Sunday, October 27, 2024

MHE. PINDA AKUTANA NA JUMUIYA YA WANADIPLOMASIA WANAOWAKILISHA NCHI ZAO BOTSWANA


Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda, na ujumbe wake katika  kikao na Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini Botswana kilichofanyika jijini Gaborone tarehe 26 Oktoba 2024


Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda, na ujumbe wake (kulia) katika  kikao na Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini Botswana kilichofanyika jijini Gaborone tarehe 26 Oktoba 2024


Balozi wa Tanzania nchini Botswana Mhe. James Bwana (Kushoto) akiwa na Mabalozi wenzake wanaoziwakilisha nchi zao nchini Botswana wakifutiliamkutano wao na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda uliofanyika jijini Gaborone tarehe 26 Oktoba 2024


Kiongozi wa Mabalozi na Balozi wa Angola nchini Botswana Mhe. Beatriz Morais (kushoto) akiwa na mabalozi wenzake wanaoziwakilisha nchi zao nchini Botswana wakifutilia mkutano wao na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda uliofanyika jijini Gaborone tarehe 26 Oktoba 2024


Balozi wa Tanzania nchini Botswana Mhe. James Bwana (Kushoto) akiwa na Mabalozi wenzake wanaoziwakilisha nchi zao nchini Botswana wakifutiliamkutano wao na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda uliofanyika jijini Gaborone tarehe 26 Oktoba 2024


Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda, katika picha ya Pamoja na Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini Botswana baada ya mkutano kati ya SEOM na Jumuiya ya wanadisplomasia wanaoziwakilisha nchi zao nchini Botswana uliofanyika jijini Gaborone tarehe 26 Oktoba 2024 uliolenga kusikiliza maoni na mtazamo wa Mabalozi kuhusiana na mwenendo wa uchaguzi mkuu wa Botswana unaotarajiwa kufanyika tarehe 30 Oktoba 2024.


Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda, akizungumza na Balozi wa Marekani nchini Botswana, Mhe. Howard Van Vranken, baada ya mkutano kati ya SEOM na Jumuiya ya wanadisplomasia wanaoziwakilisha nchi zao nchini Botswana uliofanyika jijini Gaborone tarehe 26 Oktoba 2024 ambao ulilenga kusikiliza maoni na mtazamo wa Mabalozi kuhusiana na mwenendo wa uchaguzi mkuu wa Botswana unaotarajiwa kufanyika tarehe 30 Oktoba 2024.

 

Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda, amekutana na kuzungumza na Jumuiya ya Wanadiplomasia wanaoziwakilisha nchi zao nchini Botswana katika kikao kilichofanyika jijini Gaborone tarehe 26 Oktoba 2024.

Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Pinda amewaarifu wanadiplomasia hao juu ya majukumu ya SEOM  katika kutekeleza jukumu la Uangalizi kama lilivyokasimiwa na SADC na kusisitiza kuwa SEOM inaifanya kazi hiyo kwa kuhakikisha nchi husika inazingatia na kufuata misingi na miongozo ya uchaguzi wa kidemokrasia ya SADC.

Ameeleza kuwa SEOM imekutana na wadau mbalimbali ikiwa ni sehemu ya ratiba za misheni hiyo kusikiliza na kuzungumza moja kwa moja na wadau wa uchaguzi huo kupata picha halisi ya jinsi mwenendo na maandalizi ya uchaguzi huo unavyokwenda.

Amesema SEOM imekuwa ikiangalia jinsi mwenendo, mipango na utaratibu wa uchaguzi huo unavyoendeshwakwa, kuangalia kama elimu kwa wapiga kura imetolewa vya kutosha, kama inaendelea kutolewa kwa wadau wote wa uchaguzi huo na kama kumekuwa na ushirikishwaji kwa wadau wote wa uchaguzi nchini humo na hivyo kuwa na uelewa wa pamoja kuhusiana na uchaguzi mkuu wa Botswana uliopangwa kufanyika tarehe 30 Oktoba,2024.

