Balozi wa Tanzania Nchini Malaysia Mhe Dkt. Mahadhi Juma Maalim ameongoza ujumbe wa wawekezaji kutoka Shirika la Ndege la Malaysia (AirAsia) kutembelea Ofisi za Bodi ya Utalii Tanzania (TTB ).
Katika Ofisi za TTB wamekutana na kuzungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTB Balozi Dkt. Ramadhan Dau na kuelezea dhima yao ya kuanzisha safari za ndege za moja kwa moja kutoka Malaysia kuja Tanzania na hivyo kuongeza idadi ya watalii kutoka mataifa mbalimbali duniani kuja Tanzania. Mhe. Balozi Mahadhi na ugeni wake wako nchini kuangalia jinsi ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya anga kati ya Tanzania na Malaysia. Shirika la Air Asia lina ndege 250 zinazotua katika viwanja 147 duniani. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.