Tuesday, May 12, 2015

Waziri Membe aongoza Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa EAC


Waziri wa Mambo wa Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri  wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kujadili mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini Burundi. Kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Richard Sezibera 

Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jopo la Watu Mashuhuri wanaofuatilia hali ya usalama nchini Burundi akijadili jambo na Mjumbe wakati wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri uliofanyika kujadili hali nchini Burundi
Wajumbe mbalimbali wakimsikiliza Waziri Membe (hayupo pichani). 
Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Mhe. Louise Mushikiwabo  
 Mkurugenzi Msaidizi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Burundi Bi. Victoria Mwakasege akinukuu yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye mkutano.
Mkutano ukiendelea.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe (Mb.) akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba kabla ya kuanza kwa  mkutano wa dharura wa Mawaziri wa Mambo ya Nje 
Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Mhe. Mushikiwabo (aliyetangulia), akiongozana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Mhe. Amina Mohammed kuelekea kwenye ukumbi wa mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

Picha na Reginald Philip.
==============================


Waziri Membe aongoza Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa EAC

Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) umefanyika leo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuandaa agenda za Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi  wa Jumuiya  hiyo utakaofanyika tarehe 13 Mei, 2015 kujadili hali ya usalama nchini Burundi.

Akifungua Mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa EAC, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) alisema kuwa nchi ya Burundi inapita kwenye wakati mgumu wakati ikijiandaa kwa uchaguzi mkuu utakaofanyika hivi karibuni, hivyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ameitisha mkutano huo wa dharura kujadili suala hilo na kutafuta ufumbuzi.

Waziri Membe alieleza kuwa, hali ya usalama nchini humo kwa sasa si shwari huku kukiwa na mfululizo wa maandamano ya wananchi na tayari zaidi ya Wakimbizi 50,000 wamekimbilia nchi  jirani ikiwemo Tanzania, Rwanda na Uganda.

“Lengo mojawapo la Jumuiya ya EAC ni kuhakikisha nchi zote wanachama zinakuwa katika hali ya amani, usalama na utulivu hivyo ni wakati muafaka mkutano huu kufanyika” alisisitiza Waziri Membe

Mhe. Membe aliongeza kuwa Mkutano huo ambao umehudhuriwa na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa EAC yaani Kenya, Rwanda, Burundi na Uganda pamoja na mambo mengine utapokea na kujadili Taarifa ya Timu ya Watu Mashuhuri (Eminent Persons) walioteuliwa kufuatilia hali ya usalama nchini Burundi kutoka EAC na Jumuiya ya Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) inayoongozwa na Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Jaji Joseph Sinde Warioba.

Aidha, Mkutano huo pia utapokea na kujadili Taarifa ya Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje waliotembelea Burundi hivi karibuni kwa ajili ya kupata taarifa za ndani za hali ilivyo nchini humo; Taarifa ya Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Eneo la Maziwa Makuu; Taarifa ya Kamishna wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika na Taarifa ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi.

Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki chini ya Uenyekiti wa Rais Kikwete utafanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 13 Mei, 2015 na utahudhuriwa na Marais wan chi wanachama wa Jumuiya hiyo akiwemo Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Uganda, Mhe. Paul Kagame, Rais wa Rwanda, Mhe. Pierre Nkurunziza, Rais wa Burundi na Mhe. Uhuru Kenyatta, Rais wa Kenya.

Viongozi wengine walioalikwa kushiriki Mkutano huo ni pamoja na Rais wa Afrika Kusini, Mhe. Jacob Zuma ambaye atawakilishwa na Naibu Rais, Mhe. Cyril Ramaphosa, Kamishna wa Umoja wa Afrika, Mhe. Bibi Nkosazana Dlamini Zuma, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ukanda wa Maziwa Makuu, Bw. Said Djinnit; Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR), Prof. Ntumba Luaba, Kamishna wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika na Wawakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU).

-Mwisho-

Wednesday, May 6, 2015

Waziri Membe aongoza Mawaziri wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye mazungumzo Burundi

Mhe. Pierre Nkurunziza, Rais wa Jamhuri ya Burundi akisalimiana na kumkaribisha Ikulu Mhe. Bernard K. Membe, Wazairi wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kiongozi wa mazungumzo maalaum baina ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Burundi.



Mhe. Pierre Nkurunziza, Rais wa Jamhuri ya Burundi kwenye mazungumzo na  Mhe. Bernard K. Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Mhe. Louise Mushikiwabo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda na Mhe. Amina Mohamed, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya.

Mwakilishi Mkazi wa UNDP atembelea Wizara ya Mambo ya Nje

Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Celestine Mushy akimkabidhi kitabu kinachozungumzia Hifadhi za Taifa zilizopo nchini Tanzania Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchni, Bwa. Alvaro Rodriguez alipomtembelea ofisini kwake
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Celestine Mushy akimwelezea Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchni, Bwa. Alvaro Rodriguez juu ya Kahawa inayozalishwa Tanzania  na Kampuni ya Panone (Panone Fresh Coffee) 
Balozi Mushy akimkabidhi Bwa. Rodrigues Kahawa iliyofungwa vizuri na kampuni ya Panone



Picha na Reginald Philip

Balozi wa Uholanzi atembelea Wizara ya Mambo ya Nje.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb) kulia akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Mhe. Jaap Fredriks ofisini kwake leo.  Mazungumzo hayo yalihusu kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Uholanzi.

