Wednesday, October 30, 2024

MAFANIKIO YA RAIS SAMIA KATIKA SEKTA YA AFYA YALETA HAMASA KWENYE MKUTANO WA MERCK FOUNDATION


Mafanikio ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sekta ya afya yamewavutia wabia wa maendeleo katika sekta hiyo kuwekeza zaidi nchini, ili kuongeza upatikanaji wa huduma bora za afya na kukuza maendeleo ya Taifa. 

Hayo jamejili leo tarehe 29 Oktoba 2024 kwenye Mkutao wa 11 wa Taasisi ya Merck Foundation Africa Asia Luminary unaoendelea katika Hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam ambao umefunguliwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia.

Mkutano huo uliofanyika Tanzania kwa mara ya kwanza umewakutanisha wadau wa Afya, Wenza wa Marais kutoka Mataifa 15 ya Afrika na Asia, Wawakilishi kutoka taasisi za kimataifa, Wanadiplomasia, waandishi wa habari na Wanataaluma mbalimbali kwa lengo la kubadilishana uzoefu, kujadili na kutafuta suluhu dhidi ya changamoto mbalimbali za afya na kijamii zinazokabili bara la Afrika na Asia. 

Wenza hao 15 wa Marais wanatoka; Zanzibar, Burundi, Kenya, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Gabon, Ghana, Liberia, São Tomé and Príncipe, Malawi, Maldives, Zimbabwe, Msumbiji, Cabo Verde na Gambia. 

Akifungua mkutano Rais Samia amesema Serikali imefanya maboresha makubwa katika sekta ya afya ikiwemo uboreshaji wa mifumo ya utoaji wa huduma za afya ikijumuisha ongezeko la vituo vya afya, vifaa tiba na kuimarika kwa huduma bora za afya za mama na mtoto.

“Nikiwa kama Mwanamke na Mama nimefanya kazi kubwa kwa kushirikiana na wadau katika kuboresha mifumo ya matibabu na utoaji wa elimu kwa umma ili kupiga vita ongezeko la magojwa katika jamii ikiwemo magonjwa yasiyo ambukiza” Alisema Mhe. Rais Samia. 

Rais Samia ameeleza kuwa juhudi hizo zilizofanywa na Serikali zimeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya afya ikiwemo kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi na upatikanaji wa huduma bora za afya katika jamii. 

Aidha Rais Samia ameishukuru Taasisi ya Merck Foundation kwa kufadhili miradi mbalimbali inayochangia kuboresha huduma za afya kwa mwanawake na kutoa mafunzo stahiki kwa watumishi katika sekta ya afya hatua ambayo imewezesha kuimarisha sekta za hiyo kwa nchi za Afrika na Asia. 

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Merck Foundation Dkt. Rasha Kelej amemwelezea Rais Samia kuwa ni Kiongozi mahiri Mwanamke na mwenye ushawishi duniani kutokana juhudi zake za kuibua na kutetea agenda zinazowezesha kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake kitaifa na kimatiafa. 

“Tumefarijika na kuvutiwa na namna Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuboresha sekta ya afya, elimu, kuwezesha wanawake kiuchumi na mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia. Hii imetupa hamasa kubwa ya kuendelea kushirikiana na Tanzania kwa kutanua uwigo wa huduma zetu hapa nchini ili kuhakikisha jamii ya Tanzania inapata maendeleo endelevu.” Alisema Dkt. Rash 

Awali Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawanake na Makundi Maalumu Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ameeleza kuwa Serikali imeweka mazingira mazuri ya kisera na kisheria katika kukuza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake na wasichana. Amebainisha kuwa mazingira hayo yamechangiwa na Sera ya Taifa ya Jinsia na Maendeleo ya Wanawake ya mwaka 2023, uanzishwaji wa Programu madhubuti za Elimu kwa Wasichana na Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi kupitia mikopo na mafunzo ya ujuzi wa biashara. 

Mkutano huo wa siku mbili wa Merck Foundation ambao unatarajiwa kuhitimishwa kesho tarehe 30 Oktoba 2024 umehudhuriwa na washiriki takriban 6000 kutoka nchi zaidi ya 50 duniani. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akifungua Mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Oktoba, 2024.
Sehemu ya Wenza wa Wakuu wa nchi mbalimbali Barani Afrika wakifuatilia Mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary uliokuwa ukiendelea katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Oktoba 2024.
Mkutano ukiendelea
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Cosato Chumi (Mb.) akisalimiana na wageni mbalimbali kwenye Mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary uliofanyika katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam
Mwenza wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Mama Mariam Mwinyi akifurahia jambo kwenye Mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary uliofanyika katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Wenza wa Wakuu wa nchi mbalimbali Barani Afrika wakifuatilia Mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary uliokuwa ukiendelea katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Oktoba 2024.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Merck Foundation Dkt. Rasha Kelej akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary uliofanyika katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Mabalozi wa Tanzania wanaoiwakilisha nchi sehemu mbalimbali wakifuatilia Mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary uliofanyika katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam.



Mwanza wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Mama Mbonimpaye Mpango kwenye Mkutano wa Mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary uliofanyika katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mawasiliano katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye Mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary uliofanyika katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam.
Mwenza wa Rais wa Jamhuri ya Ghana Mhe. Mama Rebecca Victoria Akufo-Addo akiwasalimia washiriki wa Mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary uliofanyika katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam.
Mwenza wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Mama Rachel Ruto akiwasalimia washiriki wa Mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary uliofanyika katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam.
Mwenza wa Rais wa Jamhuri ya Maldives Mhe. Mama Sajidha Mohamed akiwasalimia washiriki wa Mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary uliofanyika katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam.
Mkutano ukiendelea

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.