Saturday, May 28, 2022

BALOZI KOMBO, DKT. MAKAKALA WAJADILI CHANGAMOTO ZA UHAMIAJI

Na Mwandishi wetu, 

Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo amekutana kwa mazungumzo na Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Tanzania, Dkt. Anna Makakala katika Ofisi Ndogo za Uhamiaji Jijini Dar es Salaam. 

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao walijadilia masuala mbalimbali yanayowahusu Watanzania wanaoishi nchini Italia, Ugiriki na maeneo mengine ya uwakilishi yanayoratibiwa na Ubalozi wa Tanzania uliopo Rome.  

Masuala mengine yaliyogusiwa katika mazungumzo yao ni changamoto mbalimbali za WanaDiaspora wanazozikabili nchini Italia na kwingineko kuhusu masuala ya Uhamiaji. 

Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Tanzania, Dkt. Alimuahidi Balozi Kombo kufanikisha utatuzi wa changamoto zote hizo kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na ofisi za Balozi za Tanzania ulimwenguni kote ikiwemo Ubalozi wa Tanzania nchini Italia.

Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo katika picha ya pamoja na Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Tanzania, Dkt. Anna Makakala baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao yaliyofanyika katika Ofisi Ndogo za Uhamiaji Jijini Dar es Salaam 



Friday, May 27, 2022

WAZIRI MULAMULA AMWAKILISHA RAIS SAMIA MKUTANO WA DHARURA AU

Na Mwandishi wetu, Malabo

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 15 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) unaofanyika Malabo, Equatorial Guinea tarehe 27 na 28 Mei, 2022.

Mkutano huo pamoja na mambo mengine, umejadili ajenda kuu mbili ambazo ni majanga na huduma za kibinadamu, masuala ya Ugaidi na Mabadiliko ya Serikali yasiyozingatia misingi ya Katiba. 

Akiongea wakati wa Mkutano huo, Balozi Mulamula amesema anamwakilisha Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika Mkutano huo ulioitishwa na na Umoja wa Afrika (AU) kwa lengo la kuangalia na kujadili maajanga na huduma za kibinadamu pamoja na ugaidi.

“AU wameitisha mkutano huu kwa lengo la kujadili namna ya kukabiliana na majanga haya na jinsi gani Bara la Afrika linaweza kuwa na mkakati wa pamoja wa kukabiliana na majanga haya, na tunategemea baada ya kikao cha leo tutapata azimio la kukabidiliana na majanga haya katika bara letu la Afrika,” amesema Balozi Mulamula.

Kuhusu masuala ya Ugaidi, Balozi Mulamula ameongeza kuwa, Mkutano wa kesho tarehe 28 Mei, 2022 mkutano utaendelea kuangalia masuala ya kigaidi na kuona ni jinsi gani Bara la Afrika linasimama kwa umoja wake kupambana na majanga ya kigaidi.

Awali akifungua Mkutano huo, Rais wa Senegali ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mkutano huo, Mhe. Macky Sall amezisihi nchi za Afrika kuwa na umoja ambao utaziwezesha kukabiliana na majanga ya kibinadamu na mapambano dhidi ya ugaidi kwa urahisi zaidi.

Mhe. Sall amezitaka nchi za Afrika kuimarisha ushirikiano na mshikamano na kujenga uwezo wa kila nchi ili kuweza kukabiliana na majanga mbalimbali ya asili na wakati huo huo, kushughulikia changamoto za ulinzi na usalama ili kutozalisha wakimbizi na wahamaji ikiwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano na kuunda Jeshi la Afrika (ASF) na Brigedi za kikanda pamoja na kuanzisha Vikosi Maalum    kushughulikia Changamoto za Ugaidi.