Amesema SEOM imepeleka waangalizi wake katika majimbo yote ya uchaguzi ili kuangalia hali inavyokwenda , itakavyokuwa siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi na watakuwa na mikutano na watu mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kusikiliza na kupata maoni ili kuhakikisha kazi yao ya uangalizi inakwenda vizuri

Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa Mabalozi hao na Balozi wa Jamhuri ya Angola Mheshimiwa Beatriz Morais ameishukuru SEOM kwa kufikiria kukutana na mabalozi kama moja ya wadau wa uchaguzi wa Botswana ili kusikiliza mtazamo wao kuhusiana na mwenendo wa uchaguzi na kuwapongeza wananchi wa Botswana kwa hali ya utulivu waliyonayo na hivyo kuwa na amani na usalama katika maeneo yote.

Naye Balozi wa Ufaransa nchini Botswana amepongeza hali ya amani na utulivu iliyoko nchini Botswana wakati huu wakielekea katika uchaguzi mkuu na kuongeza kuwa ni jambo la msingi na la mfano kwa nchi za Afrika na nyinginezo.

Balozi wa Tanzania nchini Botswana mwenye makazi yake nchini Afrika Kusini Mhe. James Bwana amepongeza Serikali ya Botswana kwa kuruhusu na kuwakaribisha waangalizi wa uchaguzi nchini humo na kuwa tayari kushirikiana nao na kuwapongeza wananchi wa Botswana kwa utulivu waliounesha katika kipindi hiki na kuwatakia kila la heri katika uchaguzi mkuu ujao.

SEOM pia imekutana na viongozi wa vyama vya siasa vya  BPF, BMD na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) Botswana. Vyama vya siasa katika mikutano yao wameelezea kutokuridhishwa kwao na mwenendo wa uchaguzi huo huku wakisema kumekuwa na uhaba wa karatasi za kupigia kura hali ambayo inawatia mashaka juu ya uchaguzi huo kufanyika kwa uhuru na kwa haki na kuongeza kuwa kitendo cha kuchelewa kutangazwa mapema kwa tarehe ya uchaguzi kumevifanya vyama vya upinzani nchini humo kutokuwa na maandalizi mazuri ya uchaguzi huo.

Chama cha BPF kimesema wanaamini kuwa matokeo ya kurudiwa kwa kura za awali zilizohussisha Diaspora, vyombo vya ulinzi na usalama na majimbo matatu zitaongeza matumaini kwa wananchi na hivyo kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi huo.

Nayo MISA Botswana amesema taasisi yao imekuwa ikijishughulisha na utoaji wa elimu kwa waandishi wa Habari juu ya kuandaa na kuripoti taarifa za uchaguzi ila wanaelewa kuwa wnachama wao wanakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka kwa taarifa zinazotolewa na wananchi kupitia mitandao ya kijamii ambazo hazizingatii misingi na maadili ya uandishi wa habari.

 






Friday, October 25, 2024

MHE. PINDA AKUTANA NA RAIS WA BOTSWANA

Mkuu wa Misheni ya Uangalizi ya Uchaguzi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC - SEOM) kwenye Uchaguzi Mkuu wa Botswana na Waziri Mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Botswana Mheshimiwa Mokgweetsi Eric Keabetswe Masisi alipofika Ofisini kwa Mheshimiwa Masisi kujitambaulisha na ujumbe wake tarehe 24 Oktoba, 2024. Mhe. Pinda na ujumbe wake wako nchini Botswana  kuangalia uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliopangwa kufanyika tarehe 30 Oktoba 2024

 
Mkuu wa Misheni ya Uangalizi ya Uchaguzi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC - SEOM) kwenye Uchaguzi Mkuu wa Botswana na Waziri Mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda akisaini kitabu cha wageni alipowasili  Ofisini kwa Mheshimiwa Masisi kujitambaulisha na ujumbe wake tarehe 24 Oktoba, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Botswana, Mheshimiwa Mokgweetsi Eric Keabetswe Masisi (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi ya Uchaguzi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC - SEOM) kwenye Uchaguzi Mkuu wa Botswana na Waziri Mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda alipokutana na ujumbe wa SEOM katika Ikulu ya Gaborone tarehe 24 Oktoba 2024. Kulia ni Katibu Mtendaji wa SADC, Mheshimiwa Elias Magosi.

