Friday, February 4, 2022

MAAFISA JWTZ WATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI ITALIA

Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakiongozwa na Mkuu wa Kurugenzi ya Intelijensia Makao Makuu ya Jeshi, Maj. Gen. Ramadhani Mrangira pamoja na Col. Abdallah Khalfan wametembelea Ubalozi wa Tanzania Jijini Roma, Italia.

Wakiwa Ubalozini walipokelewa na mwenyeji wao Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahmoud Thabit Kombo ambapo pamoja na mambo megine wamezungumzia masuala ya ushirikiano. Maafisa hao walikuwepo nchini Italia kwa shughuli za kikazi. 

Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahmoud Thabit Kombo katika picha ya pamoja na Mkuu wa Kurugenzi ya Intelijensia Makao Makuu ya Jeshi, Maj. Gen. Ramadhani Mrangira katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Italia 


Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahmoud Thabit Kombo katika picha ya pamoja na Mkuu wa Kurugenzi ya Intelijensia Makao Makuu ya Jeshi, Maj. Gen. Ramadhani Mrangira na Col. Abdallah Khalfan   


Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahmoud Thabit Kombo katika picha ya pamoja na Mkuu wa Kurugenzi ya Intelijensia Makao Makuu ya Jeshi, Maj. Gen. Ramadhani Mrangira, Col. Abdallah Khalfan pamoja na baadhi ya watumishi wa Ubalozi    


 

Thursday, February 3, 2022

WAZIRI MULAMULA AFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE WA SERIKALI YA URUSI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Masuala ya Kibinadamu kutoka nchini Urusi Bw. Yevgeny Primakov leo tarehe 03 Februari 2022 katika ofisi za Wizara jijini Dodoma.

Bw. Primakov ameambatana na Balozi wa Urusi nchini, Mhe. Yuri Popov pamoja na Mjumbe kutoka Serikali ya Urusi, Bw. Egor Utkin.

Wawakilishi hao kutoka Serikali ya Shirikisho la Urusi waliwasilisha ujumbe wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Urusi Mhe. Vladimirovich Putin.

Pamoja na mambo mengine viongozi hao walijadili juu ya kuimarisha ushirikiano uliopo na kwamba kwa sasa Tanzania na Urusi zinajikita zaidi katika kufungua maeneo mapya ya ushirikiano katika sekta za biashara, uwekezaji, utalii na masuala mengine ya kiuchumi kwa maslahi mapana ya mataifa hayo.

Waziri Mulamula alieleza kuwa Tanzania itaendelea kuimarisha uhusiano mzuri na wa kihistoria ambao uliasisiwa na Waasisi wa Mataifa hayo mawili.  

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kushoto) akipokea ujumbe wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia)kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Urusi Mhe. Vladimirovich Putin

Mazungumzo yakiendelea. 

Picha ya pamoja Mhe. Waziri na Ujumbe kutoka Serikali ya Urusi.
Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme, na Kulia kwake ni Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Mhe. Fredrick Kibuta.
 Kutoka kulia kwa Mhe. Waziri ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Masuala ya Kibinadamu nchini Urusi, Bw. Evgeny Primakov, Balozi wa Urusi nchini,
 Mhe. Yuri Popov pamoja na Mjumbe kutoka serikali ya Shirikisho la Urusi, Bw. Egor Utkin.

Waziri Mulamula akikabidhi shajara.
                                                                                      
Picha ya Pamoja.

Wednesday, February 2, 2022

BALOZI MULAMULA AKUTANA NA WAWEKEZAJI KUTOKA SAUDIA ARABIA

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (katikati) akizungumza na ujumbe wa wawekezaji kutoka Kiwanda cha Pioneers Chemical Factory cha nchini Saudi Arabia wanaotembelea Tanzania kuangalia fursa za biashara na uwekezaji.Kikao hicho kilifanyika ofisini kwa Mhe. Waziri Mttumba jijini Dodoma

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (katikati) akizungumza na ujumbe wa wawekezaji kutoka Kiwanda cha Pioneers Chemical Factory cha nchini Saudi Arabia (walioko kushoto) wanaotembelea Tanzania kuangalia fursa za biashara na uwekezaji.

Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini (katikati) katika kikao na Wawekezaji kutoka nchini Saudi Arabia(hawapo pichani) kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Hemedi Mgaza na kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi Balozi Edwin Rutageruka wakati wa kikao na wawkezaji hao



Waziri Mulamula (katikati) katika picha ya pamoja na ujumbe wa  wawekezaji kutoka Kiwanda cha Pioneers Chemical Factory cha nchini Saudi Arabia waliokuja nchini kuangalia fursa za biashara na uwekezaji baada ya kumalizika kwa kikao chao jijini Dodoma

Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini akiwa nje ya jengo la Wizara katika Mji wa Serikali Mtumba akizungumza na wawekezaji kutoka Kiwanda cha Pioneers Chemical Factory cha nchini Saudi Arabia aliokuja nao Tanzania kuangalia fursa za biashara na uwekezaji baada ya kumalizika kwa kikao chao na Mhe Waziri Mulamulajijini Dodoma


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa wawekezaji kutoka Kiwanda cha Pioneers Chemical Factory cha nchini Saudi Arabia wanaotembelea Tanzania kuangalia fursa za biashara na uwekezaji.

 

Mhe. Waziri Mulamula amekutana na Ujumbe wa wawekezaji hao ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma leo tarehe 02 February 2022. Ujumbe wa wawekezaji hao umeongozwa na Balozi wa Tanzania nchini Saudia Arabia Mhe. Ali Mwadini umeelezea utayari wao wa kuja kuwekeza nchini.

Akizungumza katika kikao hicho Balozi Mulamula amewakaribisha wawekezaji hao na kuwahakikishia mazingira rafiki ya uwekezaji nchini na kwamba Tanzania iko tayari kuwapokea.

Amesema Tanzania na Saudia zina uhusiano wa muda mrefu ambao una historia ya aina yake na kwamba uwekezaji kutoka kwa kampuni hiyo ni sehemu ya kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia.

Kampuni hiyo inayomiliki viwanda mbalimbali nchini Saudi Arabia inajishughulisha na uzalishaji wa pembejeo za Killimo hususan, mbolea za kupandia na kukuzia mimea pamoja na dawa (pesticides) aina ya ‘phosphorus, nitrogen, potassium na sulfur’.

Mbali na uzalishaji wa mbolea na dawa, Kampuni hiyo pia inazalisha vifaa vya kilimo vya plastiki ikiwa ni pamoja na khusambaza bidhaa katika nchini za Saudi Arabia, ukanda wa Mashariki ya Kati na duniani kote.

 

Wawekezaji hao waliwasili nchini Januari 28, 2022  wametembelea Mikoa ya Mtwara, Lindi Mtwara na Dodoma na kukutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Mikoa hiyo, wadau wa sekta binafsi na wakulima wa korosho kuzungumzia biashara na uwekezaji katika nyanja hizo. 

Wawekezaji hao wamemuhakikishia Mhe. Waziri Mulamula juu ya nia yao ya kuja kuwekeza Tanzania na kutaja maeneo ambayo ni kipaumbele chao kuwa ni madini, biashara, kilimo na mifugo

 

WAZIRI MULAMULA AKUTANA NA BALOZI WA MAREKANI NCHINI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amefanya mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Mhe. Donald Wright leo tarehe 2 Februari 2022 jijini Dodoma.
Pamoja na mambo mengine viongozi hao wamejadili juu ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani katika sekta za afya, uwekezaji, biashara na uhusiano wa kimataifa. 


Kushoto ni afisa kutoka Ubalozi wa Marekani, Bi. Kristin Mencer akifuatilia mazungumzo.

Kutoka kulia ni Katibu wa Waziri, Bw. Seif Kamtunda na Afisa Mambo ya Nje Bi. Talha Waziri wakifuatilia mazungumzo.

Mazungumzo yakiendelea.

Picha ya Pamoja.



 

WAZIRI MULAMULA AKUTANA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA ALFA CARE GROUP LIMITED

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kati) amekutana kwa mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Alfa Care Group Limited Bw. Dadkarim Mulla (wa kwanza kushoto) ambaye aliambatana na  Mbunge wa Arusha Mjini, Mhe. Mrisho Gambo (wa pili kushoto) walipomtembelea Wizarani tarehe 1 Februari 2022 jijini Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi, katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Edwin Rutageruka (mwenye tai) na Katibu wa Waziri, Bw. Seif Kamtunda.

Katika Mazungumzo yao wamejadili juu ya kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi kwa lengo ya kuyafikia malengo ya kitaifa kwa ufanisi.

