Sunday, April 6, 2025

WAZIRI KOMBO: TUANGALIE MAENEO YENYE TIJA KWA MAENDELEO YA NCHI ZETU



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) akizungumza na ujumbe uliowasili Nchini Angola kwa ziara rasmi ya Kitaifa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), amesisitiza umuhimu wa kuangazia maeneo yenye tija kwa maendeleo ya pamoja kati ya Tanzania na Angola, akibainisha kuwa ushirikiano wa kweli lazima ujikite kwenye maeneo yenye fursa halisi za kiuchumi, kijamii na kidiplomasia.

Akizungumza jijini Luanda, Angola, mbele ya ujumbe wa Tanzania uliowasili kushiriki katika maandalizi ya ziara kitaifa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Waziri Kombo alisema kuwa ziara hiyo inalenga kufungua ukurasa mpya wa ushirikiano wa kimaendeleo kati ya mataifa haya mawili.

“Ni wajibu wetu kuhakikisha kuwa maeneo tutakayojadili katika ziara hii yanaakisi malengo ya kimaendeleo ya nchi zetu. Tuangalie maeneo yenye tija ya moja kwa moja kwa wananchi wetu,” alisema Mhe. Kombo.

Waziri Kombo aliwahimiza wajumbe kutoka taasisi na wizara mbalimbali za Tanzania kutumia fursa ya maandalizi haya kuchambua kwa kina maeneo yatakayochangia kukuza uchumi, kuongeza ajira, na kuinua maisha ya wananchi kupitia ushirikiano wa kimkakati.

Amesema kuwa ushirikiano kati ya Tanzania na Angola unapaswa kuimarishwa zaidi katika sekta muhimu kama biashara na uwekezaji, uchumi wa buluu, mafuta na gesi, madini, afya, elimu, miundombinu, utalii, mawasiliano, pamoja na masuala ya ulinzi na usalama wa kikanda.

“Ziara hii ya kihistoria ya Rais Samia inatarajiwa kuleta matokeo makubwa, siyo tu kwa upande wa mahusiano ya kidiplomasia, bali pia katika kutafsiri kwa vitendo fursa zilizopo kwa manufaa ya wananchi wetu,” aliongeza Waziri Kombo.

Alisisitiza kuwa Tanzania ina nia ya dhati ya kushirikiana na Angola katika miradi ya pamoja ya maendeleo ambayo itachochea ukuaji wa sekta za kimkakati, kuboresha mifumo ya uchumi na kuimarisha urafiki wa muda mrefu kati ya mataifa hayo mawili.

Ujumbe wa Tanzania ukiwa chini ya uongozi wa Mhe. Waziri Kombo, upo nchini Angola kwa ajili ya maandalizi ya ziara kitaifa ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, inayotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 7 hadi 9 Aprili 2025.

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Katikati) akiwa katika picha na Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Shaaban Ali Othman (kushoto) pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujuenga Taifa, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (kulia)
 

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujuenga Taifa, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza katika kikao hicho.
 
Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Shaaban Ali Othman akizungumza mada.
 
Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Lut. Jen Mathew Edward Mkingule, ambaye pia anaiwakilisha Tanzania nchini Angola akizungumza wakati wa kikao hicho.
 

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara akichangia mada katika kikao hicho.

 
 

Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Lut. Jen Mathew Edward Mkingule, ambaye pia anaiwakilisha Tanzania nchini Angola (kushoto), Mkurugenzi Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ally Bujiku (katikati) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa KItuo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri.
 

Mkurugenzi Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ally Bujiku akichangia mada wakati wa kikao hicho.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa KItuo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri.
 

Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Shaaban Ali Othman akizungumza wakati wa kikao hicho.
 


 


 

 
 

WAZIRI KOMBO AKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA ANGOLA KUJADILI MAANDALIZI YA ZIARA RASMI YA KITAIFA YA RAIS SAMIA.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Kushoto) akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Angola, Mhe. Tete António (Kulia).



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Angola, Mhe. Tete António, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Ziara ya Kitaifa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mazungumzo hayo, yamefanyika jijini Luanda, yamelenga kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na kiuchumi kati ya Tanzania na Angola, sambamba na kubadilishana uzoefu katika maeneo mbalimbali ya maendeleo ya kimataifa.

Aidha, viongozi hao wamejadili maandalizi ya ziara ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan inayotarajiwa kufanyika nchini humo tarehe 7- 9 Aprili 2025.

Viongozi hao pia wamesisitiza umuhimu wa ziara hiyo katika kuimarisha misingi ya ushirikiano kwa pande mbili hizo kwa maslahi ya wananchi wa Tanzania na Angola.