Rais wa Jamhuri ya Botswana, Mheshimiwa Mokgweetsi Eric Keabetswe Masisi (kushoto) na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi ya Uchaguzi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC - SEOM) kwenye Uchaguzi Mkuu wa Botswana na Waziri Mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda walipokutana  Ikulu ya Gaborone tarehe 24 Oktoba 2024.

Kikao kikiendelea

Kikao kikiendelea

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Botswana, Mhe. Dkt. Lemongang Kwape (kulia), na watendaji wake waliposhiriki kikao kati ya Rais wa Jamhuri ya Botswana, Mheshimiwa Mokgweetsi Eric Keabetswe Masisi (kushoto) na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi ya Uchaguzi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC - SEOM) kwenye Uchaguzi Mkuu wa Botswana na Waziri Mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda alipowatembelea Ikulu jijini Gaborone.

Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM), Mheshimiwa Mizengo Pinda, na baadhi ya wajumbe wake walipofika Ofisini kwa kwa Rais wa Jamhuri ya Botswana, Mheshimiwa Mokgweetsi Eric Keabetswe Masisi,  jijini Gaborone.






Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM), Mheshimiwa Mizengo Pinda, akiangalia picha za waliowahi kuwa Marais wa Jamhuri ya Botswa alipofika ofisini kwa  Rais wa Jamhuri ya Botswana, Mheshimiwa Mokgweetsi Eric Keabetswe Masisi,  jijini Gaborone.


 

Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM), Mheshimiwa Mizengo Pinda, amekutana na Rais wa Jamhuri ya Botswana, Mheshimiwa Mokgweetsi Eric Keabetswe Masisi, katika ofisi yake jijini Gaborone. SEOM ilitumia ziara hiyo kujitambulisha kwa Mhe. Rais Masisi na kubadilishana mawazo kuhusu hali ya kidemokrasia na maendeleo nchini Botswana.

Akizungumza na Mheshimiwa Masisi, Mheshimiwa Pinda alisisitiza wajibu wa SEOM kulingana na Misingi na Mwongozo wa SADC kuhusu Uchaguzi wa Kidemokrasia na kuonesha utayari kwa SEOM kutekeleza jukumu la uangalizi katika uchaguzi mkuu ujao wa Botswana.

Mhe. Pinda alieleza shukrani zake kwa mapokezi mazuri aliyoyapata yeye na timu yake tangu walipowasili Botswana na kumueleza Mhe. Rais Masisi kuwa kabla ya kukutana na yeye, SEOM ilikutana na kuzungumza na wadau mbalimbali, ambao ni pamoja na Tume Huru ya Uchaguzi ya Botswana (IEC), Kamishna wa Polisi wa Botswana, Wizara ya Mambo ya Nje, viongozi wa vyama vya kisiasa, NGO, na Mabalozi wanaowakilisha Botswana na SADC.

Aliongeza kuwa timu hiyo pia ilipitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ili kupata ufahamu kuhusu masuala yanayohusiana na uchaguzi mkuu ujao wa nchi hiyo.

Kwa upande wake, Mhe. Rais Masisi aliwakaribisha waangalizi wa SEOM na kuwahakikishia kuwa Batswana iko tayari kwa uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 30 Oktoba 2024 na kuongeza kuwa Serikali ya Botswana iko tayari kushirikiana na wadau wote, ikiwa ni pamoja na waangalizi na aliwaambia SEOM kuzungumza na yeyote wanayefikiri atawasaidia kutekeleza jukumu lao la uangalizi.

“Serikali iko tayari kufanya kazi na waangalizi; nendeni mkazungumze na yeyote mnayefikiri anaweza kuwasaidia nyinyi na timu yenu kufanya kazi zenu vizuri. Botswana ni nyumbani kwa SADC; nyote mnakaribishwa hapa na fanyeni kazi yenu  kwa uhuru," alisisitiza Mheshimiwa Masisi.

