Friday, October 11, 2024
MISHENI YA SADC YATOA TAARIFA YA AWALI KUHUSU UCHAGUZI MKUU NCHINI MSUMBIJI
Rais Mstaafu wa Zanzibar
na Mkuu wa Misheni ya SADC ya Uangalizi wa Uchaguzi Mkuu nchini Msumbiji, Mhe.
Dkt. Amani Abeid Karume, leo tarehe 11 Oktoba 2024 ametangaza Taarifa ya Awali
kuhusu Uchaguzi wa Rais na Wabunge kufuatia uchaguzi uliofanyika nchini humo
tarehe 9 Oktoba 2024.
Katika hotuba yake, Mhe.
Dkt. Karume amesema kuwa uchaguzi nchini Msumbiji kwa kiasi kikubwa umezingatia
kanuni na miongozo ya uchaguzi wa kidemokrasia ya SADC, inayosisitiza katika
haki, uhuru, usawa, na uwazi.
Amesema katika kutekeleza
jukumu lake, misheni hiyo iliangalia masuala mbalimbali muhimu kabla na wakati
wa uchaguzi, ikiwemo hali ya siasa na usalama nchini humo, usimamizi wa
uchaguzi, ripoti za vyombo vya habari kuhusu uchaguzi, na uwakilishi wa jinsia,
ambayo yote yametekelezwa kwa kiasi kikubwa.
Aidha, Misheni hiyo
imeshuhudia nchi hiyo ikiwa katika hali ya amani na utulivu katika kipindi
chote cha kabla na wakati wa uchaguzi, ambapo kampeni, mikutano ya hadhara na mchakato wa upigaji kura vilifanyika kwa amani,
licha ya changamoto za kiusalama katika baadhi ya maeneo, hususan katika jimbo
la Cabo Delgado.
Pia Mhe. Dkt. Karume
ametumia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi wa Msumbiji kwa kuonyesha ukomavu wa
kisiasa na uvumilivu katika kipindi chote cha uchaguzi, akiwataka washindani wa
kisiasa kufuata taratibu za kisheria endapo kutatokea migogoro yoyote kuhusu
uchaguzi.
Pia ametoa wito kwa wadau
mbalimbali kuendelea kuwa watulivu na wavumilivu wakati mamlaka za usimamizi wa
uchaguzi zikikamilisha matokeo ya uchaguzi kabla ya kutangazwa rasmi, akiwaomba
kuendelea kuhamasisha amani, uvumilivu, na utulivu kupitia majukwaa mbalimbali
katika kipindi cha baada ya uchaguzi.
Kulingana na Misingi na
Miongozo ya SADC inayosimamia uchaguzi wa kidemokrasia iliyorekebishwa mwaka 2021,
misheni hiyo itatoa taarifa ya mwisho kuhusu uchaguzi siku 30 baada ya kutolewa
kwa taarifa ya awali.
Misheni ya SADC,
iliyozinduliwa rasmi tarehe 3 Oktoba 2024, ilipeleka waangalizi 52 katika
majimbo yote 11 ya Msumbiji ili kuangalia uchaguzi.
Mhe. Dkt. Karume
aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Asasi ya
Siasa, Ulinzi, na Usalama, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuongoza misheni
hiyo.
Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Mhe. Phaustine Kasike akishiriki mkutano wa uwasilishwaji wa Taarifa ya Awali ya SADC ya Uangalizi wa Uchaguzi Mkuu nchini Msumbiji |
Sehemu ya wadau mbalimbali walioshiriki mkutano |
Sehemu nyingine ya wadau |
Mkutano ukiendelea |
Mkutano ukiendelea |
Thursday, October 10, 2024
MKUU WA MISHENI YA UANGALIZI WA UCHAGUZI YA SADC NCHINI MSUMBIJI ASHUHUDIA ZOEZI LA UPIGAJI KURA NCHINI MSUMBIJI
Rais Mstaafu wa Zanzibar
na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika (SADC –SEOM) nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume alitembelea
vituo kadhaa vya kupigia kura katika jiji la Maputo kwa ajili ya kuangalia
ufunguzi wa vituo hivyo, zoezi la upigaji kura na zoezi la kuhesabu kura kufuatia
uchaguzi uliofanmyika tarehe 09 Oktoba, 2024 nchini humo.
