Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), amewasili jijini Luanda, Angola ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Ziara ya Kitaifa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, nchini Angola inayotarajiwa kufanyika tarehe 7- 9 Aprili, 2025.
Alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa 4 de Fevereiro, Waziri Kombo alipokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola anayeshughulikia Masuala ya Utawala na Fedha, Mhe. Balozi Osvaldo dos Santos Varela, Balozi wa Angola nchini Tanzania, Mhe. Sandro de Oliveira na Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Lut. Jen Mathew Edward Mkingule, ambaye pia anaiwakilisha Tanzania nchini Angola.
Katika ziara hiyo, Mhe. Kombo ameambatana na Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Shaaban Ali Othman, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Stergomena Tax, pamoja na maafisa Wengine wa Serikali kutoka wizara na taasisi mbalimbali za umma.
Mhe. Waziri Kombo anatarajiwa kushiriki katika vikao vya maandalizi na mazungumzo ya awali na ujumbe wa Tanzania uliooko nchini humo kwa lengo la kuweka msingi madhubuti wa ziara hiyo ya kihistoria ya Mhe. Rais Samia.
Ziara hiyo inatarajiwa kuwa ya kihistoria, ikiwa ni ya kwanza kufanywa na Mhe. Rais Samia nchini Angola tangu aingie madarakani mwaka 2021.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola anayeshughulikia Masuala ya Utawala na Fedha, Mhe. Balozi Osvaldo dos Santos Varela wakati wa kuwasili kwake Nchini Angola.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisalimiana na Balozi wa Angola nchini, Mhe. Sandro de Oliveira.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiwa na sehemu ya ujumbe wa mapokezi.
Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Shaaban Ali Othman (kushoto) pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (kulia) mara baada ya kuwasili nchini Angola kushiriki ziara rasmi ya Kitaifa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (wa kwanza kulia) akiwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (katikati) pamoja na Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Shaaban Ali Othman (kushoto) mara baada ya kuwasili nchini Angola kushiriki ziara rasmi ya Kitaifa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.