Mazungumzo kati ya Mhe. Naibu Waziri na Mhe. Balozi yanaendelea. Wengine katika picha, kutoka kulia ni Bw. Adam Issara, Anthony Mutafya na Bi. Zulekha Tambwe ambao ni maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Naibu Waziri, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim akiagana na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Mhe. Jaap Fredriks.

Tuesday, May 5, 2015

Taarifa kwa Vyombo vya Habari








Simu: 255-22-2114615, 211906-12
Barua pepe: nje@nje.go.tz
Barua pepe: gcu@nje.go.tz
Tovuti : www.foreign.go.tz

Nukushi: 255-22-2116600

              

 


           


20 KIVUKONI FRONT,
   P.O. BOX 9000,
       11466 DAR ES SALAAM, 
                                    Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Awamu ya Tatu yenye jumla ya Watanzania 39 kutoka Yemen wanatarajiwa kuwasili nchini tarehe 06 Mei, 2015 ikiwa ni jitihada za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwarejesha nyumbani kufuatia mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yanayoendelea nchini humo.

Watanzania hao wakiwemo Wanafunzi watawasili nchini kwa Ndege ya Shirika la Qatar namba QR 1349 majira ya saa 1.55 (saa moja) asubuhi.

Kurejea kwa Watanzania hao kutafanya jumla ya Watanzania waliorejea kutoka Yemen hadi hivi sasa kuwa 62 kati ya   Watanzania 69 waliojiandikisha kurudi  huku jitihada za kuwaandikisha wengine zikiendelea kufanywa na Ubalozi wa Tanzania nchini Oman.

Awamu ya kwanza ya Watanzania waliorejea ilihusisha familia ya watu watano huku awamu ya pili ilikuwa na Watanzania 18.

Itakumbukwa kuwa, hivi karibuni Serikali kupitia Waziri wa Mambo  ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe ilitangaza kuwarejesha nchini Watanzania waliopo Yemen kufuatia machafuko yanayoendelea nchini humo.


IMETOLEWA NA: WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM.
05 MEI, 2015


Monday, May 4, 2015

Waziri Membe afanya Mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe akisalimiana naWaziri wa Mambo ya Nje wa Burundi,  Mhe. Laurent Kavakure walipokutana kwa chakula cha mchana na kufanya mazungumzo katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine Viongozi hao walizungumzia masuala ya kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizi mbili
Waziri Membe akimweleza jambo lililomfurahisha Waziri Kavakure
Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi, Mhe. Laurent Kavakure akizungumza huku Waziri Membe akimsikiliza 
Mazungumzo yakiendelea
Waziri Kavakure akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu mteule wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Hassan Simba Yahya 
Waziri Kavakure akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa  Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje, Bi. Zuhura Bundala.
Mhe. Kavakure akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika Wizara ya Mambo ya Nje, Bi. Mindi Kasiga
Waziri Membe (katikati) akimtambulisha Waziri wa Maliasili na Utalii (Kushoto) Mhe. Lazaro Nyalandu kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi Mhe. Laurent Kavakure. 
Waziri Membe (Wa Nne kutoka Kushoto), Waziri Kavakure (wa tatu kutoka kulia), Balozi wa Burundi nchini Tanzania Mhe. Issa Ntambuka (Wa pili kutoka kulia), Wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu Mteule Balozi Simba Yahya, (wa tatu kushoto) ni Mshauri wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi Balozi Hassan Lukara. 

Picha na Reginald Philip
==============================================

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA


Simu: 255-22-2114615, 211906-12
Barua pepe: nje@nje.go.tz
Barua pepe: gcu@nje.go.tz
Tovuti : www.foreign.go.tz

Nukushi: 255-22-2116600

              

 


          

 20 KIVUKONI FRONT,
          P.O. BOX 9000,
   11466 DAR ES SALAAM, 
                     Tanzania.

 



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), leo amefanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi, Mhe. Laurent Kavakure jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro. Mhe. Kavakure aliwasili nchini tarehe 03 Mei 2015.

Wakati huo huo, Mhe. Membe ataongoza ujumbe wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenda Burundi siku ya Jumatano tarehe 06 Mei 2015 kufanya mazungumzo na Serikali ya Burundi kuhusu hali ya kisiasa inayoendelea nchini humo.

