Sunday, June 11, 2023

WAZIRI TAX AINADI TANZANIA KWA JUMUIYA YA WAFANYABISHARA WA ITALIA



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Stergomena Tax Akizungumza katika mkutano na Jumuiya ya wafanyabiashara wa Italia uliofanyika jijini Roma nchini Italia tarehe 10 Juni,2023.    


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Stergomena Tax Akizungumza katika mkutano na Jumuiya ya wafanyabiashara wa Italia uliofanyika jijini Roma nchini Italia tarehe 10 Juni,2023.  
Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akizungumza katika mkutano na Jumuiya ya wafanyabiashara wa Italia uliofanyika jijini Roma nchini Italia tarehe 10 Juni,2023.

Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Gilead Teri akizungumza katika mkutano na Jumuiya ya wafanyabiashara wa Italia uliofanyika jijini Roma nchini Italia tarehe 10 Juni,2023.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya uwekezaji Zanzibar Bw. Khamis Dunia akizungumza katika mkutano na Jumuiya ya wafanyabiashara wa Italia uliofanyika jijini Roma nchini Italia tarehe 10 Juni,2023.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bw. Damas Mfugale akizungumza katika mkutano na Jumuiya ya wafanyabiashara wa Italia uliofanyika jijini Roma nchini Italia tarehe 10 Juni,2023.
Baadhi ya Washiriki wa mkutano na Jumuiya ya wafanyabiashara wa Italia uliofanyika jijini Roma nchini Italia tarehe 10 Juni,2023 wakifuatilia mkutano huo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Italia (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa TTB Bw. Damas Mfugale (wa kwanza kulia) Mkurugenzi Mkuu wa TIC Bw. Gilead Teri (wa pili kushoto) na mwakilishi wa ZIPA Bw. Khamis Dunia baada ya kukamilisha mazungumzo yao na  Jumuiya ya wafanyabiashara wa Italia uliofanyika jijini Roma nchini Italia tarehe 10 Juni,2023.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dkt. Stergomena Tax kwa kushirikiana na  Ubalozi wa Tanzania nchini Italia, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Kituo cha Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) wameinadi Tanzania kama Kituo bora cha uwekezaji kwa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Italia.
 
Waziri Tax amewaeleza Wafanyabiashara hao kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuboresha mazingira ya biashara nchini kwa kurekebisha sera na sheria mbalimbali ili kuwafanya wawekezaji wawe na mazingira bora ya kuendesha shughuli zao na hivyo kuvutia wawekezaji wengi zaidi.
 
Wafanyabiashara hao wameelezwa kuwa Tanzania ni salama kwa wao kuwekeza mitaji yao, ambapo pia watakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kulifikia na kunufaika na soko kubwa la EAC, SADC na Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA).
 
Miongoni mwa sekta zilizowavutia Wafanyabiashara walioshiriki mkutano huo ni pamoja na Kilimo, Utalii, Viwanda, Uchumi wa Buluu, na Ujenzi.
 
Mkutano huo uliofanyika jijini Roma, Italia ulijumuisha Wafanyabiashara waliowekeza nchi Tanzania katika Sekta mbalimbali na wenye nia ya kuwekeza nchini







No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.