Monday, August 21, 2017
Thursday, August 17, 2017
Balozi wa Tanzania nchini Uturuki awasilisha Hati za Utambulisho
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Balozi wa Tanzania nchini Uturuki awasilisha Hati za Utambulisho
Mhe. Prof. Elizabeth K. KIONDO, Balozi wa Kwanza Mteule wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania nchini Uturuki Jumatano ya tarehe 16 Agosti 2017,
amewasilisha Hati zake za Utambulisho pamoja na zile za Kukoma kwa Muda wa
Mtangulizi wake kwa Mheshimiwa Recep Tayyip Erdoǧan, Rais wa Jamhuri ya Uturuki. Kitendo hicho
kinamfanya Mhe. Kiondo kuwa Balozi wa kwanza mkaazi wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania nchini humo.
Katika hafla hiyo Mhe. Balozi Kiondo alipata fursa ya kufanya mazungumzo
na Mheshimiwa Rais Erdoǧan kuhusu namna ya kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizo mbili katika
maeneo ya uwekezaji, biashara, afya, Elimu, na mengineyo. Aidha, Mhe. Balozi
Kiondo alimfahamisha Mheshimiwa Rais Erdoǧan kuwa Ubalozi utakuwa kiungo muhimu katika
kuongeza kasi ya utekelezaji wa makubaliano mbalimbali yaliyofikiwa wakati wa
ziara yake nchini Tanzania mwezi Januari 2017 ambapo mikataba na makubaliano
yapatayo tisa yalisainiwa.
Kufunguliwa kwa Ubalozi mpya wa Tanzania nchini Uturuki na kuanza
kufanya kazi kunatoa fursa muhimu kwa wananchi wa mataifa hayo mawili kuongeza
shughuli za kiuchumi hususan biashara kwa manufaa ya pande zote mbili.
Mhe. Balozi anatoa rai kwa Watanzania kujipanga vizuri na kuchangamkia
fursa mbalimbali hususan za kibiashara zinazotokana na kuendelea kuimarika kwa
mahusiano kati ya Tanzania na uturuki.
Mwisho-
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 17
Agosti 2017
Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo, Balozi
Mteule wa Tanzania nchini Uturuki akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mheshimiwa Recep Tayyip Erdoǧan, Rais wa Jamhuri ya Uturuki.
|
Mhe. Balozi Kiondo akiagana na
Mheshimiwa Rais Erdoǧan, baada ya kufanya mazungumzo kuhusu mahusiano ya Tanzania
na Uturuki.
|
Picha ya pamoja |
Monday, August 14, 2017
RAIS WA MISRI AWASILI NCHINI NA KUPOKEWA NA MWENYEJI WAKE RAIS DKT. MAGUFULI
Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi akikagua gwaride la Heshima mara baada ya nyimbo za Taifa kupigwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam. |
Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi akiangalia vikundi vya ngoma za asili mara baada ya kuwasili nchini. |
Subscribe to:
Posts (Atom)