Monday, November 4, 2024

MHE. PINDA ASHIRIKI MAADHIMISHO YA MIAKA 30 YA UMOJA WA WATANZANIA BOTSWANA

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda akizungumza katika Maadhimisho ya miaka Thelathini ya kuanzishwa kwa Umoja wa Watanzania wanaoishi nchini Botswana (ATB) yaliyoandaliwa na Jumuiya hiyo kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Botswana yaliyofanyika  jijini Gaborone tarehe 2 Novemba, 2024

Balozi wa Tanzania nchini Botswana mwenye makazi yake Afrika Kusini Mhe. James Bwana akizungumza katika Maadhimisho ya miaka Thelathini ya kuanzishwa kwa Umoja wa Watanzania wanaoishi nchini Botswana (ATB) yaliyoandaliwa na Jumuiya hiyo  yaliyofanyika  jijini Gaborone tarehe 2 Novemba, 2024

Mwenyekiti wa Watanzania wanaoishi nchini Botswana (ATB) Bw. Naiman Kissasi akizungumza katika Maadhimisho ya miaka Thelathini ya kuanzishwa kwa Umoja wa Watanzania wanaoishi nchini Botswana (ATB) yaliyoandaliwa na Jumuiya hiyo  yaliyofanyika  jijini Gaborone tarehe 2 Novemba, 2024

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda akizungumza na mmoja wa wazee wanachama wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Botswana katika hafla ya  Maadhimisho ya miaka Thelathini ya kuanzishwa kwa Umoja wa Watanzania wanaoishi nchini Botswana (ATB) yaliyoandaliwa na Jumuiya hiyo kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Botswana yaliyofanyika  jijini Gaborone tarehe 2 Novemba, 2024


Watanzania wanaoishi nchini Botswana wakifuatilia Maadhimisho ya miaka Thelathini ya kuanzishwa kwa Umoja wa Watanzania wanaoishi nchini Botswana (ATB) yaliyoandaliwa na Jumuiya hiyo  yaliyofanyika  jijini Gaborone tarehe 2 Novemba, 2024

Watanzania wanaoishi nchini Botswana wakifuatilia Maadhimisho ya miaka Thelathini ya kuanzishwa kwa Umoja wa Watanzania wanaoishi nchini Botswana (ATB) yaliyoandaliwa na Jumuiya hiyo  yaliyofanyika  jijini Gaborone tarehe 2 Novemba, 2024

Watanzania wanaoishi nchini Botswana wakifuatilia Maadhimisho ya miaka Thelathini ya kuanzishwa kwa Umoja wa Watanzania wanaoishi nchini Botswana (ATB) yaliyoandaliwa na Jumuiya hiyo  yaliyofanyika  jijini Gaborone tarehe 2 Novemba, 2024

Watanzania wanaoishi nchini Botswana wakifuatilia Maadhimisho ya miaka Thelathini ya kuanzishwa kwa Umoja wa Watanzania wanaoishi nchini Botswana (ATB) yaliyoandaliwa na Jumuiya hiyo  yaliyofanyika  jijini Gaborone tarehe 2 Novemba, 2024
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda akikata keki alıposhiriki katika Maadhimisho ya miaka thelathini ya Umoja wa Watanzania wanaoishi nchini Botswana (ATB) yaliyofanyika  jijini Gaborone tarehe 2 Novemba, 2024


Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda (katikati) akiongoza viongozi walioshiriki Maadhimisho ya miaka thelathini ya Umoja wa Watanzania wanaoishi nchini Botswana (ATB) kukata keki maakum ya maadhimisho hayo katika hafla iliyofanyika  jijini Gaborone tarehe 2 Novemba, 2024
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda (katikati) katika picha ya pamoja na viongozi wa Jumuiya ya  Watanzania wanaoishi nchini Botswana (ATB) katika hafla ya madhimisho ya miaka 30 ya Jumuiya hiyo iliyofanyika  jijini Gaborone tarehe 2 Novemba, 2024

Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda (katikati) katika picha ya pamoja na viongozi wa Jumuiya ya  Watanzania wanaoishi nchini Botswana (ATB) katika hafla ya madhimisho ya miaka 30 ya Jumuiya hiyo iliyofanyika  jijini Gaborone tarehe 2 Novemba, 2024

 

Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda (katikati) katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya  Watanzania wanaoishi nchini Botswana (ATB) Bw. Naiman Kissasi na Balozi wa Tanzania nchini Botswana Mhe. James Bwana (kulia) katika hafla ya madhimisho ya miaka 30 ya Jumuiya hiyo iliyofanyika  jijini Gaborone tarehe 2 Novemba, 2024

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda ameshiriki  Maadhimisho ya miaka Thelathini ya kuanzishwa kwa Umoja wa Watanzania wanaoishi nchini Botswana (ATB) yaliyoandaliwa na Jumuiya hiyo kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Botswanayaliyofanyika  jijini Gaborone tarehe 2 Novemba, 2024.