 



Mazungumzo yakiendelea

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (kulia) pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Lut. Jen Mathew Edward Mkingule, ambaye pia anaiwakilisha Tanzania nchini Angola (kushoto)

 



Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola Mhe. Tete António.

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (kushoto) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola Mhe. Tete António (kulia).

 


Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Lut. Jen Mathew Edward Mkingule, ambaye pia anaiwakilisha Tanzania nchini Angola (kulia) akiwa na Balozi wa Angola nchini   Mhe. Sandro de Oliveira baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo(Mb.) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola Mhe. Tete António.


WAZIRI KOMBO AWASILI ANGOLA

 




Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (kulia) akiwa amepokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola anayeshughulikia Masuala ya Utawala na Fedha, Mhe. Balozi Osvaldo dos Santos Varela


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), amewasili jijini Luanda, Angola ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Ziara ya Kitaifa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, nchini Angola inayotarajiwa kufanyika tarehe 7- 9 Aprili, 2025.

Alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa 4 de Fevereiro, Waziri Kombo alipokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola anayeshughulikia Masuala ya Utawala na Fedha, Mhe. Balozi Osvaldo dos Santos Varela, Balozi wa Angola nchini Tanzania, Mhe. Sandro de Oliveira na Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Lut. Jen Mathew Edward Mkingule, ambaye pia anaiwakilisha Tanzania nchini Angola.

Katika ziara hiyo, Mhe. Kombo ameambatana na Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Shaaban Ali Othman, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Stergomena Tax, pamoja na maafisa Wengine wa Serikali kutoka wizara na taasisi mbalimbali za umma.

Mhe. Waziri Kombo anatarajiwa kushiriki katika vikao vya maandalizi na mazungumzo ya awali na ujumbe wa Tanzania uliooko nchini humo kwa lengo la kuweka msingi madhubuti wa ziara hiyo ya kihistoria ya Mhe. Rais Samia.

Ziara hiyo inatarajiwa kuwa ya kihistoria, ikiwa ni ya kwanza kufanywa na Mhe. Rais Samia nchini Angola tangu aingie madarakani mwaka 2021.

 


 

 


Waziri wa Ulinzi na Jeshi kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiwa amepokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola anayeshughulikia Masuala ya Utawala na Fedha, Mhe. Balozi Osvaldo dos Santos Varela wakati wa kuwasili kwake Nchini Angola.



Waziri wa Ulinzi na Jeshi kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola anayeshughulikia Masuala ya Utawala na Fedha, Mhe. Balozi Osvaldo dos Santos Varela wakati wa kuwasili kwake Nchini Angola.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisalimiana na Balozi wa Angola nchini, Mhe. Sandro de Oliveira.

 

Waziri wa Ulinzi na Jeshi kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiwa na sehemu ya ujumbe wa mapokezi.


 

Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Shaaban Ali Othman (kushoto) pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (kulia) mara baada ya kuwasili nchini Angola kushiriki ziara rasmi ya Kitaifa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (wa kwanza kulia) akiwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (katikati) pamoja na Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Shaaban Ali Othman (kushoto) mara baada ya kuwasili nchini Angola kushiriki ziara rasmi ya Kitaifa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Lut. Jen Mathew Edward Mkingule pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara
 
Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Shaaban Ali Othman


 






 






Friday, April 4, 2025

WAZIRI KOMBO AWASILISHA TAARIFA YA WIZARA KATIKA KAMATI YA NUU

 

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,    Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.)



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), ameongoza Menejimenti ya Wizara katika kikao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusu utendaji wa Wizara na hali ya ushirikiano wa kidiplomasia wa Tanzania.

Katika kikao hicho, Mhe. Kombo aliwasilisha taarifa kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara, ikiwa ni pamoja na hali ya ushirikiano wa Tanzania na jumuiya za kikanda kama vile Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Aidha, Mhe. Kombo aliwasilisha hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa maazimio ya Bunge yanayohusu sekta ya mambo ya nje na diplomasia ya uchumi.

Waziri Kombo pia alieleza mafanikio ya Serikali katika utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje ambayo ni pamoja na kuimarika  kwa uhusiano wa kimataifa,hususan kuongezeka kwa ushawishi wa Tanzania katika masuala ya kidiplomasia na hatua zinazochukuliwa kushughulikia changamoto zinazoikabili Wizara.

Kwa upande wake, Kamati ya Bunge iliipongeza Wizara kwa kazi nzuri na kuishauri Wizara kuchukua hatua za makusudi kufanya maboresho zaidi ili Tanzania iweze kunufaika kikamilifu na ushirikiano wa kikanda na kimataifa.


Katika kikao hicho, Mhe. Kombo aliambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi, pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara hiyo, Balozi Samwel Shelukindo na Balozi Stephen Mbundi.
 
 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (kushoto), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi (katikati), pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo (kulia).