Balozi Mulamula katika mkutano huo, ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Mhe. Innocent Shiyo ambaye anawakilisha pia Umoja wa Afrika, Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Naimi Aziz pamoja na watumishi wengine waandamizi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa tayari kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 15 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) unaofanyika Malabo, Equatorial Guinea tarehe 27 na 28 Mei, 2022

Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe. Abiy Ahmed Ali akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula walipokutana katika Mkutano wa 15 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) unaofanyika Malabo, Equatorial Guinea

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Bw. Moussa Faki Mahamat akihutubia katika Mkutano wa 15 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) unaofanyika Malabo, Equatorial Guinea

Rais wa Senegal na Mwenyekiti wa Mkutano wa 15 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU), Mhe. Macky Sall akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano huo leo Jijini Malabo, Equatorial Guninea

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na baadhi ya ujumbe wa Tanzania ulioshiriki katika Mkutano wa 15 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) unaofanyika Malabo, Equatorial Guinea

Rais wa Burundi, Mhe. Evariste Ndayishimiye katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula ambaye anamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika Mkutano huo

Sehemu ya Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ukiongozwa na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Mhe. Innocent Shiyo,  ambaye pia anawakilisha Umoja wa Afrika, Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Naimi Aziz pamoja na watumishi wengine waandamizi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mkutano ukiendelea

Wakuu wa Nchi na Serikali pamoja na Wawakilishi wa Wakuu wa Nchi na Serikali wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa mkutano wa Mkutano wa 15 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) unaofanyika Malabo, Equatorial Guinea

Sehemu ya Wakuu wa Nchi na Serikali pamoja na Wawakilishi wa Wakuu wa Nchi na Serikali wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa mkutano wa Mkutano wa 15 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) unaofanyika Malabo, Equatorial Guinea




VACANCY ANNOUNCEMENT


 

VACANCY ANNOUNCEMENT


 

Thursday, May 26, 2022

Canada Yaahidi Kushirikiana na Tanzania




Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk N. Mbarouk akiwa katika mazungumzo na  Katibu wa Bunge wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, Mhe. Robert Oliphant yaliyofanyika jijini Dar Es Salaam



 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk N. Mbarouk na Katibu wa Bunge wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, Mhe. Robert Oliphant wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wao baada ya mazungumzo yaliyofanyika jijini Dar Es Salaam.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiwa katika mazungumzo na Katibu wa Bunge wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, Mhe. Robert Oliphant yaliyofanyika jijini Dar Es Salaam

Katibu wa Bunge wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, Mhe. Robert Oliphant  akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye

Ujumbe wa Tanzania katika ukifuatilia mazungumzo kati ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye na Katibu wa Bunge wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, Mhe. Robert Oliphant. Wakwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga na anayefuatia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bi. Talha Mohammed

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye na Katibu wa Bunge wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, Mhe. Robert Oliphant wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wao baada ya mazungumzo yaliyofanyika jijini Dar Es Salaam

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima akiwa katika mazungumzo na Katibu wa Bunge wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, Mhe. Robert Oliphant yaliyofanyika jijini Dar Es Salaam.

Katibu wa Bunge wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, Mhe. Robert Oliphant  akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima jijini Dar Es Salaam.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na  Katibu wa Bunge wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, Mhe. Robert Oliphant yaliyofanyika jijini Dar Es Salaam

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga akieleza jambo wakati wa mazungumzo kati ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima na  Katibu wa Bunge wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, Mhe. Robert Oliphant

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajimana  na Katibu wa Bunge wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, Mhe. Robert Oliphant wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wao baada ya mazungumzo yaliyofanyika jijini Dar Es Salaam

Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Bibi Mary Makondo akiwa katika mazungumzo na Katibu wa Bunge wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, Mhe. Robert Oliphant yaliyofanyika jijini Dar Es Salaam.

Ujumbe wa Katibu wa Bunge wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, Mhe. Robert Oliphant ambaye unamjumuisha Balozi wa nchi hiyo hapa nchini, Mhe. Pamela O'Donnell (wa kwanza kulia) ukifutatilia mazungumzo kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Bibi Mary Makondo na Katibu wa Bunge wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, Mhe. Robert Oliphant

Katibu wa Bunge wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, Mhe. Robert Oliphant  akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Bibi Mary Makondo

Mazungumzo kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Bibi Mary Makondo na Katibu wa Bunge wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, Mhe. Robert Oliphant yanaendelea.







