Thursday, October 10, 2024

MKUU WA MISHENI YA UANGALIZI WA UCHAGUZI YA SADC NCHINI MSUMBIJI ASHUHUDIA ZOEZI LA UPIGAJI KURA NCHINI MSUMBIJI

Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC –SEOM) nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume alitembelea vituo kadhaa vya kupigia kura katika jiji la Maputo kwa ajili ya kuangalia ufunguzi wa vituo hivyo, zoezi la upigaji kura na zoezi la kuhesabu kura kufuatia uchaguzi uliofanmyika tarehe 09 Oktoba, 2024 nchini humo.

 

Mhe. Dkt. Karume ambaye aliambatana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, Mhe. Elias Magosi  na Mjumbe wa Troika kutoka Tanzania na Mshauri wa Rais masuala ya Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Sofia Mjema, alianza kwa kutembelea kituo cha kupigia kura katika Shule ya Sekondari ya Josima Machel ambapo pia ni kituo alichopigia kura Rais wa Msumbiji, Mhe. Filipe Nyusi.

 

Vituo vingine alivyotembelea ni katika Shule za Msingi za Fevereiro, Maxaquene, Maxaquene Khovo na Kitivo cha Elimu ya Michezo na Mazoezi.  

 

Mhe. Dkt. Karume pia alishuhudia ufungwaji wa vituo vya kupigia kura na zoezi la kuhesabu kura baadaye jioni.

 

Misheni ya Uangalizi ya SADC nchini Msumbiji imepeleka Waangalizi 52 katika majimbo yote 11 nchini humo ambayo ni Cabo Delgado, Gaza, Inhambane, Manica, Maputo City, Maputo, Niassa, Nampula Tete na Zambezia.

 

Mhe. Dkt. Karume aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuongoza Misheni hiyo.

Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC –SEOM) nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume akizungumza na mmoja mawakala wa vyama wanaosimamia zoezi la upigaji alipotembelea vituo kadhaa vya kupigia kura katika jiji la Maputo kwa ajili ya kuangalia ufunguzi wa vituo hivyo, zoezi la upigaji kura na zoezi la kuhesabu kura kufuatia uchaguzi uliofanmyika tarehe 09 Oktoba, 2024 nchini humo.


Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC –SEOM) nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume akizungumza na mmoja wa mawakala wa vyama wanaosimamia zoezi la upigaji alipotembelea vituo kadhaa vya kupigia kura katika jiji la Maputo kwa ajili ya kuangalia ufunguzi wa vituo hivyo, zoezi la upigaji kura na zoezi la kuhesabu kura kufuatia uchaguzi uliofanmyika tarehe 09 Oktoba, 2024 nchini humo. Mhe. Dkt. Karume aliambatana na ujumbe wake akiwemo Katibu Mtendaji wa SADC, Mhe. Eliasi Magosi (mwenye kofia) na Mjumbe wa Troika kutoka Tanzania na Mshauri wa Rais masuala ya Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Sofia Mjema (mwenye kilemba)

Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC –SEOM) nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume akizungumza na maafisa wanaosimamia zoezi la upigaji alipotembelea vituo kadhaa vya kupigia kura katika jiji la Maputo kwa ajili ya kuangalia ufunguzi wa vituo hivyo, zoezi la upigaji kura na zoezi la kuhesabu kura kufuatia uchaguzi uliofanmyika tarehe 09 Oktoba, 2024 nchini humo.

Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC –SEOM) nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume akizungumza na mmoja wa mawakala wa vyama wanaosimamia zoezi la upigaji alipotembelea vituo kadhaa vya kupigia kura katika jiji la Maputo kwa ajili ya kuangalia ufunguzi wa vituo hivyo, zoezi la upigaji kura na zoezi la kuhesabu kura kufuatia uchaguzi uliofanmyika tarehe 09 Oktoba, 2024 nchini humo.

Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC –SEOM) nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume akizungumza na maafisa wanaosimamia zoezi la upigaji alipotembelea vituo kadhaa vya kupigia kura katika jiji la Maputo kwa ajili ya kuangalia ufunguzi wa vituo hivyo, zoezi la upigaji kura na zoezi la kuhesabu kura kufuatia uchaguzi uliofanmyika tarehe 09 Oktoba, 2024 nchini humo.

Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC –SEOM) nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume akiangalia moja ya sanduku la kupigia kura alipotembelea vituo kadhaa vya kupigia kura katika jiji la Maputo kwa ajili ya kuangalia ufunguzi wa vituo hivyo, zoezi la upigaji kura na zoezi la kuhesabu kura kufuatia uchaguzi uliofanmyika tarehe 09 Oktoba, 2024 nchini humo.

Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC –SEOM) nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume akizungumza na mawakala wanaosimamia zoezi la upigaji kura alipotembelea vituo kadhaa vya kupigia kura katika jiji la Maputo kwa ajili ya kuangalia ufunguzi wa vituo hivyo, zoezi la upigaji kura na zoezi la kuhesabu kura kufuatia uchaguzi uliofanmyika tarehe 09 Oktoba, 2024 nchini humo.
Wananchi wakiwa wamejipanga mstari katika vituo vya kupigia kura jijini Maputo tayari kwa kupiga kura

Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC –SEOM) nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume akishuhudia Afisa anayesimamia zoezi la upigaji akitoa maelezo kwa mpiga kura kabla ya kupiga kura
Mwananchi akipiga kura
Mwananchi akiwa katika chumba cha kupigia kura
Mwananchi akiwekwa alama ya wino mara baada ya kupiga kura
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Talha Waziri akimwonesha Mhe. Dkt. Karume taarifa  iliyotumwa kwa njia ya video  kutoka kwa waangalizi wa uchaguzi wa SADC waliopelekwa kwenye majimbo mbalimbali kuhusu namna uchaguzi unavyoendelea kwenye maeneo hayo

Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC –SEOM) nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume akishuhudia zoezi la kuhesabu kura
Zoezi la kuhesabu kura likiendelea





















































 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.