Wednesday, February 17, 2021

WIZARA YA MAMBO YA NJE YAIAHIDI USHIRIKIANO PAPU

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge mapema leo amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (Pan African Postal Union - PAPU) wenye Makao Makuu yake jijini Arusha, Tanzania Mhe. Younouss Djibrine, alipotembelea Makao Makuu ya Wizara hiyo jijini Dodoma. 


Djibrine ameeleza kuwa pamoja na masuala mengine ziara hiyo imelenga kuishukuru Serikali chini ya Uongozi mahiri wa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa ushirikiano inayoendelea kuutoa kwa Taasisi hiyo ya Kimataifa katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku. Djibrine pia alitumia nafasi hiyo kuelezea hatua ya maendeleo iliyofikiwa katika ujenzi wa mradi mkubwa wa jengo la ofisi za Taasisi hiyo unaoendelea kufanyika jijini Arusha. Djibre ameeleza kuwa Sekali ya Tanzania imeendelea kuwa rafiki na kutoa ushirikiano wakati wote ambao Taasisi hiyo imekuwa ikihitaji, hivyo kuifanya itekeleze majukumu yake kwa ufanisi na mafanikio.


Kwa upande wake Balozi Brigedia Jenerali Ibuge amempongeza na kumshuruku Djibrine kwa uongozi wake mahiri katika kipindi chote alichoiongoza PAPU hasa katika kusimamia kwa mafanikio programu mbalimbali za Umoja huo na mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi za Taasisi hiyo. Licha ya hayo Balozi Brigedia Jenerali Ibuge amemwahidi Mhe. Djibrine kuwa Wizara na Serikali kwa ujumla itaendelea kutoa ushirikiano kwa Taasisi hiyo katika utekelezaji wa majukumu yake na hasa katika utatuzi wa changamoto mbalimbali ikiwemo za kiutendaji na zakimazingira kadri zitakavyokuwa zikijitokeza.


Wazo la kuanzishwa kwa Umoja wa Posta wa Afrika (Pan African Postal Union – PAPU) lilitokana na Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) uliofanyika jijini Libreville, Gabon mwaka 1977 kwa lengo la kusimamia maendeleo ya Sekta ya Posta Afrika. Baadae, tarehe 18 Januari 1980 Umoja huo ulianzishwa rasmi na Mkutano wa 35 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika uliofanyika jijini Arusha Tanzania tarehe 8 hadi 18 Januari 1980.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge akisalimiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (Pan African Postal Union - PAPU) Mhe. Younouss Djibrine alipowasili katika ofisi za Wizara jijini Dodoma.


Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (Pan African Postal Union - PAPU) Mhe. Younouss Djibrine akisaini kitabu cha wageni alipowasili alipowasili katika ofisi za Wizara jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge (kulia) akimsiliza Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (Pan African Postal Union - PAPU) Mhe. Younouss Djibrine walipokutana kwa mazungumzo jijini Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge (kulia) akielezea jambo wakati wa mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (Pan African Postal Union - PAPU) Mhe. Younouss Djibrine yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge (katikati) Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (Pan African Postal Union - PAPU) Mhe. Younouss Djibrine (kushoto) na Mkuu wa Mawasiliano na Mkakati Bw. Amadou Amadou wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge (katikati) Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (Pan African Postal Union - PAPU) Mhe. Younouss Djibrine (kushoto) na Mkuu wa Mawasiliano na Mkakati Bw. Amadou Amadou wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo



Tuesday, February 16, 2021

BALOZI BRIGEDIA JENERALI IBUGE; USHAWISHI WA TANZANIA BADO NI IMARA KIKANDA NA KIMATAIFA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge amaeleza kuwa nguvu ya ushawishi wa Tanzania katika majukwaa ya kikanda na kimataifa bado upo imara, licha ya Tanzania kutoa mchango mkubwa katika ukombozi wa Bara la Afrika na uanzishwaji wa Jumuiya za Kikanda kama vile Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) hadi hivi sasa Tanzania bado ni kinara katika kutetea na kuadai maslahi ya Bara la Afrika.

Balozi Brigedia Jenerali Ibuge, amebainisha haya alipokuwa akizungumza na wadau kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) ambao waliitemebelea Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma kwa lengo la kujifunza kuhusu majukumu ya Wizara, hasa katika kutetea maslahi ya Nchi nje ya mipaka ya Tanzania. Katibu Mkuu aliendelea kubainisha kuwa Wizara katika utekelezaji wa sera ya mambo ya nje pamoja na mambo mengine inahakikisha kuwa inatoa kipaumbele kwenye kulinda maslahi ya Nchi ikiwewo ulinzi na usalama.


NDC kwa upande wao wameipongeza Wizara kwa kazi nzuri inayofanywa na Ofisi zake za Ubalozi sehemu mbalimbali duniani katika kutangaza fursa zilizopo nchini kwenye maeneo yao ya uwakilishi madhalani utalii, biashara ya madini na mazao ya kilimo, pia kuvutia wawekezaji kuja kuwekeza nchini.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wadau na uongozi wa NDC na Watendaji wa Wizara.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na wadau kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) walipofanya ziara ya mafunzo Wizarani.

