Sunday, May 25, 2014

Sherehe za Kuadhimisha Siku ya Afrika Zafana jijini Dar es Salaam

Brass band ikiongoza maandamano ya wanadipolomasia wa nchi za Afrika, watumishi wa Serikali ya Tanzania, wanafunzi na wageni wengine waalikwa kwenda Viwanja vya Karimjee kuadhimisha Siku ya Afrika.

Wanafunzi wakiwa wamebeba bendera mbalimbali za nchi za Afrika na ile ya Umoja wa Afrika wakiwa katika maandamano kuelekea Viwanja vya Karimjee.

Waheshimiwa Mabalozi wa Nchi za Afrika nchini Tanzania wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha Siku ya Afrika

Waheshimiwa Mabalozi wakiendelea na maandamano
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb) aliyevaa suti ya rangi ya kijivu akipokea maandamno katika Viwanja vya Karimjee 

Burudani ya ngoma katika Viwanja vya Karimjee kusherehekea Siku ya Afrika


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt Mahadhi Juma Maalim akiwahutubia watu waliohudhuria sherehe za Siku ya Afrika. Naibu Waziri alipongeza kaulimbiu ya maadhimisho hayo ambayo ni Kilimo na Usalama wa Chakula. Alisema usalama wa Chakula ni changamoto ambayo  lazima nchi za Afrika zichukuwe juhudi za pamoja kukabiliana nayo

Wanadiplomasia na wananchi wengine wakimsikiliza Naibu Waziri.

Balozi wa Kenya akichangia mada Kilimo na Usalama wa Chakula.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Dkt. Yamungu Kayandabila naye akitoa neno wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afrika

Balozi Sweden nchini Tanzania alipata fursa pia ya kuchangia mada katika maadhimisho hayo 


Picha ya pamoja ya Mabalozi na Mabalozi wastaafu mara baada ya sherehe za kuadhimisha Siku ya Afrika kukamilika

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim akihojiwa na wana habari


Picha ya pamoja kati ya Dkt. Maalim na Wanadipolomasia.



Picha na Reginald Philip


Saturday, May 24, 2014

Maadmisho ya Siku ya Afrika kufanyika Jumapili


Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Vicent Kibwana akiwa katika mkutano na waandishi wa Habari kuelezea maadhimisho ya Siku ya Afrika yatakayofanyika katika Viwanja vya Karimjee siku ya Jumapili tarehe 25 Mei, 2014. wengine katika picha ni Mhe. Meja Gen. Edzai Chimonyo (kushoto), Kaimu Mkuu wa Mabalozi wa nchi za Afrrika ambaye pia ni Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania na Balozi wa DRC nchini Tanzania, Mhe. Juma Mpango (kulia). kaulimbiu ya mwaka huu ya siku ya Afrika ni Kilimo na Usalama wa Chakula ambapo Waheshimiwa Mabalozi walisisitiza umuhimu wa nchi za Afrika kutoa kipaumbele katika sekta ya kilimo kwa kutengeneza sera nzuri za umiliki wa ardhi ili itumike kama dhamana katika taasisi za fedha. 

Balozi wa kenya nchini Tanzania akichangia mada kuhusu kaulimbiu ya Siku ya Afrika.

Waheshimiwa Mabalozi wa Nchi za Afrika nchini Tanzania na wana habari wakiendelea na mkutano.

Thursday, May 22, 2014

Rais Kikwete apokea Hati za Utambulisho za Balozi mpya wa Marekani nchini



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Hati za Utambulisho za Balozi mpya wa Marekani nchini, Mhe. Mark Childress IKULU, Dar es Salaam tarehe 22 Mei, 2014.
Mhe. Childress akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili IKULU.
Mhe. Rais Kikwete akimtambulisha kwa Balozi Childress  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule
Mhe. Rais Kikwete akimtambulisha kwa Balozi Childress  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Victoria Mwakasege
Balozi Childress akisalimiana na Afisa Dawati la Ulaya na Amerika  katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Redemptor Tibaigana.


Mhe. Rais Kikwete katika mazungumzo na Balozi Childress
Mhe. Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Balozi Childress
Picha ya Pamoja
Brass Band ikipiga wimbo wa Taifa la Marekani mara baada ya Balozi wa Marekani kuwasili IKULU kwa ajili ya kuwasilisha Hati zake za utambulisho kwa Rais.