Alisema anaamini kuwa Tume Huru ya Uchaguzi ya Botswana (IEC) imeshirikisha wadau wote wanaohusika na uchaguzi huo mkuu, na kwamba Serikali yake ina imani kuwa kila kitu kitakuwa sawa na uchaguzi utakuwa huru, haki, na wa kuaminika, na kwamba usalama na amani vitakuwepo wakati wa uchaguzi na hata baada ya uchaguzi huo.

Aliwahakikishia wajumbe wa SEOM kuwa Serikali imetumia rasilimali zote zilizopo kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa mafanikio makubwa na alisisitiza kuwa Serikali iko tayari kutoa msaada wowote kwa SEOM pale itakapohitajika.

Septemba 2024, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa Ulinzi na Usalama ya  SADC TROIKA, alimteua Mheshimiwa Pinda kuongoza Misheni ya  Uangalizi wa SADC katika uchaguzi mkuu wa Botswana.

SEOM ilijumuisha maafisa kutoka Sekretarieti ya SADC, wanachama wa Taasisi ya SADC Troika kutoka Jamhuri ya Malawi, Zambia, na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na Baraza la Ushauri la Uchaguzi la SADC (SEAC).

 


 

Thursday, October 24, 2024

Waandishi Waendesha Ofisi 16 mafunzoni Mjini Morogoro


Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imefanikiwa kupeleka waandishi waendesha Ofisi 16 kwenye mafunzo ya matumizi fasaha ya Kiswahili Sanifu, yanayoendeshwa na Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA). Mafunzo hayo yanayofanyika katika Hoteli ya Morena Mjini Morogoro yalianza tarehe 21 Oktoba 2024 na yatahitimishwa tarehe 26 Oktoba 2024 

Akifungua mafunzo hayo Mratibu wa Mafunzo kutoka BAKITA Bi. Razati Mmary alieleza kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwawezesha Waandishi Waendesha Ofisi kuwa na matumizi ya Kiswahili Fasaha na Sanifu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

 

Aidha, alisisitiza Waandishi waendesha Ofisi wanao wajibu wa kurekebisha makosa yaliyozoeleka katika uandishi wa nyaraka za Serikali.



MHE. PINDA AKUTANA NA VIONGOZI WA TUME HURU YA UCHAGUZI YA BOTSWANA

 

Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC -SEOM) nchini Botswana, Mhe. Mizengo Pinda (wa pili kulia) akisalimiana na Mwenyekiti na Uongozi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Botswana (IEC) Mhe. Jaji Barnabas Nyamadzabo na Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Bw. Jefferson Siamisangwalipokutana jijini Gaborone, Botswana.


Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC -SEOM) nchini Botswana, Mhe. Mizengo Pinda na timu yake akizungumza na Mwenyekiti na Uongozi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Botswana (IEC) Mhe. Jaji Barnabas Nyamadzabo na Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Bw. Jefferson Siamisang (hawapo pichani) walipokutana jijini Gaborone, Botswana.


Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC -SEOM) nchini Botswana, Mhe. Mizengo Pinda na timu yake akizungumza na Mwenyekiti na Uongozi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Botswana (IEC) Mhe. Jaji Barnabas Nyamadzabo na Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Bw. Jefferson Siamisang (hawapo pichani) walipokutana jijini Gaborone, Botswana.


Mwenyekiti  wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Botswana (IEC) Mhe. Jaji Barnabas Nyamadzabo akiwasilisha mamlaka ya Tume hiyo kwa Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC -SEOM) nchini Botswana, Mhe. Mizengo Pinda na timu yake walipokutana jijini Gaborone, Botswana.


Katibu Mtendaji wa IEC Bw. Jefferson Siamisang akiwasilisha taarifa ya maandalizi ya uchguzi mkuu wa Botswana kwa Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC -SEOM) nchini Botswana, Mhe. Mizengo Pinda na timu yake walipokutana jijini Gaborone, Botswana.