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge akipokea kalenda kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha NDC Brigedia Jenerali Ibrahim Michael Muhona baada ya kumaliza kutoa mhadhara
Sehemu ya Wadau kutoka NDC wakifuatilia mhadhara uliokuwa ukitolewa na viongozi wa Wizara
Mkurugenzi wa Siasa,Ulinzi na Usalama Balozi Stephen P. Mbundi akifafanua jambo kwa wadau kutoka NDC wakati walipofanya ziara ya mafunzo Wizarani

TANZANIA MBIONI KUSAINI MKATABA WA ENEO HURU LA BIASHARA YA UTATU COMESA-EAC-SADC


Tanzania imeshiriki katika Mkutano wa Pili wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Utatu uliofanyika kwa njia ya video. Katika mkutano huo moja ya agenda ilikuwa nchi Wanachama kutoa taarifa kuhusu hatua iliyofikiwa katika kusaini na kuridhia mkataba wa kuanzishwa kwa Eneo Huru la Biashara ya Utatu ya COMESA-EAC-SADC. Katika mkutano huo Tanzania kupitia Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Dkt. Leonard Chamuriho imeeleza kuwa ipo katika hatua za kusaini na kuridhia mkataba huo. 

Mkutano huo ulioitishwa kwa dharura pia ulilenga kupitia na kujadili rasimu ya mwongozo wa utatu wa usimamizi na ufuatiliaji wa uvukaji salama wa watu na bidhaa mipakani katika kipindi hiki cha Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO-19). Jumuiya za COMESA, EAC na SADC baada ya kugundua kuwa nchi mbalimbali ziliaandaa miongozo ya kudhibiti maambukizi ya UVIKO-19 bila kuathiri uchumi na biashara iliamua kuratibu maandalizi ya miongozo ya kikanda ili kuondokana na changamoto za biashara baina ya nchi wanachama. Nchi wanachama zimekubaliana kuwa mkutano uitishwe tena baada ya wiki mbili ili kujadili agaenda hii na kufikia maamuzi ya pamoja.

Katika mkutano huo kwa upande wa Tanzania ulihudhuriwa na Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Geofrey Pinda Watendaji na Maafisa mbalimbali wa Serikali


Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Dkt. Leonard Chamuriho, Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Geofrey Pinda wakifuatilia Mkutano wa Pili wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Utatu uliokuwa ukiendelea kwa njia ya video


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge akifuatilia Mkutano wa Pili wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Utatu uliokuwa ukiendelea kwa njia ya video
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Dkt. Leonard Chamuriho akichangia jambo katika Mkutano wa Pili wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Utatu uliofanyika kwa njia ya video

Badhi ya Watumishi wa Serikali waliohudhuria Mkutano wa Pili wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Utatu uliokuwa ukiendelea kwa njia ya video wakifualia mjadala uliokuwa ukiendelea
Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Dkt. Leonard Chamuriho, Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Geofrey Pinda wakifuatilia Mkutano wa Pili wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Utatu uliokuwa ukiendelea kwa njia ya video

Mkutano ukiendelea

 

Saturday, February 13, 2021

BALOZI IBUGE: SIJARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA MAJENGO CHUO CHA DIPLOMASI

 Na Mwandishi wetu,

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ameonesha kutoridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa majengo ya mihadhara katika chuo cha Diplomasia na kumuagiza Mkandarasi anayetekeleza mradi huo kuzingatia thamani ya fedha, muda wa mkataba na ubora.

Balozi Ibuge ametoa maagizo kwa Mkandarasi huyo ambaye ni Kampuni ya Casco Construction pamoja na mshauri muelekezi Ask architects wakati alipotembelea mradi huo katika chuo cha Diplomasia leo jijini Dar es Salaam kusema kuwa endapo Mkandarasi hata fanya hivyo atakuwa amekiuka masharti ya mkataba na mkataba wake utasitishwa mara moja.

“Huu mradi ni mradi wenye maslahi ya Taifa majadiliano yaishe leo mkataba ulishaisha tangu mwezi Disemba 2020, hizi ni hela za walipa kodi…..nataka nione thamani halisi ya fedha [Value for Money] ya walipa kodi katika mradi huu, siatakubali kupoteza fedha za walipa kodi,” Amesema Balozi Ibuge

Katibu Mkuu ameuagizo pia uongozi wa chuo hicho kuhakikisha kuwa unasimamia ujenzi wa majengo hayo kwa karibu zaidi na umakini ili kuiwezesha serikali kupata thamani halisi ya fedha katika mradi huo wenye maslahi mapana ya Taifa.

Awalia akiongea na wahadhiri pamoja na wafanyakazi katika chuo hicho Balozi Ibuge amewataka wote kwa pamoja kuhakikisha kuwa wanatekeleza diplomasia ya uchumi kutokana na mabadiliko ya dunia.