Akizungumza katika hafla hiyo Mhe. Pinda amesema Serikali ya Tanzania inabuni mbinu na mikakati mahsusi kwa lengo la kuwawezesha Diaspora kuendelea kuchangia zaidi katika maendeleo ya taifa kupitia maeneo ya kimkakati na kuwasihi wachangamkie fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji zinazopatikana nyumbani.

Mhe. Pinda pia amewasihi Diaspora hao kutumia mifumo rasmi ya kutuma fedha nyumbani (remittances) ili kuiwezesha Serikali kuwa na taarifa na takwimu sahihi za mchango wa disapora kwa Taifa lao.
“Nichukue nafasi hii kuwajulisha kuwa Serikali iko katika hatua ya maandalizi ya Dira ya Maendeleo ya Mwaka 2050, niwasihi Diaspora mtumie ujuzi na uzoefu mlioupata huku ugenini kwa kutoa maoni yenu kwa ajili ya Dira ya mpya ya Maendeleo ya Mwaka 2050 kwani kwa kufanya hivyo mtaliwezesha Taifa kupata dira itakayolifikisha kule  kunakotarajiwa, alisisitiza Mhe. Pinda.

Pia amewasihi Diaspora hao kuendelea kujisajili katika mfumo wa kidijitali ujulikanao kama Diaspora Digital Hub (DDH) ili kuiwezesha Serikali kuwa na takwimu sahihi za Diaspora wake na kufanikisha maamuzi ya kisera kwa kuzingatia idadi na mchango wa dispora kwa Taifa.

Mhe. Pinda amewaomba Disapora hao wa Botswana kuendelea kuitetea nchi yao, kudumudisha mila, desturi na tamaduni zao, kupendana, kusadiana, kuinuana na kutatua changamoto kwa pamoja huku wakiendelea kushirikiana na Balozi wao aliyepo Pretoria, Afrika Kusini kama mlezi wao na kufuata sheria za nchi mwenyeji na wakumbuke kuwa nyumbani kwao ni Tanzania. 

Maadhimisho hayo yalihudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Said Shaib Mussa, Balozi wa Tanzania Afrika Kusini anayewakilisha pia nchi za Botswana na Lesotho Mhe. James  Bwana; Balozi Dkt. Salim Omar Othman; Mwambata wa Biashara na Uwekezaji katika Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini  Bi. Happyness  Godfrey pamoja na Watanzania wanaoishi nchini Botswana.

Maadhimisho hayo yalitanguliwa na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa ATB ambao uliambatana na Uchaguzi wa Viongozi wa ATB kwa Muhula mpya ambapo Bw. Naiman Kissasi alichaguliwa kuwa Mwenyekiti , Peace Byengozi alichaguliwa kuwa Katibu pamoja na Viongozi wengine wa Kamati Tendaji. Kupitia Maadhimisho hayo Benki ya CRDB pamoja na Kampuni ya KC LAND walipata fursa ya kunadi huduma zao mahususi kwa ajili ya Diaspora wa nchini Botswana.

Mhe. Pinda yuko nchini Botswana kwa ajili ya kuongoza misheni ya Uangalizi ya Uchaguzi. Mkuu wa Botswana ya SADC (SEOM) uliofanyika nchini humo tarehe 30 Oktoba, 2024 ambako Chama cha Upinzani cha UDC kilipata ushindi wa zaidi ya viti 31 vya Bunge la nchi hiyo na hivyo kukiondoa madarakani chama tawala cha BDP kilichokuwa kikiongozwa na aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Mokgweetsi Masisi

