia na hivyo kusaidia
uendelezaji wa maeneo ya utalii kwa faida ya pande zote mbili.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.