Katibu Mtendaji wa IEC Bw. Jefferson Siamisang akiangalia taarifa yake pamoja na Mwenyekiti wake Mhe. Jaji Barnabas Nyamadzabo  walipokutana na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC -SEOM) nchini Botswana, Mhe. Mizengo Pinda na timu yake jijini Gaborone, Botswana.


Viongozi wa IEC mkutanoni

Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC -SEOM) nchini Botswana, Mhe. Mizengo Pinda na timu yake

Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC -SEOM) nchini Botswana, Mhe. Mizengo Pinda na timu yake


Baadhi ya wajumbe wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC -SEOM) nchini Botswana  

 

 

Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC -SEOM) nchini Botswana, Mhe. Mizengo Pinda amekutana na kuzungumza na Mwenyekiti na Uongozi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Botswana (IEC) katika mazungumzo yaliyofanyika jijini Gaborone, Botswana.

Mhe. Pinda amekutana na kuzungumza na Mwenyekiti na Uongozi wa IEC  Mhe. Jaji Barnabas Nyamadzabo na Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Bw. Jefferson Siamisang ikiwa ni miongoni mwa viongozi  na Taasisi mbalimbali ambazo SEOM inakutana nazo ili kusikiliza na kufahamu mawazo na mitazamo yao kuhusiana na masuala mbalimbali ya uchaguzi Mkuu wa Botswana uliopangwa kufanyika tarehe 30 Oktoba, 2024.

Akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa IEC Mhe. Jaji Nyamadzabo alielezea Majukumu ya Tume hiyo kama yalivyoainishwa katika Kifungu cha 65A cha Katiba ya Botswana kuwa ni Kusimamia na kuendesha uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Taifa na Mamlaka za Serikali za Mitaa; ⁠Kuendesha kura ya maoni; ⁠Kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa ufanisi, kwa usahihi, kwa uhuru na kwa haki; ⁠Kutoa maagizo na maelekezo kwa Katibu wa Tume kuhusiana na majukumu yao chini ya Katiba na Sheria za Uchaguzi kwa ujumla na ⁠Kutekeleza majukumu mengine yoyote kama itakavyowekwa na Sheria ya Bunge la nchi hiyo.

Alisema kuwa IEC pia inajukumu la kuandikisha wapiga kura na kudhibiti gharama za kampeni na kuongeza kuwa Tume hiyo haina mamlaka ya kuamua migogoro ya uchaguzi ambayo inapelekwa Mahakama Kuu.

Naye Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Bw. Siamisang alieleza kuwa IEC imejipanga kikamilifu kuendesha zoezi la Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo na iko tayari kuifanya kazi hiyo kwa tija na ufanisi.

Amesema IEC tayari imeendesha zoezi la upigaji kuwa kwa diaspora wa Botswana, watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama na watumishi wa IEC lililofanyika tarehe 18 Oktoba 2024 na kuongeza kuwa IEC imeandikisha wapiga kura sawa na asilimia 80 ya lengo walilojiwekea katika zoezi lililofanyika kwa awamu tatu ikiwa ni ongezoko la asilimia Saba kutoka kwa wapiga kura wa mwaka 2019 walipofanya uchaguzi mkuu.

“IEC imeshaendesha zoezi la kupiga kura kwa hatua ya kwanza, zowezi hilolimehusisha diaspora wetu tuliowaandikisha, vyombo vya ulinzi na usalama n ahata awatumishi wa Tume, nikuhakikishie kuwa tumejipanga na tuko tayari kusimamia na kuendesha zoezi la uchaguzi kwa ufanisi, kila kitu kiko tayari na wahudumu wetu pia wako tayari kwa ujumla maandalizi yamekamilika tunasubiri tu siku ya kupiga kura,” alisema

Akizungumza baada ya kupokea taarifa ya Tume hiyo ya IEC, Mkuu wa misheni ya Uangalizi ya SADC -SEOM Mhe. Mizengo Pinda ameishukuru IEC kwa kukutana nao na kuwalezea jinsi walivyojipanga kuendesha zoezi zima la uchaguzi.