“Najua mmeanzisha mitaala inayogusia masuala ya diplomasia ya uchumi hadi mmeanza kuanzia baadhi ya matawi katika baadhi ya mikoa hili ni jambo jema, lakini uwezo wa nyinyi kuleta [link] ya utekelezaji wa diplomasia ya uchumi ambao ndiyo Wizara yetu inasimamia…unapohusisha na nchi nyingine ni lazima utafiti wenu pamoja na kuboresha wigo wa utekelezaji wa diplomasia ya uchumi,”

Balozi Ibuge ameongeza kuwa diplomasia ya uchumia inaambatana na siasa pamoja na diplomasia ya utamaduni wetu hasa kwenye lugha ya kiswahili hiyo ndiyo sehemu ya mahusiano yetu na wengine.

“Urathi wa ukombozi kusini mwa Afrika anayehusika ni Tanzania sasa Chuo cha Diplomasia ambapo ndipo mawazo mazuri ya namna bora ya sisi kuhakikisha tunaiendeleza na kuishindania na kuhakikisha hakuna mwingine wa kushindana na sisi, njia pekee ni kupitia kwenu nyinyi na tafiti zenu,” Amesema Balozi Ibuge

Kwa upande wake Mkandarasi anayetekeleza mradi huo Mhandisi Cosmas Salufu kutoka kamupuni ya ujenzi ya Casco, pamoja na mshauri elekezi mhandisi Ally Simbano kutoka kampuni Ask Architects kwa pamoja wameahidi kutekeleza maagizo ya Katibu Mkuu na kuhakikisha kuwa thanami halisi ya fedha inapatikana katika mradi huo.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge (aliyesimama) akiongea na wahadhiri pamoja na wafanyakazi wa chuo cha Diplomasia leo Jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara chuoni hapo 


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akiongea na uongozi wa chuo cha Diplomasia leo Jijini Dar es Salaam  


Afisa Miliki wa Chuo cha Diplomasia, Mhandisi Athumani Mashaka akimueleza jambo Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge wakati akitembelea mradi wa ujenzi wa majengo chuoni hapo


Mhandisi Cosmas Salufu pamoja na Mshauri Elekezi Mhandisi Ally  wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge wakati wa ziara ya ukaguzi wa majengo




Friday, February 12, 2021

MKUTANO WA SADC TROIKA WASOGEZA MBELE MKUTANO WA WAKUU WA NCHI

 Na Mwandishi wetu,

Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali za Utatu wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC- TROIKA) uliopangwa kufanyika mwezi Machi 2021 umesogezwa mbele hadi mwezi Mei au Juni 2021 kutokana na changamoto za (Covid 19).

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha (Mb) amesema kuwa mkutano huo umekutana kwa lengo la kupitia na kuridhia mapendekezo ya Mawaziri wa afya wa SADC uliofanyika mwishoni wa mwezi Februari 2021.  

“Awali mawaziri wa Afya wa SADC walipendekeza kuwa mkutano wa Baraza la Mawaziri ufanyike kwa njia ya mtandao pamoja na ule wa Wakuu wa Nchi uliokuwa umepangwa pia kufanyika mwezi Machi usogezwe mbele hadi mwezi Mei au Juni 2021 kutegemeana na hali ya maambukizi ya ugonjwa wa COVID 19 itakavyokuwa na kuongeza kuwa mikutano mingine yote itafanyika kwa njia ya mtandao (Video Conference) hadi hapo hali ya maambukizi itakapokuwa imetengemaa,” Amesema Mhe. Ole Nasha

Mkutano wa (SADC TROIKA) umetanguliwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu ambapo, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ameeleza kutokana na hali halisi ya kujitokeza kwa kirusi cha Covid 19 kilichojitokeza kusini mwa Jangwa la Afrika imekuwa vigumu kufanyika kwa mkutano huo wa ana kwa ana na badala yake imeamuliwa mkutano huo usogezwe mbele hadi mwezi Mei au Juni 2021.

“Mwezi Januari 2021 Mawaziri wa Afya wa SADC walikutana na kufanya mkutano kwa njia ya mtandao na kufikia maazimio kuwa mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali uhairishwe hadi mwezi Mei au Juni kutegemeana na hali ya COVID 19 itakapokuwa imetengemaa……. ambapo pamoja na mambo mengine, mkutano wa Baraza la Mawaziri umeridhia kusogezwa mbele kwa mkutano huo,” Amesema Balozi Ibuge

Utatu wa SADC TROIKA kwa sasa unaundwa na nchi za Msumbiji, Tanzania na Malawi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha (Mb) akiwa amesimama wakati wimbo wa Taifa wa Msumbiji ulipokuwa ukipigwa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Utatu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC TROIKA) uliofanyika kwa njia ya mtandao  


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha (Mb) akiandika jambo wakati wa mkutano cha SADC TROIKA) uliofanyika kwa njia ya mtandao


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akichangia mada katika mkutano wa Makatibu Wakuu wa SADC TROIKA 


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akifuatilia mkutano wa Makatibu Wakuu wa SADC TROIKA