Tuesday, October 8, 2024
Monday, October 7, 2024
WAZIRI KOMBO: TANZANIA ITAENDELEA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA KULETA AMANI AFRIKA
Mkutano ukiedelea |
Sunday, October 6, 2024
MKUU WA MISHENI YA UANGALIZI WA UCHAGUZI YA SADC NCHINI MSUMBIJI AONGOZA KIKAO CHA WAKUU WA MISHENI ZA UANGALIZI ZA KIMATAIFA ZILIZOPO MSUMBIJI
Mkutano huo ulihudhuriwa na
Wakuu wa Misheni za Uangalizi kutoka Umoja wa Afrika (AU-EOM), Umoja wa Ulaya
(EU-EOM), Jumuiya ya Madola na Jukwaa la Uchaguzi la Nchi za Jumuiya ya
Maendeleo Kusini mwa Afrika (ECF-SADC).
Misheni ya uangalizi ya
Umoja wa Afrika inaongozwa na Makamu wa Rais Mstaafu wa Angola, Mhe. Bornito de
Sousa Baltazar Diogo huku Misheni ya Jumuiya ya Madola ikiongozwa na Waziri
Mkuu Mstaafu wa Saint Lucia, Mhe. Kenny Anthony.
Aidha, Misheni ya Umoja wa
Ulaya inaongozwa na Mbunge katika Bunge la Ulaya, Mhe. Laura Ballarin Cereza na
Misheni ya ECF-SADC inaongozwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya
Angola, Jaji Dkt. Manuel Pereira da Silva.
Mhe. Dkt. Karume akisalimiana na Mhe. Kenny Anthony, Waziri Mkuu Mstaafu wa Saint Lucia ambaye pia ni Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi nchini Msumbiji kutoka Jumuiya ya Madola |
Mhe. Dkt. Karume akizungumza na Mwakilishi wa Mkuu wa Misheni ya Uangalizi ya Umoja wa Ulaya. Kushoto ni Mjumbe wa Troika kutoka Tanzania ambaye pia ni Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaibu Mussa |
Balozi Mussa akisalimiana na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi wa Msumbiji kutoka Umoja wa Afrika (AU-EOM) na Makamu wa Rais Mstaafu wa Angola, Mhe. Bornito de Sousa Baltazar Diogo |
Picha ya pamoja ya Waku wa Misheni za Uangalizi za Kimataifa |
Picha ya pamoja ya Wakuu wa Misheni za Kimataifa za Uangalizi wa Uchaguzi nchini Msumbiji wakiwa na Wajumbe wa Troika kutoka Tanzania ambao ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ay Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mussa (kushoto) na Mshauri wa Rais masuala ya Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Sofia Mjema (kulia) |
Picha ya pamoja |
MKUU WA MISHENI YA UANGALIZI WA UCHAGUZI YA SADC NCHINI MSUMBIJI AFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA VYAMA VYA UPINZANI VYA NCHINI MSUMBIJI
Rais Mstaafu wa Zanzibar na
Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika (SADC –SEOM) nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume tarehe 06
Oktoba, 2024 jijini Maputo amefanya mazungumzo na viongozi na wawakilishi kadhaa wa vyama vya
upinzani vya Msumbiji ikiwa ni mwendelezo wa jukumu lake la kukutana na wadau
mbalimbali wa uchaguzi mkuu wa Msumbiji unaotarajiwa kufanyika tarehe 09 Oktoba
2024.
Katika mazungumzo yake na
viongozi hao kutoka vyama vya MPD, PEMO, UDM, RD, PDM, Ecologists na PPD, Mhe. Dkt. Karume
pamoja na mambo mengine aliwaeleza lengo la Misheni anayoiongoza kuwa ni
kuangalia uchaguzi kwa mujibu wa kanuni na miongozo ya uchaguzi ya SADC
iliyorekebishwa mwaka 2021 inayozingatia misingi ya haki, usawa na demokrasia.
Pia alitumia fursa hiyo kuwatakia wananchi wa Msumbiji uchaguzi wa amani na utulivu.
Ujumbe wa Mhe. Dkt. Karume
kwenye mkutano huo uliwajumuisha Wajumbe
wa Troika kutoka Tanzania, Zambia na Malawi, Sekretarieti ya SADC akiwemo Mkurugenzi
wa Organ , Prof.
Kula Ishmael Theletsane na
Wajumbe wa Baraza la Ushauri wa masuala
ya Uchaguzi la SADC (SEAC). Wajumbe wa
Troika kutoka Tanzania walioshiriki ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushiriano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaibu Mussa na Mshauri wa Rais masuala ya Wanawake na
Makundi Maalum, Mhe. Sofia Mjema.