Mhe. Pinda alieleza kuwa SEOM wanajukumu la kuangalia namna uchaguzi huo unavyoeendeshwa ikiwa ni sehemu ya kukuza na kuendeleza demokrasia katika ukanda a wa SADC.

Amesema SEOM imepeleka waangalizi katika wilaya na majiji yote ya Botswana ili kuangalia zoezi zima kabla ya uchaguzi, siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi jinsi itakavyokuwa na inatarajia kutoa taarifa ya awali kuhusu hali ilivyokuwa tarehe 1 Novemba 2024.

MHE. PINDA AZUNGUMZA NA VIONGOZI WA SIASA NA VYA KIRAIA BOTSWANA


Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda na ujumbe wake (kulia) wamekutana na Mkurugenzi Mtendaji  wa Taasisi ya African Trust ya jijini Gaborone Bw. Monametsi Sokwe na kusikiliza maoni na mtazamo wake juu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu yanavyokwenda nchini humo.



     













 
    




 
 

 

 

 

 

Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda na ujumbe wake wamekutana na Mkurugenzi Mtendaji  wa Taasisi ya African Trust ya jijini Gaborone Bw. Monametsi Sokwe na kusikiliza maoni na mtazamo wake juu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu yanavyokwenda nchini humo.

Bw. Sokwe ameshukuru kukutana na SEOM na kusema kuwa vyama vingi ni vichanga na havina nguvu za kifedha kuendesha shughuli zao za kisiasa hasa za kampeni wakati huu wa uchaguzi.

Mhe. Pinda amemuomba Bw. Sokwe na washirika wake kuhakikisha wanaongeza na kuwashirikisha kwa wingi wanawake na vijana katika shughuli za siasa kwani kufanya hivyo ndivyo kunachochea ukuaji wa demokrasia nchini humo.

Katika tukio jingine Mhe. Pinda na ujumbe wake mazungumzo kwa njia ya mtandao na Kiongozi  wa Chama Kipya cha Siasa cha Botswana Republican Party (BRP) Bw. Biggie Butale ambacho kimesimamisha wagombea 10 katika nafasi ya viti vya Bunge la nchi hiyo.

Mhe. Pinda alieleza dhamira ya ujumbe wake kuzungumza na kiongozi huyo kuwa ni kutaka kusikia maoni na mawazo yake kuhusu namna kampeni za vyama vya siasa zinavyoendeshwa na kama mazingira ni mazuri na yanaridhisha kwa nyakati husika.

Bw. Biggie alielezea kuridhishwa kwake na namna shughuli za kuelekea uchaguzi mkuu zinavyoendeshwa na kwamba mazingira yamekuwa salama ila alielezea kutokuridhishwa kwake na wazo la kutoa fedha za uchaguzi kwa vyama vya siasa baada ya uchaguzi na kuongeza kuwa hatua hiyo haitoi nafasi kwa vyama vya siasa kuwa sawa na hivyo kuwapa manufaa vyama vikongwe na vikubwa na kuviacha vyama vichanga njiani.

Tarehe 30 Oktoba, 2024 Wananchi wa Botswana watapiga kura katika Uchaguzi mkuu kuchagua Wabunge wa Bunge la 13 la nchi hiyo na wajumbe wa Mabaraza ya Mitaa ambpo Viti 61 vya Bunge la Taifa na viti 609 vya mabaraza ya mitaa vitashindaniwa.

SEOM imepeleka waangalizi wake wa uchaguzi katika wilaya, miji na majiji yote nchini Botswana.


Wednesday, October 23, 2024

BALOZI SHELUKINDO AFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE WA BUNGE LA MAREKANI

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samwel Shelukindo na Bi. Heather Flynn, Mtaalamu wa Masuala ya Uhusiano wa Kimataifa wa Kamati ya Uhusiano wa Kimataifa ya Bunge (Senate) la Marekani na ujumbe wao wakiwa katika mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es salaa.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samwel Shelukindo, leo tarehe 23 Oktoba 2024, amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Bunge la Marekani wa Kamati ya Uhusiano wa Kimataifa yaliyofanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam. 

