Thursday, January 18, 2018

Tanzania yashiriki maonesho ya utalii ya kimataifa nchini Uholanzi






Washiriki kutoka Tanzania wakiwa katika banda la Tanzania kwenye Maonesho maarufu ya Utalii ya Kimataifa (Vakantiebeurs 2018) yaliyofanyika hivi karibuni mjini Utrecht, Uholanzi.

Kutoka kushoto ni Bw. Willy Lyimo wa Bodi ya Utalii (TTB), Bibi Agnes Kiama Tengia, Afisa Ubalozi, Bw. Susuma Kusekwa wa Hifadhi za Taifa (TANAPA), Bw. John Sung’are wa African Wildcats Expeditions Ltd. (Arusha), Bibi Naomi Z. Mpemba, Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Tanzania The Hague Uholanzi na Bw. Mushtaqali Abdalla wa Bobby Tours and Safaris (Arusha).

Kaimu Balozi Bibi Naomi Z. Mpemba akimsikiliza mteja aliyefika kwenye banda la Tanzania.

Bw. Iddi Mavura wa NCAA na Bw. Susuma Kusekwa wa TANAPA wakiwasiliza wateja waliofika kwenye banda la Tanzania katika Maonesho ya Utalii ya Kimataifa ya Vakantiebeurs 2018.

Bi. Sophia Tumsifu, Mtumishi wa Ubalozi akiwapa maelezo wateja waliofika katika banda la Tanzania ambapo pamoja na kupata taarifa kuhusu vivutio vya Tanzania, walipata pia ladha ya vyakula vya Tanzania.

Bibi Mwajuma Kitano, Mwanamuziki Mtanzania anayeishi Uholanzi, akiwa pamoja na wanafunzi wake ambao ni raia wa Uholanzi, kwa pamoja wakitumbuiza katika banda la Tanzania katika Maonesho ya Utalii ya Kimataifa ya Vakantiebeurs 2018.

Monday, January 15, 2018

Waziri Mahiga apokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Taifa la Israel


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Taifa la Israel mwenye makazi yake Nairobi-Kenya, Mhe. Noah Gal Gendler. Makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 15 Januari 2017. 
Mhe. Waziri Mahiga akizungumza na Mhe. Gendler ambapo mazungumzo yao yalijikika katika kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia unaolenga kuinua uchumi kwa kufanya maboresho katika sekta ya uwekezaji, Utalii na Kilimo kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania na Israel.
Mazungumzo yakiendelea.

Picha ya pamoja Mhe. Waziri Mahiga, Mhe. Gendler na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati Bw. Hangi Mgaka.