Vilevile wamejadili namna ya kuongeza uwekezaji katika miradi ya maendeleo husasani sekta ya afya, miundombinu, teknolojia, utalii sambamba na kukuza ajira kwa watanzania.

Mazungumzo yakiendelea.

Picha ya pamoja
Mhe. Balozi Mulamula akimkabidhi Mhe. Gambo Calenda na Shajara za Wizara.

Mhe. Waziri akimkabidhi pia Bw. Mulla calenda ya Wizara

 

Saturday, January 29, 2022

BALOZI MULAMULA: MISINGI YA SERA YA MAMBO YA NJE HAIJABADILIKA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) amesema kuwa Misingi ya Sera ya Mambo ya Nje haijabadilika na iko imara, kusisitiza umoja na kutoshabiana kisiasa na upande wowote pamoja na kuwaunga mkono wale wote wanaokandamizwa.

Balozi Mulamula ameyasema hayo wakati alipokutana katika kikao kazi na watumishi wa Wizara ya leo Jijini Dodoma na kuwasihi watumishi kujenga mahusiano na kutekeleza kwa ufanisi Diplomasia ya Uchumi.

“Uchumi wa Tanzania unakuwa kutokana na juhudi zetu, na mtakumbuka kuwa Wizara ya Mambo ya Nje majukumu yake ni mtambuka kwani yanagusa kila sekta, na lengo la kikao hiki ilikuwa kukumbushana maagizo ya Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,”

“Nashukuru sana katika kukutana kwenye kikao na wafanyakazi binafsi nimehamasika na kuwa na ari mpya ya kuchapa kazi, na pia wafanyakazi wamehamasika mara baada ya kikao cha leo,” 

Katika awamu ya Sita, Serikali imefungua balozi mbili mpya na Konseli mbili na naamini kutokana na msisitizo wa Mhe. Rais Samia wa kutekeleza Diplomasia ya uchumi kwa vitendo tutaendelea kufungua balozi nyingine zaidi kadri tutakapokuwa tunapata uwezo…….kile tulichonacho tukitumie vizuri kwani milango imefunguka.

Mazingira ni mazuri na ndiyo maana tunaendelea kuhamasisha wawekezaji na wafanyabiashara kuja kuwekeza Tanzania.

Mwana Diplomasia namba moja Mhe. Rais Samia amekuwa mstari wa mbele kutusaidia katika hili na hata juzi alipokutana na mabalozi na wakuu wa mashirika ya kimataifa aliweza kuwaeleza kuwa Tanzania ipo pamoja na kwamba tunaenda wote katika kufanikisha malengo ya watanzania yaweze kuboreka Zaidi.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Nassor Mbarouk (Mb), Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine pamoja na Naibu katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma Rajab.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akifurahia jambo alipokuwa akizungumza na Watumishi wa Wizara jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Nassor Mbarouk (Mb), akizungumza na watumishi wa Wizara kwenye kikao kilichofanyika jijini Dodoma 

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akizungumza na watumishi wa Wizara kwenye kikao kilichofanyika jijini Dodoma 

Kutoka kushoto; Naibu katibu Mkuu Mhe. Balozi Fatma Rajab, Naibu Waziri Mhe. Balozi Nassor Mbarouk (Mb), Waziri Mhe. Balozi Liberata Mulamula, Mkurugenzi Msaidizi Menejimenti ya Rasilimali Watu Bw. Peter Bunyazu wakiwa kwenye kikao na Watumishi wa Wizara kilichofanyika jijini Dodoma
Sehemu ya Wakuu wa Idara na Vitengo (mstari wa mbele) wakifuatilia Kikao kilichokuwa kikiendelea baina Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula na watumishi wa Wizara.
Kikao kikiendelea

Kikao kikiendelea

Picha ya pamoja Meza Kuu na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Picha ya pamoja Meza Kuu na Wakuu wa Taasisi zilipo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Picha ya pamoja Meza Kuu na baadhi ya Watumishi wa Wizara

TANZANIA NA MAURITIUS ZASAINI MKATABA WA JUMLA

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Mauritius zimesaini Mkataba wa Jumla (General Framework Agreement - GFA)

