Friday, September 19, 2014

Makamu wa Rais akutana kwa mazungumzo na Mwenyekiti wa Shirika la Nyumba la Dubai

Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na Mwenyekiti wa Shirika la Nyumba la  Dubai, Mhe. Ali Rashid Ahmed Lootah alipofika   Ofisi kwake kumsalimia na kufanya nae mazungumzo. Mhe. Lootah alimwelezea Makamu wa Rais dhumuni la ziara yake nchini Tanzania kuwa ni kuangalia nafasi ya uwekezaji katika Sekta ya Utalii, Ujenzi wa Nyumba na Makazi ya watu.
Mwenyekiti wa Shirika la Nyumba la  Dubai, Mhe. Lootah akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Ofisi ya Makamu wa Rais
Mhe. Dkt. Bilal akizungumza na Mhe. Lootah
Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Bilal akimsikiliza Mhe. Lootah alipokuwa akizungumza naye Ofisini kwake. Kulia kwa Mhe. Dkt. Bilal ni Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mmabo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya.

Mazungumzo yakiendelea.
Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Gharib Bilal akiagana na Mwenyekiti wa Shirika la Nyumba la Serikali ya Dubai  mara baada ya mazungumzo yao
Wakiwa katika picha ya pamoja.

Picha na Reginald Philip

Mwenyekiti wa Shirika la Nyumba la Dubai atembelea Wizara ya Maliasili na Utalii

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bi Maimuna Tarishi akisalimiana na Mwenyekiti wa Shirika la Nyumba la Serikali ya Dubai, Mhe. Ali Rashid Ahmed Lootah alipowasili Wizarani hapo na kufanya mazungumzo na baadhi ya viongozi katika Wizara hiyo, Mhe. Lootah katika mazungumzo yake aligusia suala zima la utunzaji vivutio vya utalii na uboreshaji wa miundombinu kwa lengo la kukuza sekta ya Utalii.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi akisalimiana na Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai Mhe. Omar Mjenga 
Bi. Maimuna Tarishi akielezea juu ya vivutio mbalimbali vilivyopo nchini na sifa za vivutio hivyo katika mazungumzo na Mhe. Lootah pamoja na ujumbe alioambata nao pia aliwahamasisha Dubai kuja kuwekeza Tanzania katika Sekta ya Utalii 
Mazungumzo yakiendelea
Kulia ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango katika Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw Iddi Mfunda  akichangia katika mazungumzo.
Balozi Mdogo,  Omar Mjenga akichangia jambo katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Wizara ya Maliasili na Utalii
Mhe. Lootah akichangia jambo wakati wa mazungumzo huku wajumbe wengine wakimsikiliza


Picha ya pamoja



Reginald Philip







Thursday, September 18, 2014

Mwenyekiti wa Shirika la Nyumba la Serikali ya Dubai atembelea mradi wa nyumba za gharama nafuu Kigamboni


Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba ncini Tanzania Mhe. Nehemia Mchechu (wakwanza kushoto), watatu kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Shirika la Nyumba la Serikali ya Dubai Mhe. Ali Rashid Ahmed Lootah, wapili kutoka kulia ni Bwa. Issack Peter, na wakwanza kutoka kulia ni Balozi Mdogo Mhe. Omar Mjenga, watembelea mradi wa nyumba za gharama nafuu za Kigamboni zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mapema leo asubuhi jijini Dar es salaam. 
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa Mhe. Nehemia Mchechu akimwelezea Mhe. Lootah ubora wa nyumba za mradi wa gharama nafuu (hazipo pichani) zilizojengwa katika eneo hilo la Kigamboni jijini Dar es Salaam
Baadhi ya Nyumba za mradi za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika eneo la Kigamboni.
Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai Mhe. Omar Mjenga akizungumza mara baada ya kumaliza kuangalia mradi wa nyumba hizo za gharama.

Picha na Reginald Philip

Mwenyekiti wa Shirika la Nyumba la Serikali ya Dubai akutana na Mkuu wa Majeshi

Mkuu wa Majeshi Nchini Tanzania Davids Mwamunyange akisalimiana na Mwenyekiti wa Shirika la Nyumba la Serikali ya Dubai (NAKHEEL) Mhe. Ali Rashid Ahmed Lootah alipo mtembelea Ofisini kwake jijini Dar es salaam.
Mh. Davis Mwamunyange akifanya mazungumzo na Mhe. Lootah mara tu baada ya kuwasili ofisini kwake, Mhe. Lootah katika ziara yake anaangalia fursa za uwekezaji katika uchumi, ujenzi wa nyumba na makaazi
Afisa Mambo ya Nje Bw. Hangi Mgaka akifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Mhe. Davis Mwamunyange na Mhe. Lootah (Hawapo pichani) na (wakwanza na wapili kutoka kulia) ni wajumbe walioambatana na Mhe. Lootah katika ziara
Viongozi mbalimbali wa Serikali wakisikiliza kwa makini mazungumzo hayo.
Mazungumzo yakiendelea.
Kulia ni Balozi Mdogo Omar Mjenga akizungumza jambo huku Mhe. Davis mwamunyange (wakwanza kushoto) na Mhe. Lootah (katikati) wakimsikiliza wakielekea nje mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo. 
Katikati ni Mkurugenzi wa Nyumba kutoka Dubai Mhe. Ali Rashid Ahmed lootah, nawa kwanzakushoto ni Mkuu wa Majeshi nchini Tanzania Mhe. Davis Mwamunyange na wakwanza kulia ni Balozi mdogo wa Tanzania, Dubai Mhe. Omar Mjenga wakiwa katika picha ya pamoja.
Picha ya Pamoja.
Picha na Reginald Philip.


