|
Mkuu wa Misheni ya Uangalizi uchaguzi Mkuu ya
SADC (SEOM) Mhe. Mizengo akiwa na
wajumbe wa SEOM wakiangalia moja ya sanduku la kuwekea karatasi za kupigia
kura katika kituo cha Taasisi ya sayansi
ya Afya alipotembelea kituo hicho kabla ya zoezi la kupiga kura kuanza jijini
Gaborone tarehe 30 Oktoba, 2024
|
|
Mkuu wa Misheni ya Uangalizi uchaguzi Mkuu ya
SADC (SEOM) Mhe. Mizengo akiwa katika chumba cha kupigia kura akiangalia zoezi hilo lilivyoendelea katika kituo cha kupigia kura alipotembelea kituo hicho jijini
Gaborone tarehe 30 Oktoba, 2024
|
|
Mkuu wa Misheni ya Uangalizi Uchaguzi Mkuu wa
Botswana wa SADC( SEOM) Mhe. Mizengo Pinda akiangalia mmoja wa wapiga kura
wenye uhitaji maalum akipokea karatasi ya kupigia kura huku asaidiwa na mmoja
wa watu waliokuwa katika kituo hicho kutekeleza haki yake katika moja ya kituo
cha kupiga kura alipotembelea kuangalia zoezi linaendaje katika Uchaguzi Mkuu wa Botswana tarehe 30 Oktoba, 2024
|
|
Mkuu wa Misheni ya Uangalizi Uchaguzi Mkuu wa
Botswana wa SADC (SEOM) Mhe. Mizengo Mhe. Pinda akisalimiana na Rais wa zamani
wa Botswana Mhe. Festus Mogae alipokutana naye katika kituo cha kupigia
kura alipotembelea kituo hicho kuangalia upigaji kura unavyoendeshwa tarehe 30 Oktoba, 2024
|
|
Wananchi wa Botswana wakiwa nje ya kituo cha kupigia
kura wakisubiri kuingia ndani ya kituo hicho kupiga kura zao kuchagua wabunge na wenyeviti wa mabaraza ya serikali za mitaa katika uchaguzi mkuu wa Botswana uliofanyika tarehe 30 Oktoba, 2024 |
|
Mkuu wa Misheni ya Uangalizi uchaguzi Mkuu ya
SADC (SEOM) Mhe. Mizengo akiwa na
wajumbe wa SEOM wakiwa nje ya kituo cha kupiga kura baada ya kuangalia zoezi la kupiga
kura lilivyokuwa likiendelea |
|
Mkuu wa Misheni ya Uangalizi Uchaguzi Mkuu wa
Botswana wa SADC (SEOM) Mhe. Mizengo Pinda akiwa na Rais wa zamani wa Nigeria na Mkuu wa Misheni ya uangalizi ya Umoja wa
Afrika (AU EOM) Mhe. Goodluck Jonathan walipokutana katika moja ya kituo cha
kupigia kura jijini Gaborone Botswana tarehe 30 Oktoba, 2024
|
|
Mkuu wa Misheni ya Uangalizi Uchaguzi Mkuu wa
Botswana wa SADC (SEOM) Mhe. Mizengo Pinda katika picha ya pamoja na
Rais wa zamani wa Nigeria na Mkuu wa Misheni ya uangalizi ya Umoja wa
Afrika (AU EOM) Mhe. Goodluck Jonathan (katikati) na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Said Shaib Mussa walipokutana katika moja ya kituo cha
kupigia kura jijini Gaborone Botswana tarehe 30 Oktoba, 2024
|
|
Rais wa zamani wa Nigeria na Mkuu wa Misheni ya uangalizi ya Umoja wa
Afrika (AU EOM) Mhe. Goodluck Jonathan (katikati) akizungumza na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi Uchaguzi Mkuu wa
Botswana wa SADC (SEOM) Mhe. Mizengo Pinda (kulia) walipokutana katika moja ya kituo cha
kupigia kura jijini Gaborone Botswana tarehe 30 Oktoba, 2024
|
Wananchi wa Botswana leo tarehe 30 Oktoba 2024 wamepiga kura kuchagua wabunge watakaounda Bunge la 13 la nchi hiyo na wenyeviti wa Serikali za mitaa ambao wataongoza nchi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda na timu yake wametembelea vituo vitatu vya kupigia kura katika jiji la Gaborone na vituo viwili katika kijiji cha Mochudi kujionea hali ya upigaji kura inavyoendelea.
Jumla ya Viti 61 vya ubunge na vinagombewa na wagombea kutoka vyama vinne vya siasa vya Botswana Democratic Party (BDP); Umbrella for Democratic Change (UDC); Botswana Congress Party (BCP) na Botswana Patriotic Front (BPF) ambapo Viti 609 vya mabaraza ya Serikali za mitaa vinagombewa na vyama mbalimbali vya siasa na wagombea binafsi ambao wamekidhi vigezo vilivyowekwa na Tume Huru ya Uchaguzi nchini humo (IEC).
Uchaguzi mkuu wa Botswana umeshuhudiwa na waangalizi wa kimataifa kutoka wa Misheni za Umoja wa Afrika (AUEOM) iliyoongozwa na Rais wa Mstaafu wa Nigeria, Mhe. Goodluck Jonathan, Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) iliyoongozwa na Waziri Mkuu wa Zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda, Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Madola iliyoongozwa na Mhe. Gideon Moi, na Jukwaa la Tume za Uchaguzi kutoka nchi za SADC lililoongozwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania (INEC), Mhe. Jaji Jacob Mwambegele.
Sambamba na hilo, uchaguzi huo umeshuhudiwa na Ubalozi wa Marekani, Japan, Indonesia, Namibia na waangilizi kutoka katika taasisi mbalimbali zinazoshughulikia masuala ya siasa kutoka nchini humo.
Misheni hizo zimewapongeza wananchi wa Botswana kwa kuendesha shughuli za uchaguzi kwa amani na usalama katika siku ya uchaguzi mkuu ambapo waangalizi hao wameshuhudia idadi kubwa ya wapiga kura ikiwa imejitokeza kupiga kura katika hali ya amani na usalama katika jiji la Gaborone.
Kwa mujibu wa utaratibu wa uchaguzi nchini humo chama kitakachopata zaidi ya viti 31 vya Bunge ndicho kitakachotoa Rais ambaye ataunda Serikali itakayoongoza nchi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.