-Mwisho-
Imetolewa na:
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam
04 Mei 2015


Friday, May 1, 2015

Balozi Njoolay akabidhi barua ya pongezi kwa Rais Mteule wa Nigeria Generali Mstaafu Muhammadu Buhari

Balozi wa Tanzania, Nchini Nigeria Mhe. Daniel Ole Njoolay, alimkabidhi Rais Mteule wa Nigeria Generali Mstaafu Muhammadu Buhari, barua ya pongezi toka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Jakaya Mrisho Kikwete. 
Balozi wa Tanzania, Nchini Nigeria Mhe. Daniel Ole Njoolay (kulia) akiwa katika mazungumzo na Rais Mteule wa Nigeria Generali Mstaafu Muhammadu Buhari, mara baada ya kukabidhi barua ya pongezi toka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Jakaya Mrisho Kikwete
Balozi Daniel Ole Njoolay akiendelea kuelezea jambo kwa Rais Mteule wa Nigeria Generali Mstaafy Muhammad Buhari mara baada ya kumaliza mazungumzo


====================================

Tarehe 28 Aprili 2015 Balozi wa Tanzania, Nchini Nigeria Mhe. Daniel Ole Njoolay, alimkabidhi Rais Mteule wa Nigeria Generali Mstaafu Muhammadu Buhari, barua ya pongezi toka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Jakaya Mrisho Kikwete. 

Rais Mteule Jenerali Buhari alimshukuru Rais Kikwete kwa salamu hizo na kukiri kwamba alikwishapokea simu ya pongezi kutoka kwake mara tu baada ya matokeo kutangazwa. Wakati wa mazungumzo yake na Balozi Njoolay, Generali Buhari aliisifu Tanzania kwa kudumisha amani na utulivu na kusema kuwa anaamini kwamba Tanzania itaendelea kuwa kitovu cha amani na utulivi Barani Afrika. Imetolewa na Ubalozi Tanzania, Abuja

Thursday, April 30, 2015

Stop Flocking in South Africa, President Mugabe


Heads of State and government of the Southern African Development Community (SADC), meeting in Harare, Zimbabwe yesterday condemned the recent attacks against African migrants in parts of Durban and Johannesburg in South Africa.
The summit meeting was reacting to a briefing by South Africa President Jacob Zuma on the nature of the xenophobic attacks and measures taken by his government to restore peace.

According to a communique issued after the meeting, "Summit commended the measures that the government of South Africa has put in place and resolved to work together to deal with the situation and ensure it does not recur."
The attacks affected the citizens of SADC member countries of Zimbabwe, Mozambique, Malawi, Zambia and Tanzania, which were forced to evacuate their people.

The violence heightened tension between South Africa and its neighbours, some of whom threatened retaliatory measures.
But briefing the media after the summit yesterday, The SADC Chairman, President Robert Mugabe, said the situation should not be blamed on South Africa alone.
He said an virtually unchecked influx of migrants from neighbouring countries was stretching resources to the limit in South Africa, where the majority blacks were living in dire conditions.

"Only the whites are living well there. Our people should not have the instinct to rush to Johannesburg in the false hope that it is heaven," he said.
The SADC Chair said one way to arrest the influx was for SADC member countries to improve their economies and attract their youth to stay and work at home.
Hundreds of Zimbabweans, Malawians, Mozambicans and Zambians were evacuated following the attacks, but millions more, who are largely unskilled, remain in South Africa.

Twenty six Tanzanians were facilitated by the government to return home last week and the Tanzania High Commission in Pretoria is looking for others who may wish to return home. There was no Tanzanian among eight foreigners reported to have been killed in the attacks

President Zuma has been quoted in the media as saying he would address the root causes of the xenophobic attacks, which he said were poverty, unemployment and immigration.

An estimated 53 percent of the South African population lives below the poverty line, according to the United Nations.

(Ends)
 

Arrival of Dr. Bilal in Zimbabwe 

Vice President of the United Republic of Tanzania, H.E Dr. Mohamed Gharib Bilal is received by Tanzania Government Officials when he arrived at the Melkles Hotel in Zimbabwe. Dr. Bilal represented President Jakaya Mrisho Kikwete at the SADC Heads of State Extra Ordinary Summit on Industrialization held in Harare yesterday.

 

High Commissioner of Tanzania to Zimbabwe, H.E Adadi Rajab makes a briefing to the Vice President prior the SADC Summit. On the left is the Minister of Industry and Trade, Hon. Dr. Abdallah Kigoda (MP).

High Commissioner of Tanzania to South Africa, H.E Radhia Msuya contributes a point during a briefing session towards SADC Summit.


Government Leaders and Officials during the briefing session.

 

Ubalozi wa Tanzania nchini Malaysia washerehekea Miaka 51 ya Muungano

Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Mhe. Dkt. Aziz Ponary Mlima akiwa  na mkewe Mama Mkola Mlima pamoja na Wafanyakazi wa Ubalozi wakiwapokea wageni waalikwa kwenye maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Ubalozi wa Tanzania nchini humo uliandaa sherehe fupi kuuenzi Muungano.
Balozi Mlima akitoa hotuba fupi wakati  wa maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Balozi Mlima akikata keki kuadhimisha miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Anayeshuhudia ni Mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo ambaye ni Naibu Waziri wa Biashara ya Kimataifa na Viwanda wa Malaysia, Seneta Deto' Lee Chee Leong.
Juu na Chini ni Wageni waalikwa wakimsikiliza Balozi Mlima (hayupo pichani) alipowahutubia wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika  na Zanzibar
Zawadi ya Muungano