Sunday, April 6, 2025

WAZIRI KOMBO AKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA ANGOLA KUJADILI MAANDALIZI YA ZIARA RASMI YA KITAIFA YA RAIS SAMIA.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Kushoto) akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Angola, Mhe. Tete António (Kulia).



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Angola, Mhe. Tete António, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Ziara ya Kitaifa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mazungumzo hayo, yamefanyika jijini Luanda, yamelenga kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na kiuchumi kati ya Tanzania na Angola, sambamba na kubadilishana uzoefu katika maeneo mbalimbali ya maendeleo ya kimataifa.

Aidha, viongozi hao wamejadili maandalizi ya ziara ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan inayotarajiwa kufanyika nchini humo tarehe 7- 9 Aprili 2025.

Viongozi hao pia wamesisitiza umuhimu wa ziara hiyo katika kuimarisha misingi ya ushirikiano kwa pande mbili hizo kwa maslahi ya wananchi wa Tanzania na Angola.

 



Mazungumzo yakiendelea

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (kulia) pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Lut. Jen Mathew Edward Mkingule, ambaye pia anaiwakilisha Tanzania nchini Angola (kushoto)

 



Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola Mhe. Tete António.

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (kushoto) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola Mhe. Tete António (kulia).

 


Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Lut. Jen Mathew Edward Mkingule, ambaye pia anaiwakilisha Tanzania nchini Angola (kulia) akiwa na Balozi wa Angola nchini   Mhe. Sandro de Oliveira baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo(Mb.) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola Mhe. Tete António.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.