Friday, November 1, 2024

MISHENI ZA UANGALIZI UCHAGUZI MKUU BOTSWANA ZATOA TAARIFA ZA AWALI KUHUSU UCHAGUZI HUO ULIVYOENDESHWA


Wakuu wa Misheni ya Uangalizi uchaguzi mkuu wa Botswana kutoka SADC -SEOM Mhe. Mizengo Pinda (katikati aliyekaa) akiwa na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi uchaguzi ya Umoja wa Afrika (AU-EOM) Mhe. Goodluck Jonathan (wa pili kushoto) na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi uchaguzi kutoka Jukwaa la Tume za Uchaguzi SADC(SADC -ECF) Jaji Jacob Mwambegele (wa pili kulia) wakiwa katika meza kuu

 

Mkuu wa Misheni ya Uangalizi uchaguzi ya Umoja wa Afrika (AU-EOM) Mhe. Goodluck Jonathan (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi uchaguzi mkuu wa Botswana wa SADC -SEOM Mhe. Mizengo Pinda

Wakuu wa Misheni ya Uangalizi uchaguzi mkuu wa Botswana kutoka SADC -SEOM Mhe. Mizengo Pinda (kulia) akiwa na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi uchaguzi ya Umoja wa Afrika (AU-EOM) Mhe. Goodluck Jonathan (katikati) na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi uchaguzi kutoka Jukwaa la Tume za Uchaguzi za SADC Jaji Jacob Mwambengele (kushoto) katika meza kuu wakati wa kuwsilisha tarifa za misheni zzao jijini Gaborone tarehe 01 November, 2024.

Mkuu wa Misheni ya Uangalizi uchaguzi mkuu wa Botswana wa SADC -SEOM Mhe. Mizengo Pinda (kulia) akiwasilisha tarifa ya SEOM

 

wageni waalikwa wakisikiliza taarifa za awali kutoka kwa waangalizi wa kimataifa wa uchaguzi mkuu wa Botswana zilizowasilishwa jijini Gaborone tarehe 01 Novemba 2024

Waangalizi wa SEOM  wakifuatilia tarifa ya wali iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkuu wa misheni hiyo

wageni waalikwa wakisikiliza taarifa za awali kutoka kwa waangalizi wa kimataifa wa uchaguzi mkuu wa Botswana zilizowasilishwa jijini Gaborone tarehe 01 Novemba 2024

 

Wakuu wa Misheni ya Uangalizi uchaguzi mkuu wa Botswana kutoka SADC -SEOM Mhe. Mizengo Pinda (katikati aliyekaa) akiwa na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi uchaguzi ya Umoja wa Afrika (AU-EOM) Mhe. Goodluck Jonathan (wa pili kushoto) na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi uchaguzi kutoka Jukwaa la Tume za Uchaguzi SADC(SADC -ECF) Jaji Jacob Mwambegele (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini Botswana baada ya misheni hizo kutoa taarifa za awali za mishenio zao jijini Gaborone tarehe 01 Novemba, 2024

Mkuu wa Misheni ya Uangalizi uchaguzi mkuu wa Botswana wa SADC -SEOM Mhe. Mizengo Pinda (katikati) akiwa na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi uchaguzi ya Umoja wa Afrika (AU-EOM) Mhe. Goodluck Jonathan (wa pili kushoto) na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi uchaguzi kutoka Jukwaa la Tume za Uchaguzi SADC(SADC -ECF)Jaji Jacob Mwambegele (wa pili kulia) na Katibu Mtendaji wa SADC Mhe. Elias Magosi (kulia) na wajumbe wa SEOM waliosimama

Wakuu wa Misheni ya Uangalizi uchaguzi mkuu wa Botswana kutoka SADC -SEOM Mhe. Mizengo Pinda (katikati aliyekaa) akiwa na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi uchaguzi kutoka Jukwaa la Tume za Uchaguzi SADC(SADC -ECF) Jaji Jacob Mwambegele (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na wajumbe wa SEOM na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Botswana Mhe. James Bwana (kulia)  jijini Gaborone tarehe 01 Novemba, 2024


Misheni za Uangalizi uchaguzi mkuu wa Botswana kutoka Jumumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC-SEOM), Umoja wa Afrika (AU_EOM) na Jukwaa la Tume za Uchaguzi la SADC (ECF) zimetoa taarifa za awali kuhusiana na uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo uliofanyika tarehe 30 Oktoba 2024.

Akıwasilisha taarifa hiyo jijini Gaborone, kwa upande wa misheni ya  SADC-SEOM  Mkuu wa Misheni hiyo Mhe.Mizengo Pinda amesema katika uchaguzi huo SEOM imeona kuwa mazingira ya kisiasa nchini humo yalikuwa ya utulivu na yenye amani kuanzia kipindi cha kampeni, siku ya kupiga kura na hata baada ya kupiga kura.

