Monday, May 23, 2022

Zanzibar Mwenyeji wa Tamasha la Utamaduni na Sanaa la Afrika

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma M. Rajab ameshiriki kwenye ufunguzi wa Tamasha la Utamaduni na Sanaa la Afrika 2022 (FESTAC 2022) linalofanyika katika viwanja vya Hotel ya Verde Zanzibar kuanzia tarehe 23 hadi 29 Mei 2022.

Tamasha hilo limefunguliwa na Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Mhe. Simai Mohammed Said, akimwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Hussein Ali Mwinyi. 

Viongozi wa Serikali na Binafsi kutoka ndani na nje ya nchi wanashiriki tamasha hilo wakiwemo Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini.

Tamasha hilo lilianzishwa mwaka 1966 na hufanyika Barani Afrika kwa lengo la kuwaunganisha pamoja Waafrika kusherehekea sanaa, urithi na mila za Kiafrika na linafanyika sambamba na maonesho ya biashara, uwekezaji na utalii.

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Simai Mohammed Said akisoma hotuba ya ufunguzi ya Tamasha la Utamaduni na Sanaa la Afrika 2022 (FESTAC 2022) linalofanyika Zanzibar kuanzia tarehe 23 hadi 29 Mei 2022. akimwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Hussein Ali Mwinyi. 

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma M. Rajab (katikati) akiwa na Waziri Mstaafu wa Viwanda, Biashara na Masoko, Balozi Amina Mohammed (kulia)  na Mshindi wa Tuzo ya Nobel, Prof. Abdulrazak Gurnah wakati wa hafla ya ufunguzi wa Tamasha la Utamaduni na Sanaa la Afrika 2022 (FESTAC 2022) mjini Zanzibar
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma M. Rajab (wa pili kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabiti Kombo  wakiwa katika picha ya pamoja na  watumishi wa Ofisi ya Mambo ya Nje-Zanzibar wakati wa hafla ya ufunguzi wa Tamasha la Utamaduni na Sanaa la Afrika 2022 (FESTAC 2022) mjini Zanzibar. 
 Kikundi cha ngoma kikitoa burdani wakati wa hafla ya ufunguzi wa Tamasha la Utamaduni na Sanaa la Afrika 2022 (FESTAC 2022) mjini Zanzibar
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma M. Rajab akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mbalimbali wa ndani na nje ya nchi wakati wa hafla ya ufunguzi wa Tamasha la Utamaduni na Sanaa la Afrika 2022 (FESTAC 2022) mjini Zanzibar

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.