Thursday, June 15, 2023

MAHAKAMA YA AFRIKA YAISHUKURU SERIKALI YA TANZANIA

Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Jaji Imani Aboud kutoka Tanzania ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa misaada inayoipatia mahakama hiyo ikiwemo ujenzi wa jengo la ofisi ambapo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ilikabidhi eneo la ujenzi kwa Mkandarasi CRJE jijini Arusha tarehe 02 Juni 2023.

 

Jaji Aboud ametoa shukrani hizo wakati wa kikao na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena L. Tax (Mb) kilichofanyika jijini Dodoma leo tarehe 15 Juni 2023.

 

Rais wa Mahakama ya Afrika na watumishi wengine, wakiwemo Makamu wa Rais; Majaji na Msajili wapo jijini Dodoma kwa ajili ya kikao (retreat) cha kutathmini utekelezaji wa majukumu ya Mahakama hiyo ili kubaini mafanikio na changamoto kwa ajili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.

 

Kwa kutumia fursa ya kikao kufanyika Dodoma, Rais na ujumbe wake wametumia nafasi hiyo kukutana na wadau mbalimbali ikiwemo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) ili kajadili utekelezaji wa majukumu ya chombo hicho muhimu barani Afrika.

 

Kwa upande wake, Mhe. Waziri Dkt. Tax alieleza kufurahishwa na uamuzi wa Mahakama hiyo wa kufanya kikao chao jijini Dodoma ambapo ni makao makuu ya nchi. Aidha, aliwahakikishia kuwa Serikali itaendelea kuwapa ushirikiano unaohitajika ili mahakama hiyo iweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kukamilisha ujenzi wa jengo la Ofisi.

 

Mhe. Waziri Dkt. Tax alihitimisha mazungumzo yake kwa kumpongeza Jaji Aboud kwa kuchaguliwa tena kwa kipindi cha awamu ya pili na cha mwisho cha miaka miwili kuwa Rais wa Mahakama hiyo. Jaji Aboud alichaguliwa wakati wa ufunguzi wa Baraza la 69 la Pan-Afrika lililofanyika Arusha tarehe 12 Juni 2023.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikino wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza wakati wa Mkutano kati yake na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Mhe. Jaji Imani Aboud (hayupo pichani) alipomtembelea Ofisi kwake jijini Dodoma tarehe 15 Juni 2023. Mhe. Jaji Imani na ujumbe wake, wakiwemo Makamu wa Rais; Majaji na Msajili wapo jijini Dodoma kwa ajili ya kikao cha kutathmini utekelezaji wa majukumu ya Mahakama hiyo ili kubaini mafanikio na changamoto kwa ajili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikino wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza wakati wa Mkutano kati yake na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Mhe. Jaji Imani Aboud (kshoto) alipomtembelea Ofisi kwake jijini Dodoma tarehe 15 Juni 2023. Kulia ni Makamu Rais wa Mahakama hiyo, Mhe. Jaji Sacko Madibo
Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Mhe. Jaji Imani Aboud akizungumza wakati wa Mkutano kati yake na Mhe. Dkt. Tax (hayupo pichani)
Mkutano ukiendelea
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Levina Maleo akizungumza wakati wa Mkutano kati ya Mhe. Waziri Dkt. Tax na Mhe. Jaji Aboud hawapo pichani
Afisa kutoka Kitengo cha Sheria, Bi. Elizabeth Bukwimba akichangia jambo wakati wa Mkutano kati ya Mhe. Dkt. Tax na Mhe. Jaji Aboud hawapo pichani
Mhe. Jaji Aboud akimpatia Mhe, Dkt. Tax zawadi ya nembo ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu mara baada ya kukamilisha mazungumzo yao
Mhe. Dkt. Tax na Mhe. Jaji Aboud wakijadili jambo baada ya mazungumzo yao
Picha ya pamoja 
Picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.