“SEOM iliona kuwa shughuli za kisiasa kuanzia hatua za awali kuelekea siku ya uchaguzi na siku ya kupiga katika Jamhuri ya Botswana zilifanyika kwa amani na kwa utulivu mkubwa na hivyo kuwawezesha wananchi wa Botswana kutumia haki yao ya kimsingi ya kidemokrasia ya kupiga kura, kwa utulivu na amani pia,” alisisitiza Mhe. Pinda.

Ameongeza kuwa SEOM ilishuhudia vyama vya siasa na wagombea binafsi nchini humo wakiendesha kampeni kwa uhuru na amani  ambazo zilifanyika kupitia mikutano, nyumba kwa nyumba, midahalo kwa wagombea wa urais , mahojiano na mijadala katika vyombo vya Habari na mabango katika sehemu mbalimbali nchini humo ambapo amesema katika shughuli zote hizo hakukuwa na vurugu wala fujo hali iliyoonesha uvumilivu wa hali ya juu wa kisiasa na ukomavu kwa watu wa Botswana.

Akiongelea zoezi la upigaji kura la awali lililofanyika tarehe 19 na 26 Oktoba 2024, Mhe.Pinda alisema kuwa zoezi hilo liliendeshwa kwa amani licha ya kuwepo kwa tukio la mpiga kura mmoja kuondoka na karatasi ya kupigia kura na baadhi ya vyama kulalamika kuondolewa kwa mabango yao na kuongeza kuwa askari polisi walikuwepo  katika mikutano ya kampeni katika maeneo yote na kuliendelea kuwa na amani hata pale ambapo hakukuwa na askari polisi.

Amesema SEOM  iliangalia masuala mbalimbali ya muhimu kabla na wakati wa uchaguzi, ikiwa ni pamoja na hali ya siasa na usalama chini humo, usimamizi wa uchaguzi, ripoti za vyombo vya habari kuhusu uchaguzi, na uwakilishi wa jinsia na Makundi maalum ambayo yote yametekelezwa kwa kiasi kikubwa.

Akiwasilisha taarifa ya misheni yake Mkuu wa Misheni ya AU_EOM na Rais wa zamani wa Nigeria Mhe. Goodluck Jonathan amesema AU pia inawapongeza wananchi wa Botswana  kwa kuonyesha ukomavu wa kisiasa na uvumilivu wa hali ya juu katika kipindi chote cha uchaguzi, na kuwasihi kuendelea hivyo kwakuwa siasa si uadui bali ni ushindani wa hoja na kupigiana kura zitakazoamua kupitia uchaguzi.

Naye Mkuu wa misheni ya SADC _ECF na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania Mhe. Jaji Jacob Mwambegele ametoa wito kwa wadau mbalimbali nchini humo kuendelea kuwa watulivu na wavumilivu wakati mamlaka za usimamizi wa uchaguzi zikikamilisha matokeo ya uchaguzi kabla ya kutangazwa rasmi, akiwaomba kuendelea kuhamasisha amani, uvumilivu, na utulivu kupitia majukwaa mbalimbali katika kipindi hiki cha baada ya uchaguzi.

Kulingana na Misingi na Miongozo ya SADC inayosimamia uchaguzi wa kidemokrasi iliyorekebishwa mwaka 2021, misheni hizo za SADC na AU zitatoa taarifa ya mwisho kuhusu uchaguzi siku 30 baada ya kutoa taarifa ya awali ambayo itawasilishwa kwa Serikali ya nchi hiyo ili kufanyia kazi mapendekezo ya taarifa hizo na hivyo kuboresha mazingira ya ufanyaji uchaguzi mkuu mwingine ujao nchini humo.

SEOM ilipeleka waangalizi 72 waliotoka katika nchi 10 wanachama wa SADC  ambao walikwenda katika wilaya 9 za kiutawala za nchini humo za Kati, Ghanzi; Kgalagadi; Kgatleng; Kweneng; Ngamiland; Kaskazini Mashariki; Kusini na Kusini Mashariki.

Siku ya Uchaguzi tarehe 30 Oktoba, 2024 Misheni hizo zilitembelea vituo vya uchaguzi kuangalia namna zoezi linavyoendeshwa na pia zilishuhudia awamu ya pili ya upigaji kura wa awali uliofanyika tarehe 26 Oktoba,2024.