 

WATANZANIA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA UFADHILI WA MASOMO ZINAZOTANGAZWA NA SERIKALI

Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme amewataka Watanzania kuendelea kuchangamkia fursa mbalimbali zikiwemo za ufadhali wa masomo zinazotangazwa na Serikali ili kunufaika nazo.


Balozi Mndeme ametoa rai hiyo leo tarehe 26 Mei 2022 jijini Dodoma alipokutana na wawakilishi wa vijana 26 wanaokwenda nchini Marekani kushiriki mafunzo chini ya Program ya YALI  kwa lengo la kuwaaga.


Amesema kuwa, Serikali kupitia Wizara mbalimbali ikiwemo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeendelea kutangaza fursa mbalimbali zikiwemo za ajira na ufadhili wa masomo zinazopokelewa nchini kutoka nchi mbalimbali lakini bado mwitikio wa Watanzania wa kuchangamkia fursa hizo ni mdogo.


“Wizara imekuwa na utaratibu wa kutangaza fursa nyingi za ufadhili wa masomo zinazopokelewa kutoka nchi mbalimbali tunazoshirikiana nazo. Hata hivyo, bado fursa hizi hazijachangamkiwa ipasavyo. Nawaomba Watanzania mzichangamkie fursa hizi pale zinapotangazwa ili zitunufaishe” alisema Balozi Mndeme


Aidha, Balozi Mndeme aliwapongeza vijana hao kwa kufanikiwa kuchaguliwa kushiriki program hiyo ambayo inaheshimika duniani na kuwaeleza kuwa ni fursa nzuri kwao kuitumia kwa ajili ya kujifunza masuala mbalimbali yakiwemo yanayohusu Uongozi ili kupitia wao vijana wengine wengi wa Tanzania wanufaike. Pia aliwaasa kuwa Mabalozi wazuri wa Tanzania, kuzingatia nidhamu na kutanguliza maslahi ya nchi mbele wakati wote wakiwa nchini Marekani.


“Nawapongeza sana kwa kufanikiwa kupata fursa hii. Wizara inafurahi kuona vijana wa Kitanzania mmepata fursa hii kwani pamoja na kuwajenga pia ni ushahidi wa uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Marekani. Nawaasa mkawe mabalozi wazuri wa Tanzania mzingatie nidhamu ili kulinda heshima na taswira nzuri ya nchi yetu” alisema Balozi Mndeme.


Kwa upande wao vijana hao waliishukuru na kuipongeza Wizara kwa ushirikiano iliowapatia na kuahidi kuzingatia mafunzo yote watakayoyapata wakiwa  Marekani kwa maslahi mapana ya nchi.


Program ya YALI (Young African Leaders Initiative) ilianzishwa na Serikali ya Marekani mwaka 2010 kwa lengo la kuwawezesha vijana kutoka mataifa ya Afrika kwenda nchini humo kujifunza masuala mbalimbali ya kuwajengea uwezo katika Uongozi. Vijana hao 26 wamechaguliwa kati ya Vijana wa Kitanzania 700 walioomba kujiunga na Program hiyo kwa mwaka 2022. 

Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme akizungumza wakati wa kikao kifupi cha kuwaaga  Vijana 26 wa Kitanzania (hawapo pichani) waliopata fursa ya kushiriki mafunzo nchini Marekani kupitia Program ya Young African Leaders Initiative (YALI)  kwa mwaka 2022. Pamoja na mambo mengine aliwaasa vijana hao kuwa mabalozi wazuri wa Tanzania  nchini Marekani ili kulinda heshima ya nchi. Kikao hicho kimefanyika jijini Dodoma tarehe 26 Mei 2022.