Mkataba huo umesainiwa na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Mauritius mwenye makazi yake Harare Zimbabwe Mhe. Prof. Emmanuel Mbennah pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kikanda na Biashara za Kimataifa ya nchini Mauritius Mhe. Balozi Haymandoyal Dillum na kushuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kikanda na Biashara za Kimataifa Mhe. Alan Ganoo  

Mkataba huo pamoja na mambo mengine utaimarisha uhusiano wa kiuchumi, kisayansi na kiutamaduni. Mkataba huo pia utaanzisha Tume ya Pamoja ya Kudumu baina ya Nchi itakayokuwa ikifuatilia utekelezaji wa masuala mbalimbli kuhusu ushirikiano wa Tanzania na Mauritius. Hafla ya Uwekaji saini ilihudhuriwa pia na Viongozi wa Serikali na Taasisi kutoka Sekta Binafsi.

Aidha, kwa nyakati tofauti Balozi Mbennah alikutana kwa mazungumzo na Waziri mwenye dhamana na masuala ya Biashara Mhe. Soodesh Satkam Callichurn na Waziri mwenye dhamana na masuala ya Viwanda Mhe. Soomilduth Bholah. 

Mazungumzo na viongozi hao yalijikita katika utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi ili Tanzania na Mauritius ziweze kunufaika na fursa zilizopo katika Nchi hizo.

Balozi waTanzania nchini Mauritius Mhe. Prof. Emmanuel Mbennah pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kikanda na Biashara za Kimataifa ya nchini Mauritius Mhe. Balozi Haymandoyal Dillum wakisaini Mkataba wa Jumla (General Framework Agreement - GFA) na kushuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kikanda na Biashara za Kimataifa Mhe. Alan Ganoo

Balozi waTanzania nchini Mauritius Mhe. Prof. Emmanuel Mbennah katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kikanda na Biashara za Kimataifa ya nchini Mauritius Mhe. Balozi Haymandoyal Dillum na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kikanda na Biashara za Kimataifa Mhe. Alan Ganoo mara baada ya kusaini Mkataba wa Jumla (General Framework Agreement - GFA) 

Balozi waTanzania nchini Mauritius Mhe. Prof. Emmanuel Mbennah akibadilishana Mkataba wa Jumla na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kikanda na Biashara za Kimataifa ya nchini Mauritius Mhe. Balozi Haymandoyal Dillum  

Balozi wa Tanzania nchini Mauritius Prof. Emmanuel Mbennah akizungumza na Waziri Mkuu Mhe. Pravind Kumar Jugnauth, ambapo Mhe. Jugnauth ameipongeza Tanzania na Mauritius kuweka saini Mkataba wa Jumla ambao utaongeza wigo wa ushirikiano kwa nchi hizo mbili 


Thursday, January 27, 2022

MKUTANO WA 19 WA MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE WA AFRIKA NA NORDIC KUFANYIKA JUNI 2022 FINLAND


Na Mwandishi Wetu, Dar

Mkutano wa 19 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika na nchi za Nordic unatarajiwa kufanyika mwezi Juni 2022 nchini Finland.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Finland nchini Mhe. Riitta Swan leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Katika kuendeleza na kuimarisho ushirikiano wa nchi hizo mbili viongozi hao wamependekeza kufanikisha ziara ya Mhe. Waziri Mulamula nchini Finland pamoja na ushiriki wake katika mkutano wa 19 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Nordic utakaofanyika nchini Finland mwezi Juni 2022. 

Katika mazungumzo ya viongozi hao, Balozi Mulamula amemhakikishia Balozi Swan kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana kwa karibu na Finland katika kuhakikisha Mataifa hayo yanashirikiana kijamiii, kisiasa na kiuchumi.

"Finland amekuwa mdau Mkubwa wa Maendeleo hapa nchini kwetu hasa katika sekta ya fedha hususan katika masuala ya kodi, mazingira, tehama, uongozi pamoja na uwezeshaji wa wanawake........pia tumekubaliana kuendeleza ushirikiano wetu kwa Maendeleo endelevu," amesema Balozi Mulamula.