Mhe. Dkt. Karume ambaye
aliambatana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, Mhe.
Elias Magosi na Mjumbe wa Troika kutoka
Tanzania na Mshauri wa Rais masuala ya Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Sofia
Mjema, alianza kwa kutembelea kituo cha kupigia kura katika Shule ya Sekondari
ya Josima Machel ambapo pia ni kituo alichopigia kura Rais wa Msumbiji, Mhe.
Filipe Nyusi.
Vituo vingine alivyotembelea
ni katika Shule za Msingi za Fevereiro, Maxaquene, Maxaquene Khovo na Kitivo
cha Elimu ya Michezo na Mazoezi.
Mhe. Dkt. Karume pia alishuhudia
ufungwaji wa vituo vya kupigia kura na zoezi la kuhesabu kura baadaye jioni.
Misheni ya Uangalizi ya
SADC nchini Msumbiji imepeleka Waangalizi 52 katika majimbo yote 11 nchini humo
ambayo ni Cabo Delgado, Gaza, Inhambane, Manica, Maputo City, Maputo, Niassa,
Nampula Tete na Zambezia.
Mhe. Dkt. Karume aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuongoza Misheni hiyo.
Mwananchi akipiga kura |
Mwananchi akiwa katika chumba cha kupigia kura |
Mwananchi akiwekwa alama ya wino mara baada ya kupiga kura |
Wednesday, October 9, 2024
NAIBU WAZIRI CHUMI ASISITIZA WELEDI NA UWAJIBIKAJI
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi (Mb.) akifungua mafunzo ya siku nne (4) ya Mawasiliano ya Kidiplomasia kwa Maafisa Waandamizi wa Wizara hiyo yanayofanyika katika Hotel ya St. Gaspar jijini Dodoma kuanzia tarehe 8 hadi 11 Oktoba 2024. |
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Chiku Kiguhe akimkaribisha Naibu Waziri Mhe. Cosato Chumi kwenye ufunguzi wa mafunzo ya Mawasiliano ya Kidiplomasia kwa Maafisa Waandamizi wa Wizara hiyo yanayofanyika katika Hotel ya St. Gaspar jijini Dodoma. |
Mfunzo yakiendelea |
Mafunzo yakiendelea |
Picha ya pamoja |
Hafla ya ikiendelea |
Katibu wa Mabalozi Wastaafu, Balozi Bertha Semu Somi akisisitiza jambo kwenye ufunguzi wa mafunzo ya Mawasiliano ya Kidiplomasia kwa Maafisa Waandamizi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki yanayofanyika katika Hotel ya St. Gaspar jijini Dodoma. |
Balozi Peter Kalaghe akifuatilia mafunzo Maafisa Waandamizi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akifuatilia hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya Mawasiliano ya Kidiplomasia kwa Maafisa Waandamizi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki yanayofanyika katika Hotel ya St. Gaspar jijini Dodoma. |
Tuesday, October 8, 2024
Monday, October 7, 2024
WAZIRI KOMBO: TANZANIA ITAENDELEA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA KULETA AMANI AFRIKA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) akihutubia kwenye Mdahalo wa kwanza wa Amani na Usalama Afrika (APSD) ulioandaliwa na Taasisi ya Thabo Mbeki uliofanyika jijini Johannesburg, nchini Afrika Kusini. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) akihutubia kwenye Mdahalo wa kwanza wa Amani na Usalama Afrika (APSD) ulioandaliwa na Taasisi ya Thabo Mbeki uliofanyika jijini Johannesburg, nchini Afrika Kusini. |
Rais wa zamani wa Afika Kusini Mhe. Thabo Mbeki akichangia jambo kwenye Mdahalo wa kwanza wa Amani na Usalama Afrika (APSD) ulioandaliwa na Taasisi ya Thabo Mbeki jijini Johannesburg, nchini Afrika Kusini. |
Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Mhe. James G. Bwana akifuatilia Mdahalo wa kwanza wa Amani na Usalama Afrika (APSD) ulioandaliwa na Taasisi ya Thabo Mbeki uliofanyika jijini Johannesburg, nchini Afrika Kusini. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Bertha Makilagi |
Mkutano ukiedelea |