Mhe. Dkt. Karume kwa nafasi yake ya Mkuu wa Uangalizi wa Uchaguzi ya SADC ameendelea kukutana na viongozi wa Serikali na wadau mbalimbali wa uchaguzi ambapo hadi sasa amekutana na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Msumbiji (CNE), Mabalozi wa Nchi za SADC waliopo Msumbiji, Waziri wa Mambo ya Nje wa Msumbiji, Kamishna Msidizi wa Jeshi la Polisi la Msumbiji na Mgombea urais wa Chama Tawala cha FRELIMO, Mhe. Daniel Francisco Chapo na Viongozi wa dini.
|
Mjumbe wa Troika kutoka Tanzania ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaibu Mussa akijitambulisha wakati wa kikao kati ya Mkuu wa Misheni ya Uangalizi ya SADC, Mhe. Dkt. Karume na viongozi wa vyama vya upinzani vya nchini Msumbiji |
Mjumbe wa Troika kutoka Tanzania ambaye pia ni Mshauri wa Rais masuala ya Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Sofia Mjema akijitambulisha wakati wa kikao kati ya Mkuu wa Misheni ya Uangalizi ya SADC, Mhe. Dkt. Karume na viongozi wa vyama vya upinzani vya nchini Msumbiji |
Sehemu ya viongozi hao wa vyama vya upinzani vya Msumbiji wakizungumza wakati wa kikao kati yao na Mkuu wa Misheni ya SADC ya Uangalizi wa Uchaguzi nchini humo, Mhe. Dkt. Karume |
Kiongozi wa Chama cha Ecologists akizungumza |
Kikao kikiendelea |
Kikao kikiendelea |
Kikao kikiendelea |
Mjumbe kutoka Baraza la SADC la Ushauri kuhusu masuala ya Uchaguzi akizungumza |
Mjumbe wa Troika kutoka Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Talha Waziri akizungumza |
Mhe. Dkt. Karume akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya viongozi wa vyama vya upinzani aliokutana nao |
Picha ya pamoja |
Picha ya pamoja |
Picha ya pamoja |
Picha ya pamoja |
MKUU WA MISHENI YA UANGALIZI WA UCHAGUZI YA SADC NCHINI MSUMBIJI AENDELEA KUKUTANA NA WADAU WA UCHAGUZI NCHINI MSUMBIJI
Rais Mstaafu wa Zanzibar na
Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika (SADC –SEOM) nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume ameendelea
kukutana na wadau mbalimbali wa uchaguzi mkuu wa Msumbiji unaotarajiwa
kufanyika tarehe 09 Oktoba 2024.
Mhe. Dkt. Karume kwa nyakati tofauti leo tarehe 05 Oktoba 2024
jijini Maputo, amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili
la Kilutheri la Msumbiji, Mchungaji Augusto Pedro na Mkurugenzi wa Kituo cha
Demokrasia na Haki za Binadamu (CDD), Prof. Adriano Nuvunga.
Katika mazungumzo yake na
viongozi hao, Mhe. Dkt. Karume pamoja na mambo mengine aliwaeleza lengo la
Misheni hiyo ya SADC kuwa ni kuangalia uchaguzi kwa mujibu wa kanuni na
miongozo ya uchaguzi ya SADC iliyorekebishwa mwaka 2021 inayozingatia misingi
ya haki, usawa na demokrasia.
Ujumbe wa Mhe. Dkt. Karume
kwenye mikutano hiyo uliwajumuisha
Wajumbe wa Troika kutoka Tanzania, Zambia na Malawi, Sekretarieti ya SADC
akiwemo Mkurugenzi wa Organ , Prof. Kula Ishmael Theletsane na
Wajumbe wa Baraza la Ushauri wa masuala
ya Uchaguzi la SADC (SEAC). Wajumbe wa
Troika kutoka Tanzania walioshiriki ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushiriano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaibu Mussa na Mshauri wa Rais masuala ya Wanawake na
Makundi Maalum, Mhe. Sofia Mjema.
Vilevile, Mhe. Dkt. Karume
amepokea taarifa kutoka kwenye Kamati ya Uandishi ya Misheni hiyo kuhusu utekelezaji
wa masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupokea taarifa kutoka kwa waangalizi wa
SADC ambao walisambazwa kwenye majimbo 11 ya uchaguzi nchini humo tangu tarehe
03 Oktoba 2024.
Mhe. Dkt. Karume kwa nafasi yake ya Mkuu wa Uangalizi wa Uchaguzi ya SADC ameendelea kukutana na viongozi wa Serikali na wadau mbalimbali wa uchaguzi ambapo hadi sasa amekutana na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Msumbiji (CNE), Mabalozi wa Nchi za SADC waliopo Msumbiji, Waziri wa Mambo ya Nje wa Msumbiji, Kamishna Msidizi wa Jeshi la Polisi la Msumbiji na Mgombea urais wa Chama Tawala cha FRELIMO, Mhe. Daniel Francisco Chapo.
Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC –SEOM) nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume akizungumza na Katibu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Msumbiji, Mchungaji Augusto Pedro (hayupo pichani) ikiwa ni mwendelezo wa Mkuu huyo wa Misheni ya SADC wa kukutana na wadau mbalimbali wa uchaguzi mkuu wa Msumbiji unaotarajiwa kufanyika tarehe 09 Oktoba 2024. Mazungumzo yao yalifanyika jijini Maputo tarehe 5 Oktoba 2024 |
Katibu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Msumbiji, Mchungaji Augusto Pedro akizungumza na Mkuu wa Misheni ya SADC ya uangalizi wa Uchaguzi nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Karume (hayupo pichani) |
Mhe. Dkt. Karume akizungumza na Mkurugenzi wa Kituo cha Demokrasia na Haki za Binadamu (CDD), Prof. Adriano Nuvunga katika mkutano uliofanyika jijini Maputo tarehe 5 Oktoba 2024 |
Mjumbe wa Troika na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Sahibu Mussa akichangia jambo wakati wa mkutano kati ya Mhe. Dkt. Karume na Prof. Nuvunga hawapo pichani. |
Mjumbe wa Troika na Mshauri wa Rais masuala ya Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Sofia Mjema akichangia hoja wakati wa Mkutano kati ya Mhe. Dkt. Karume na Mkurugenzi wa CDD, Prof. Nuvunga hawapo pichani |
Mjumbe wa Troika ambaye pia ni Balozi wa Malawi nchini Msumbiji, Mhe. Wezi Moyo akichangia jambo. Kushoto ni Mjumbe wa Troika kutoka Zambia, Bw. Lubasi |
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Talha Waziri naye akichangia jambo |
Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi wa Taarifa ya Misheni ya SADC, Bi. Shazma Msuya akitoa taarifa kwa Mkuu wa Misheni ya SADC ya Uangalizi wa Uchaguzi nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Karume (hayupo pichani) |
Bi. Msuya akiwasilisha taarifa kwa Mkuu wa Misheni, Mhe. Dkt. Karume |
Uwasiishaji taarifa ya Misheni ukiendelea |
Mhe. Dkt. Karume akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Msumbiji baada ya kukamilisha mazungumzo yao |
Mhe. Dkt. Karume akiagana na Katibu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Msumbiji mara baada ya mazungumzo yao |
Mhe. Dkt. Karume akiagana na Mkurugenzi wa Kituo cha Demokrasia na Haki za Binadamu (CDD), Prof. Adriano Nuvunga baada ya mazungumzo yao |
Picha ya pamoja |
Saturday, October 5, 2024
WAZIRI KOMBO AWATAKA WATAFITI WA AFRIKA KUZINGATIA UZALENDO
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) akichangia mada kwenye Mdahalo wa kwanza wa Amani na Usalama Afrika (APSD) ulioandaliwa na Taasisi ya Thabo Mbeki unaondelea jijini Johannesburg, nchini Afrika Kusini. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo akifuatilia jambo kwenye Mdahalo wa kwanza wa Amani na Usalama Afrika ulioandaliwa na Taasisi ya Thabo Mbeki unaondelea jijini Johannesburg, Afrika Kusini. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo akifafanua jambo kwenye Mdahalo wa kwanza wa Amani na Usalama Afrika ulioandaliwa na Taasisi ya Thabo Mbeki unaondelea jijini Johannesburg, Afrika Kusini. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Zimbambwe Mhe. Federick Shava na Prof. Antoni van Nieuwkerk (katikati) akiongoza mdahalo huo |
Mdahalo ukiendelea |
Mdahalo ukiendelea |
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Bertha Makilagi akifuatilia Mdahalo wa kwanza wa Amani na Usalama Afrika ulioandaliwa na Taasisi ya Thabo Mbeki unaondelea jijini Johannesburg, Afrika Kusini. |
Afisa Mambo ya Nje Mwandamizi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Emmanuel Shayo akifuatilia Mdahalo wa kwanza wa Amani na Usalama Afrika ulioandaliwa na Taasisi ya Thabo Mbeki unaondelea jijini Johannesburg, Afrika Kusini. |
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Mhe. Thabo Mbeki akifuatilia Mdahalo wa kwanza wa Amani na Usalama Afrika ulioandaliwa na Taasisi ya Thabo Mbeki unaondelea jijini Johannesburg, Afrika Kusini. |
Rais wa zamani wa Zibwabwe Mhe. Johaquim Chissano akihutubia kwenye ufunguzi wa Mdahalo wa kwanza wa Amani na Usalama Afrika uliofanyika jijini Johannesburg, Afrika Kusini kwa njia ya mtandao. |