Picha na Reginald Philip 















Monday, May 19, 2014

Mfanyakazi Hodari wa Wizara na Wafanyakazi Bora wapokea vyeti vyao

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bw. Dushhood Mndeme akijiandaa kutaja majina ya Wafanyakazi Bora wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwemo Mfanyakazi Hodari  wakati wa Kikao cha 8 cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Waliokaa ni Katibu Mkuu na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, Bw. John Haule (mwenye miwani), Naibu Katibu Mkuu, Balozi Rajabu Gamaha (wa kwanza kulia), Katibu wa Baraza la Wafanyakazi, Bw. Cosato Chumi (mwenye tai nyekundu) na Naibu Katibu wa Baraza la Wafanyakazi na Bi. Asya Hamdani.
Baadhi ya Wafanyakazi Bora wakiwa na nyuso za furaha.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Katibu Mkuu na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, Bw. Haule akimkabidhi Cheti Mfanyakazi Hodari wa Wizara Bw. Bujiku Sakila kutoka Idara ya Afrika.
Katibu Mkuu akimkabidhi Cheti Mfanyakazi Bora wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bw. Ally Kondo.
Katibu Mkuu akimkabidhi Cheti Mfanyakazi Bora wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar, Bi. Asya Hamdani.
Katibu Mkuu akimkabidhi Cheti Mfanyakazi Bora wa Idara ya Sera na Mipango,  Bw. Elly Chuma.
Katibu Mkuu akimkabidhi Cheti Mfanyakazi Bora wa Idara ya DIASPORA, Bw. Seif Kamtunda.
Katibu Mkuu akimkabidhi Cheti Mfanyakazi Bora wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani, Bw. Ibrahim Mamboya.
Katibu Mkuu akimkabidhi Cheti Mfanyakazi Bora wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bi. Gloria Mboya.
Katibu Mkuu akimkabidhi Cheti Mfanyakazi Bora wa Idara ya Mashariki ya Kati, Bw. Batholomeo Jungu.
Katibu Mkuu akimkabidhi Cheti Mfanyakazi Bora wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Rose Kitandula.
Katibu Mkuu akimkabidhi Cheti Mfanyakazi wa Kada ya Makatibu Muhtasi , Bi. Faith Masaka.
Katibu Mkuu akimkabidhi Cheti Mfanyakazi Bora wa Kada ya Wahudumu, Bi. Hadija Mwichande.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wakifuatilia tukio la utoaji vyeti kwa Wafanayakazi Bora wa Wizara
Bw. Iman Njalikai, Mwenyekiti wa TUGHE wa Wizara akizungumza mara baada ya utoaji vyeti kwa Wafanyakazi Bora wa Wizara.

Katibu Mkuu akibadilishana neno na baadhi ya Wajumbe mara baada ya kikao.

Friday, May 16, 2014

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Vietnam awasili nchini kwa ziara ya kikazi



Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Vietnam, Mhe. Nguyen Phuong Nga mara baada ya kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Mhe. Nguyen yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tano.




Mhe. Dkt. Maalim na Mhe. Nguyen wakizungumza huku Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Vo Thanh Nam (kushoto), Bw. Nathaniel Kaaya (kulia), Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Asia na Australasia na Bw.Emmanuel Ruangisa, Afisa Mambo ya Nje  wakifuatilia mazungumzo hayo.
Mhe. Nguyen akimkabidhi zawadi Dkt. Maalim mara baada ya mazungumzo yao.


Press Release

PRESS RELEASE
H.E President Jakaya Mrisho Kikwete of the United Republic of Tanzania has sent a congratulatory message to H.M. King Harald V of Norway on the occasion to celebrate 200 years Anniversary of the Norwegian Constitution on 17th May, 2014.

“Your Majesty King Harald V,
   The King of Norway,
   Oslo,
   NORWAY.

It is my pleasure on behalf of the people and the Government of the United Republic of Tanzania to extend to Your Majesty and through you to the people of Norway my heartfelt congratulations on the occasion to celebrate your Constitution Day.
The celebration of your Constitution Day offers me yet another opportunity to reiterate my personal commitment and that of my Government towards our shared aspirations in further strengthening the healthy relations that happily exist between our two countries and peoples. I am confident that the bonds of friendship and co-operation that our two countries enjoy will continue to grow in greater heights for our mutual benefit.
Please accept, Your Majesty, my best wishes for your continued good health and peace and prosperity for the people of Norway.

Issued by the Ministry of Foreign Affairs and International

Co-operation, Dar es Salaam



16th May 2014

Thursday, May 15, 2014

Balozi wa Tanzania nchini Urusi aapishwa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha  Lt. Gen. Wynjones Mattew Kisamba kuwa Balozi wa Tanzania nchini Urusi. Hafla hiyo fupi ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 15 Mei 2014.
Picha ya Pamoja
Mhe. Rais Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na Familia ya Balozi Kisamba

Balozi Kisamba akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika Bibi Victoria Mwakasege mara baada ya kuapishwa.

Picha na Reginald Philip


VACANCY ANNOUNCEMENT - ICGLR