Katika tukio jingine, Waziri Mulamula amekutana kwa mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Stanbink Tanzania Bw. Kevin Wingfield
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula katika mazungumzo na Balozi wa Finland nchini Mhe. Riitta Swan leo katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiteta jambo na  Balozi wa Finland nchini Mhe. Riitta Swan pamoja na Afisa kutoka Ubalozi wa Finland nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Balozi wa Finland nchini Mhe. Riitta Swan, wengine ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Afrika Mashariki Balozi Swahiba Mndeme, Bi. Kisa Mwaseba Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje pamoja na Afisa kutoka Ubalozi wa Finland 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Stanbink Tanzania Bw. Kevin Wingfield yaliyofanyika katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam



TANZANIA NA INDIA KUONGEZA MAENEO YA USHIRIKIANO

Na Mwandishi wetu, Dar

Tanzania na India zimeahidi kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano katika kuhakikisha maendeleo endelevu kwa maslahi mapana ya pande zote mbili.

Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula wakati akihutubia sherehe za maadhimisho ya 73 ya Jamhuri ya India jana jioni Jijini Dar es Salaam.

Tanzania na India zimedhamiria kufanya kazi kwa karibu katika kutafuta njia bora ya kufungua fursa mpya na kuimarisha fursa mpya za biashara na uwekezaji zilizopo kati ya nchi hizo.

“Kuanza kwa safari za ndege za moja kwa moja kutoka Dar es Salaam hadi Mumbai kwa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) na kufunguliwa kwa soko la parachichi nchini India ni miongoni mwa hatua zilizochukuliwa ili kuimarisha na kukuza uhusiano wetu katika sekta za biashara na uwekuzaji pamoja na utalii kati ya India na Tanzania,” Amesema Balozi Mulamula. 

Pamoja na mambo mengine, Balozi Mulamula ameongeza kuwa Tanzania na India kwa sasa zimeanzisha ushirikiano katika usambazaji wa nishati, ujenzi wa miundombinu na Kilimo. Matarajio ya kuimarisha ushirikiano unaoendelea kati ya nchi hizi mbili ni mazuri na yanatia matumaini. 

“Uwekezaji wa India pamoja na idadi ya Wahindi wanaotembelea Tanzania kwa madhumuni ya kuwekeza katika sekta za madini, utalii, viwanda, kilimo, usindikaji wa mazao ya kilimo, nishati, usafirishaji, ujenzi, huduma za fedha na maendeleo ya rasilimali watu unaendelea kuongezeka kwa kasi,” amesema Balozi Mulamula.

Kwa upande wake, Balozi wa India nchini, Mhe. Binaya Srikanta Pradhan amesema kuwa Tanzania imekuwa na uhusiano mzuri na India ambapo uhusiano huo umekuwa ni chachu ya maendeleo kwa mataifa yote mawili na umepelekea kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano.

“Ushirikiano na mshikamano uliopo baaina ya mataifa yetu mawili umekuwa chachu ya maendeleo na lengo la ushirikiano wetu yetu ni kukuza uchumi wetu,” amesema Balozi Pradhan 

Aidha, Balozi Pradhan amebainisha kuwa Tanzania itaendelea kuwa ya kipekee kwa taifa la India kutokana na mshikamano ambao umepelekea mataifa haya kufanya biashara, uwekezaji, kujenga uwezo, ujenzi wa miundiombinu pamoja na maendeleo ya kiuchumi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akihutubia sherehe za maadhimisho ya 73 ya Jamhuri ya India jana jioni Jijini Dar es Salaam

Balozi wa India nchini, Mhe. Binaya Srikanta Pradhan akihutubia sherehe za maadhimisho ya 73 ya Jamhuri ya India jana jioni Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula. 

Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Kiongozi wa Mabalozi nchini ambaye pia ni Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini Mhe. Dkt. Ahmada El Badaoui Mohamed 

Sherehe za maadhimisho ya 73 ya Jamhuri ya India zikiendelea jana jioni Jijini Dar es Salaam

Balozi Mulamula na baadhi ya Mabalozi wakifuatilia sherehe za maadhimisho ya 73 ya Jamhuri ya India jana jioni Jijini Dar es Salaam

Sehemu ya Mabalozi wakifuatilia sherehe za maadhimisho ya 73 ya Jamhuri ya India jana jioni Jijini Dar es Salaam

Sherehe za maadhimisho ya 73 ya Jamhuri ya India jana jioni Jijini Dar es Salaam

Mabalozi na wageni waalikwa wakifuatilia sherehe za maadhimisho ya 73 ya Jamhuri ya India  

Sehemu ya Mabalozi wakifuatilia sherehe za maadhimisho ya 73 ya Jamhuri ya India