Wednesday, May 25, 2022

WAZIRI MULAMULA ASHIRIKI MKUTANO WA BARAZA LA MAWAZIRI AU

Na Mwandishi wetu, Malabo


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) ameshiriki Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje la Umoja wa Afrika (AU) ulioanza leo Jijini Malabo, Equatorial Guinea.

Kufanyika kwa mkutano huo ni utekelezaji wa maamuzi ya Mkutano wa 35 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika uliofanyika tarehe 6 - 7 Februari 2022 Jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Mkutano wa Baraza la Mawaziri ulitanguliwa na Mkutano wa Kisekta wa Mawaziri wanaoshughulika na Wakimbizi, Wahamaji na Majanga ya Kibinadamu uliofanyika kuanzia tarehe 23 - 24 Mei, 2022 Jijini Malabo.

Mkutano huo pamoja na mambo mengine, jukumu lake kubwa ni kuandaa Mkutano Maalum wa 16 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu majanga ya kibinadamu pamoja na masuala ya mapambano dhidi ya ugaidi na mabadiliko ya serikali yasiyozingatia Katiba unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 – 28 Mei, 2022 Jijini Malabo.

Akiongea wakati wa Ufunguzi wa Mkutano huo, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Bw. Moussa Faki Mahamat alisema kuwa mkutano huo ni mahsusi katika kujadili changamoto mbalimbali za majanga ya kibinadamu pamoja na mapambano dhidi ya ugaidi na mabadiliko ya Serikali yasiyozingatia katiba

“Mkutano huu unafanyika wakati Afrika linapita katika changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na za majanga ya kibinadamu,” alisema Bw. Mahamat

Aidha, Bw. Mahamat aliongeza kuwa ugaidi bado ni changamoto na mabadiliko ya Serikali yasioyofuata misingi ya katiba ambayo yametokea miaka ya hivi karibuni yamerudisha nyuma taratibu za kidemokrasia katika chaguzi katika Bara la Afrika. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akishiriki Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje la Umoja wa Afrika (AU) ulioanza leo Jijini Malabo, Equatorial Guinea


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiteta jambo na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi, Balozi Alain Nyamitwe wakati wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje la Umoja wa Afrika (AU) ulioanza leo Jijini Malabo, Equatorial Guinea


Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Mhe. Nancy Gladys Tembo akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje la Umoja wa Afrika (AU) ulioanza leo Jijini Malabo, Equatorial Guinea


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipata maelezo kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Balozi Innocent Shiyo kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje la Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika Jijini Malabo, Equatorial Guinea


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipata ufafanuzi kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Balozi Innocent Shiyo (kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Naimi Aziz kabla ya kuanza kwa mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje la Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika Jijini Malabo, Equatorial Guinea


Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Bw. Moussa Faki Mahamat akiwasilisha hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje la Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika Jijini Malabo, Equatorial Guinea 


Waziri wa Mambo ya Nje wa Senegal, Mhe. Aïssata Tall Sall akihutubia washiriki wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje la Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika Jijini Malabo, Equatorial Guinea  


Sehemu ya Ujumbe wa Tanzania ukishiriki katika Mkutano


Mkutano ukiendelea 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya ujumbe wa Tanzania baada ya kumalizika kwa mkutano


Mawaziri wa Mambo ya Nje Mambo ya Nje wa Umoja wa Afrika (AU) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mkutano wao  



No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.