Thursday, May 12, 2022

TANZANIA, JAMAICA KUONGEZA MAENEO MAPYA YA USHIRIKIANO

Na Mwandishi Wetu, Dar 

Serikali ya Tanzania na Jamaica zimeahidi kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano katika sekta za utalii, biashara na uwekezaji pamoja na elimu kwa maslahi mapana ya pande zote mbili.

Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) wakati alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Jamaica Mhe. Kamina Smith katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

“Leo nimekutana na Mhe. Smith na tumejadili na kudhamiria kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano katika sekta za utalii, biashara na uwekezaji, elimu, uwezeshaji wa wanawake kiuchumi pamoja na vijana 

Tanzania na Jamaica tumedhamiria kufanya kazi kwa karibu katika kutafuta njia bora ya kufungua fursa mpya kwa maslahi ya mataifa yote mawili,” alisema Balozi Mulamula 

Nae Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Jamaica Mhe. Kamina Smith amesema kuwa Tanzania imekuwa na uhusiano mzuri na Jamaica ambapo uhusiano huo umekuwa ni chachu ya maendeleo inayopelekea kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano katika sekta za utalii, biashara na uwekezaji na elimu.

“Ushirikiano uliopo baina ya mataifa yetu mawili umekuwa chachu ya maendeleo na lengo la ushirikiano huu ni kukuza, kuendeleza na kuimarisha uchumi wetu,” alisema Mhe. Smith

Katika tukio jingine, Waziri Mulamula amekutana na Kufanya Mazungumzo na Balozi wa Misri nchini, Mhe. Mohamed Gaber Abouelwafa.  

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili masuala ya kuendeleza na kuimarisha uhusiano katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara na uwekezaji, elimu, pamoja na afya. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Jamaica, Mhe. Kamina Smith katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Jamaica, Mhe. Kamina Smith akimueleza jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mazungumzo ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Jamaica, Mhe. Kamina Smith yakiendelea katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimsikiliza Balozi wa Misri nchini, Mhe. Mohamed Gaber Abouelwafa walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza Balozi wa Misri nchini, Mhe. Mohamed Gaber Abouelwafa walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mazungumzo ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Balozi wa Misri nchini, Mhe. Mohamed Gaber Abouelwafa yakiendelea katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam



No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.