Tuesday, May 10, 2022

BALOZI SOKOINE ATETA NA BALOZI MALAWI, COMORO

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine amekutana kwa mazungumzo Balozi wa Malawi nchini, Mhe. Andrew Kumwenda pamoja na Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini Dkt. Ahamada El Badaoui leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Awali akizungumza na Balozi wa Malawi nchini, Balozi Sokoine amemhakikishia ushirikiano wa Wizara na Serikali kwa ujumla wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yake hapa nchini.  

Kwa Upande wake Balozi wa Malawi nchini, Mhe. Kumwenda ameishukuru Serikali kwa ushirikano inaompatia tangu alipowasili nchini na ameahidi kuendeleza uhusiano mzuri kati ya Tanzania na Malawi kwa maslahi ya pande zote mbili.

Katika tukio jingine, Balozi Sokoine amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini, Dkt. Ahamada El Badaoui ambapo pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali ya kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Comoro.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akizungumza na Balozi wa Malawi nchini, Mhe. Andrew Kumwenda katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mazungumzo ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine na Balozi wa Malawi nchini, Mhe. Andrew Kumwenda yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akizungumza na Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini Dkt. Ahamada El Badaoui leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akiagana na Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini Dkt. Ahamada El Badaoui baada ya kumaliza mazungumzo yao  


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.