Kupitia mazungumzo hayo wamejadili masuala muhimu katika kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo biashara na uwekezaji, utalii, demokrasia na utawala bora na ulinzi na usalama. 

Balozi Shelukindo akizungumza na ujumbe huo ulioongozwa na Bi. Heather Flynn, Mtaalamu wa Masuala ya Uhusiano wa Kimataifa wa Kamati ya Uhusiano wa Kimataifa ya Bunge (Senate) la Marekani amewaeleza kuwa hali ya kisiasa nchini ni salama na tulivu. Katibu Mkuu Balozi Shelukindo alisisitiza kuwa hali hiyo inachagizwa na juhudi zinazofanywa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Falsafa ya R4, ambazo ni Maridhiano, Mageuzi, Ustahimilivu na Kujenga upya.

Kwa upande wake Bi. Heather Flynn ameeleza kuridhishwa kwake na mageuzi mbalimbali ya kisiasa na kiuchumi yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita, ambayo ameeleza kuwa ni muhimu katika ustawi wa siasa, jamii na uchumi wa Taifa.

Ujumbe wa Kamati ya Uhusiano wa Kimataifa ya Bunge la Marekani ipo nchini kwa ziara ya kikazi, ambapo watakutana na kufanya mazungumzo na watendaji na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samwel Shelukindo na Bi. Heather Flynn, Mtaalamu wa Masuala ya Uhusiano wa Kimataifa wa Kamati ya Uhusiano wa Kimataifa ya Bunge (Senate) la Marekani na ujumbe wakifurahia jambo walipokuwa kwenye mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es salaa.

NAIBU WAZIRI CHUMI AFANYA MAZUNGUMZO NA WABUNGE WA BUNGE LA AFRIKA


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi (Mb.) amekutana kwa mazungumzo na Wabunge wa Bunge la Afrika (PAP) katika Ofisi ya Wizara jijini Dodoma tarehe 22 Oktoba, 2024.

Wabunge hao wa Bunge la Afrika wa Kamati ya Biashara, Forodha na Uhamiaji wapo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku nane (8) yenye lengo la kujionea hatua iliyopigwa na Tanzania katika utekelezaji wa muongozo wa awali wa kufanya Biashara (Guided Trade Initiatives - GTI) wa Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA).

Akizungumza na wabunge hao naibu Waziri Chumi ameeleza Tanzania imekuwa ikifanya shughuli nyingi za kibiashara ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki na bara la Afrika kwa ujumla kupitia AfCFTA ambapo Tanzania ilichaguliwa kuwa miongoni mwa nchi 8 za mfano katika utekelezaji wa awali wa kufanya biashara. Nchi nyingine ni Rwanda, Ghana, Egypt, Mauritius,Cameroon na Tunisia.

AfCFTA ni sehemu ya utekelezaji wa Agenda 2063 iliyosainiwa Rwanda mwaka 2018 na Wakuu wa Nchi na Serikali ya Afrika ikiwa na matarajio ya kuwa na mtangamano wa kikanda wenye amani na ustawi.
 Aidha, amefafanua kuwa uratibu wa wafanyabiashara unafanywa na taasisi za biashara mfano taasisi ya sekta binafsi Tanzania, Chama cha wafanya biashara wenye viwanda na wakulima, Chama cha wafanyabiashara wanawake Tanzania na nyingine ambazo zimekuwa zikiratibu na kuwaunganisha na Serikali katika kuwezesha shughuli za kibiashara na kujenga uelewa wa masuala mbalimbali kwa wafanyabishara.

“Elimu kwa umma bado inahitajika katika kujenga uelewa kwa wafanyabiashara ili waweze kutumia fursa za masoko na biashara zinazopatika barani Afrika, hivyo Tanzania inaendelea kujenga uwezo katika hilo ili kuongeza fursa za mazao ya kibishara na taratibu za kufanya biashara” alisema Mhe. Chumi.

