Wednesday, September 17, 2014

Mwenyekiti wa Shirika la Nyumba Serikali ya Dubai afanya ziara nchini

Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya akisalimiana na Mkurugenzi wa Nyumba kutoka Dubai Mhe. Ali Rashid Ahmed Lootah walipokutana kwa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Kampuni inayojishughulisha na masuala ya Nyumba ya OYO. Bw. Lootah yupo nchini kwa ziara ya siku mbili ya kuangalia fursa za uwekezaji katika Sekta ya Nyumba na Makazi.
Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai Bw. Omar Mjenga (katikati) akimtambulisha Mhe. Lootah (wa kwanza kulia) kwa Mkurugenzi wa IPP Media Bw. Reginald Mengi walipokutana katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam
Bw. Mjenga (wa kwanza kulia) akimtambulisha Bw. Harbert Marwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya OYO kwa Mhe. Ali Rashid Ahmed Lootah mara baada ya kuwasili nchini. 
Bw. Mjenga akiwa na mmoja wa wajumbe waliofutana na Mhe. Lootah wakati wa chakula cha jioni kwa wageni hao katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.


Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Adadi Rajabu (wa kwanza kulia) akisalimiana na Mkurugenzi wa Mashariki ya Kati Balozi Simba Yahya (wa kwanza kushoto) huku Mhe. Lootah akishuhudia  
Mwenyekiti wa Kampuni ya NAKHEEL Mh. Lootah akizungumza na viongozi mbali mbali kutoka Tanzania, kabla ya chakula cha jioni, Jijini Dar es Salaam
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya OYO  Bw. Hubert Marwa akimkaribisha Mhe. Lootah katika chakula cha jioni kilichoandaliwa na kampuni yake.
Balozi Simba akizungumza kwa niaba ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika hafla iliyoandaliwa na Kampuni ya OYO  katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam
Mwenyekiti wa kampuni ya NAKHEEL Mh. Lootah akizungumza katika hafla iliyoandaliwa na Kampuni ya OYO jijini Dar es salaam
 Meya wa Ilala,  Mh. Jerry Slaa (wa kwanza kushoto), akifuatiwa na  Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu, (watatu  kushoto) ni Mkurugenzi Masood Al Zarooni aliyeambatana na Mh. Lootah na wa kwanza kulia ni Bw. Harbert Marwa, wakimsikiliza kwa makini mh. Al Rashid Ahmed Lootah alipokuwa akizungumza.
Balozi Simba akimsikiliza Mh. Lootah wakati wanazungumza.


Wageni waalikwa wengine
Mazungumzo yakiendelea.
Balozi mdogo wa Tanzania nchini Dubai Balozi Mdogo. Omar Mjenga alitoa shukrani kwa Menyekiti wa Shirika la Nyumba la Serikali ya Dubai, Mhe. Lootah kwa kukubali mwaliko wake wakuja nchini Tanzania, pia aliwashukuru Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuwa mwenyeji wa ugeni huo na mwisho kwa wageni wote walio udhuria.


Balozi Simba Yahya (wa kwanza kulia),  Balozi Adadi Rajabu (katikati) na  Balozi mdogo wa Tanzania nchini Dubai Bw. Omar Mjenga.
Picha ya Pamoja


Picha na Reginald Philip

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.