Wednesday, September 17, 2014

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje akutana na Balozi wa Tanzania Paris, Ufaransa

Mhe. Bernard K. Membe, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa na Mhe. Begum Taj, Balozi wa Tanzania Paris Ufaransa mara baada ya kuwasili Paris, Ufaransa leo tarehe 17 Septemba 2014.
Waziri Membe akiwa kwenye mazungumzo na mwakilishi wa kampuni ya Airbus Bw. Pierre-Etienne Courage. Akiwa Mjini Paris, Waziri Membe pia alikutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Kampuni ya Renault. Pia alipokea taarifa ya maendeleo ya ununuzi wa jengo jipya la Ubalozi wa Tanzania nchini humo kutoka kwa Balozi Taj. Baada ya mikutano hiyo Mhe. Membe alielekea nchini Marekani kuhudhuria mikutano ya Umoja wa Mataifa. Wengine pichani ni maafisa wakuu wa Wizara ya Mambo ya Nje James Bwana na Olivia Maboko. Upande wa kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Ulaya na Marekani Mama Vicky Mwakasege na Balozi Begum Taji.



Mwenyekiti wa Shirika la Nyumba Serikali ya Dubai afanya ziara nchini

Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya akisalimiana na Mkurugenzi wa Nyumba kutoka Dubai Mhe. Ali Rashid Ahmed Lootah walipokutana kwa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Kampuni inayojishughulisha na masuala ya Nyumba ya OYO. Bw. Lootah yupo nchini kwa ziara ya siku mbili ya kuangalia fursa za uwekezaji katika Sekta ya Nyumba na Makazi.
Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai Bw. Omar Mjenga (katikati) akimtambulisha Mhe. Lootah (wa kwanza kulia) kwa Mkurugenzi wa IPP Media Bw. Reginald Mengi walipokutana katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam
Bw. Mjenga (wa kwanza kulia) akimtambulisha Bw. Harbert Marwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya OYO kwa Mhe. Ali Rashid Ahmed Lootah mara baada ya kuwasili nchini. 
Bw. Mjenga akiwa na mmoja wa wajumbe waliofutana na Mhe. Lootah wakati wa chakula cha jioni kwa wageni hao katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.


Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Adadi Rajabu (wa kwanza kulia) akisalimiana na Mkurugenzi wa Mashariki ya Kati Balozi Simba Yahya (wa kwanza kushoto) huku Mhe. Lootah akishuhudia  
Mwenyekiti wa Kampuni ya NAKHEEL Mh. Lootah akizungumza na viongozi mbali mbali kutoka Tanzania, kabla ya chakula cha jioni, Jijini Dar es Salaam
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya OYO  Bw. Hubert Marwa akimkaribisha Mhe. Lootah katika chakula cha jioni kilichoandaliwa na kampuni yake.
Balozi Simba akizungumza kwa niaba ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika hafla iliyoandaliwa na Kampuni ya OYO  katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam
Mwenyekiti wa kampuni ya NAKHEEL Mh. Lootah akizungumza katika hafla iliyoandaliwa na Kampuni ya OYO jijini Dar es salaam
 Meya wa Ilala,  Mh. Jerry Slaa (wa kwanza kushoto), akifuatiwa na  Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu, (watatu  kushoto) ni Mkurugenzi Masood Al Zarooni aliyeambatana na Mh. Lootah na wa kwanza kulia ni Bw. Harbert Marwa, wakimsikiliza kwa makini mh. Al Rashid Ahmed Lootah alipokuwa akizungumza.
Balozi Simba akimsikiliza Mh. Lootah wakati wanazungumza.


Wageni waalikwa wengine
Mazungumzo yakiendelea.
Balozi mdogo wa Tanzania nchini Dubai Balozi Mdogo. Omar Mjenga alitoa shukrani kwa Menyekiti wa Shirika la Nyumba la Serikali ya Dubai, Mhe. Lootah kwa kukubali mwaliko wake wakuja nchini Tanzania, pia aliwashukuru Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuwa mwenyeji wa ugeni huo na mwisho kwa wageni wote walio udhuria.


Balozi Simba Yahya (wa kwanza kulia),  Balozi Adadi Rajabu (katikati) na  Balozi mdogo wa Tanzania nchini Dubai Bw. Omar Mjenga.
Picha ya Pamoja


Picha na Reginald Philip

Tuesday, September 16, 2014

Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia akutana na Balozi wa China nchini

Mkurugenzi Idara ya Asia na Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki (kulia) akutana na Balozi wa China nchini Mhe. Lu Youqing,  kuhusu maandalizi ya maadhimisho ya miaka 50 ya ushirikiano kati ya Tanzania na China yatakayofanyika nchini China mwezi Oktoba 2014.  
Maafisa kutoka Hazina na Mambo ya Nje wakifuatilia mazungumzo hayo kwa makini. 
Maafisa walioambatana na Balozi wa China wakinukuu mazungumzo kati ya Balozi Mbelwa na Balozi Lu Youqing (hawapo pichani).
Kikao kikiendelea.
Picha na Reginald Philip