Naye, Mkuu wa ujumbe huo wa Wabunge hao na Mbunge wa Kenya, Mhe. Prof. Margaret Kamar  ameeleza kuwa Bunge la Afrika hushirikiana katika utendaji wake na Mawaziri wa Mambo ya Nje barani Afrika katika kuhakikisha malengo na mipango mbalimbali yenye maslahi ya kikanda inafikiwa.

Pia ametumia nafasi hiyo kuipongeza Serikali ya Jamhuri ya Tanzania kwa kufanikiwa kufanya maboresho na mageuzi ya kibiashara hususan katika kuhakikisha inakua na barabara nzuri inayowezesha shughuli za kibiashara baina yake na nchi jirani na bara la Afrika kwa ujumla.

“ Miongoni mwa mikoa tuliyotembelea kabla ya kuja huku Dododma ni mkoa wa Arusha, tumejionea dhahiri namna barabara zilivyoboreshwa na kutuwezesha kutembelea kwa urahisi kila
sehemu tuliyohitaji kutembelea” Mhe. Kamar alisema.

Pia alibainisha kuwa huo ni ushahidi tosha kwa nchi nyingine za Afrika kuona kuwa inawezekana kuiunganisha Afrika kibiashara endapo hatua madhubuti za kufanikisha hilo litapewa mkazo.

Vilevile ameeleza kuwa hatua hizo zilizopigwa zinaonesha kuwa Tanzania ina uwezo wa kupiga hatua zaidi kibiashara na kuzipita kanda nyingine kwakuwa ina nafasi na fursa za kutosha hususan kupitia uwingi wa rasilimali za kibiashara.

Msisitizo mwingine uliotolewa na Wabunge hao wa PAP ni pamoja na suala la uhuru wa watu kutembea baina ya nchi na nchi ambalo kwa upande mwingine linahitaji muongozo kwakuwa kwasasa bado halijielezi vizuri mipaka ya uhuru huo.

Kwa upande wa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi ameeleza kuwa Tanzania katika jitihada zake za kuwaunganisha Watanzania kibiashara barani Afrika, imefanikiwa kufanya yafuatayo; uwepo wa nishati ya umeme ya uhakika, Ujenzi wa miundombinu hususan barabara, reli ya kisasa, kuimarisha shirika la ndege la Tanzania kwa kuongeza ndege ikiwemo ndege za mizigo zenye uwezo kusafiri popote duniani.

Pia Balozi Mbundi ameeleza kuwa GTI imewezesha usafirishaji wa bidhaa za biashara zilizoongezwa thamani ambapo kwa upande wa Tanzania ilianza kuuza bidhaa kama mkonge, kahawa, viungo na karanga.

Kadhalika, ujenzi wa Vituo vya Huduma za Pamoja Mipakani umewezesha kuondoa changamoto nyingi zilizokuwa kikwazo katika biashara na nchi nyingine. Vituo hivyo vimewezesha kuokoa muda kwa wasafirishaji wa bidhaa na wasafiri na kupunguza muda wa kupitisha bidhaa mipakani ambapo maboresho hayo yameenda sambamba na maboresho ya mizani ya kupima mizigo inayotoka bandarini na kuelekea katika nchi jirani.

Hata hivyo, Tanzania ipo katika hatua za mapitio za kutathimini bidhaa nyingine ambazo zitafaa kuingia katika utekelezaji wa Muongozo wa Awali wa kufanya Biashara ili kuona namna gani
inanufaika na soko la AfCFTA.

“Nchi zetu za Afrika zinazalisha bidhaa zinazofanana hivyo ni lazima tathimini yetu ifanyike kwa kina ili kupata bidhaa zenye upekee, tofauti na bidhaa za nchi nyingine na kuleta tija katika maendeleo ya biashara nchini’’ alisisitiza Balozi Mbundi.




Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi (Mb.) akizungumza na wabunge wa Bunge la Afrika walipomtembea ofisini kwake jijini Dodoma tarehe 22october 2024.


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi akichangia mada wakati wa mazunguzo.


Naibu Waziri Mh. Cosato David Chumi akizungumza na sehemu ya wabunge waliokuja nchini kwa ziara ya siku nane.



Picha ya pamoja