Mmoja wa vijana watakaoshiriki program ya YALI Bi. Victoria akizungumza wakati wa mkutano kati yao na Balozi Mndeme (hayupo pichani)
Sehemu ya wawakilishi wa vijana 26 wa Kitanzania watakaoshiriki program ya YALI nchini Marekani wakimsikiliza Balozi Mndeme (hayupo (ichani)
Sehemu nyingine ya vijana hao wakati wa mkutano kati yao na Balozi Mndeme
Vijana watakaoshiriki program ya YALI nchini Marekani wakifuatilia mazungumzo kati yao na Balozi Mndeme
Sehemu ya vijana hao wakati wa kikao cha kuwaaga 
Vijana watakaoshiriki program ya YALI nchini Marekani wakimsikiliza Balozi Mndeme alipozungumza nao kwa ajili ya kuwaaga
Balozi Mndeme akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wawakilishi wa vijana 26 watakaoshiriki program ya YALI nchini Marekani
Picha ya pamoja
Picha ya pamoja



 

Wednesday, May 25, 2022

WAZIRI MULAMULA ASHIRIKI MKUTANO WA BARAZA LA MAWAZIRI AU

Na Mwandishi wetu, Malabo


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) ameshiriki Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje la Umoja wa Afrika (AU) ulioanza leo Jijini Malabo, Equatorial Guinea.

Kufanyika kwa mkutano huo ni utekelezaji wa maamuzi ya Mkutano wa 35 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika uliofanyika tarehe 6 - 7 Februari 2022 Jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Mkutano wa Baraza la Mawaziri ulitanguliwa na Mkutano wa Kisekta wa Mawaziri wanaoshughulika na Wakimbizi, Wahamaji na Majanga ya Kibinadamu uliofanyika kuanzia tarehe 23 - 24 Mei, 2022 Jijini Malabo.

Mkutano huo pamoja na mambo mengine, jukumu lake kubwa ni kuandaa Mkutano Maalum wa 16 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu majanga ya kibinadamu pamoja na masuala ya mapambano dhidi ya ugaidi na mabadiliko ya serikali yasiyozingatia Katiba unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 – 28 Mei, 2022 Jijini Malabo.

Akiongea wakati wa Ufunguzi wa Mkutano huo, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Bw. Moussa Faki Mahamat alisema kuwa mkutano huo ni mahsusi katika kujadili changamoto mbalimbali za majanga ya kibinadamu pamoja na mapambano dhidi ya ugaidi na mabadiliko ya Serikali yasiyozingatia katiba

“Mkutano huu unafanyika wakati Afrika linapita katika changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na za majanga ya kibinadamu,” alisema Bw. Mahamat

Aidha, Bw. Mahamat aliongeza kuwa ugaidi bado ni changamoto na mabadiliko ya Serikali yasioyofuata misingi ya katiba ambayo yametokea miaka ya hivi karibuni yamerudisha nyuma taratibu za kidemokrasia katika chaguzi katika Bara la Afrika. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akishiriki Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje la Umoja wa Afrika (AU) ulioanza leo Jijini Malabo, Equatorial Guinea


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiteta jambo na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi, Balozi Alain Nyamitwe wakati wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje la Umoja wa Afrika (AU) ulioanza leo Jijini Malabo, Equatorial Guinea


Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Mhe. Nancy Gladys Tembo akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje la Umoja wa Afrika (AU) ulioanza leo Jijini Malabo, Equatorial Guinea


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipata maelezo kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Balozi Innocent Shiyo kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje la Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika Jijini Malabo, Equatorial Guinea


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipata ufafanuzi kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Balozi Innocent Shiyo (kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Naimi Aziz kabla ya kuanza kwa mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje la Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika Jijini Malabo, Equatorial Guinea


Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Bw. Moussa Faki Mahamat akiwasilisha hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje la Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika Jijini Malabo, Equatorial Guinea 


Waziri wa Mambo ya Nje wa Senegal, Mhe. Aïssata Tall Sall akihutubia washiriki wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje la Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika Jijini Malabo, Equatorial Guinea  


Sehemu ya Ujumbe wa Tanzania ukishiriki katika Mkutano


Mkutano ukiendelea 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya ujumbe wa Tanzania baada ya kumalizika kwa mkutano


Mawaziri wa Mambo ya Nje Mambo ya Nje wa Umoja wa Afrika (AU) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mkutano wao