Tuesday, September 2, 2014

Balozi Mdogo wa Tanzania- Dubai akutana na uongozi wa juu wa Hospital ya Iran ya Dubai


Mhe. Omar Mjenga akiwa katika picha ya pamoja na mwenyeji wake Dk. Asghar Fashad.
Mhe. Omar Mjenga akizungumza na Uongozi wa Juu wa Hospitali ya Iran, akiwemo Mkurugenzi Mkuu Dk. Asghar Fashad.

Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Iran Dkt. Asghar Fashad akizungumza.

===========================================

Mhe. Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa Tanzania- Dubai, leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Iran ya Dubai, Dr. Asghar Fashad. Katika mazungumzo, Mhe. Mjenga alimuomba Dr asghar kuangalia uwezekano wa kuwa na makubaliano kati ya hospitali yake na Ubalozi Mdogo kwa ajili ya kutoa huduma za afya kwa Watanzania kwa gharama nafuu ukilinganisha na gharama zake za sasa. 

Baada ya mazungumzo na mashauriano ya muda wa saa moja, Uongozi wa Juu wa Hospitali, ulikubali ombi la Mhe. Mjenga la kupunguza gharama za matibabu kwa Watanzania kwa asilimia 40 (40%). Mwanzo, Uongozi ulipendekeza asilimia 20, ambayo Mhe. Mjenga aliwaeleza kuwa bado ilikuwa ni punguzo dogo na bado ingekuwa ni mzigo mkubwa kwa Watanzania. Hatmaye, ndio maafikiano hayo yakafikiwa ya asilimia 40.

Mpango wa huu utajumuisha Watanzania wote waishiyo UAE na wale wanaoishi nje ya UAE ikiwa ni pamoja na wale wanaoishi Tanzania. Hospital ya Irani ni moja ya hospitali zenye huduma za hali ya juu kwa hapa Dubai na UAE kwa ujumla.

Uongozi wa Hospitali umekubali kuanza kutoa Vitambulisho Maalum kwa ajili ya Watanzania wote kuanzia Jumapili tarehe 1 Septemba. Mkataba wa Makubaliano haya utatiwa saini Jumatatu tarehe 2 Septemba.

Aidha, Mhe. Mjenga, amemuomba Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hii, kuangalia uwezekano wa kujenga Hospitali kubwa yenye hadhi kama hii, nchini Tanzania. Kimsingi, Mkurugenzi Mkuu amekubali ombi hili, na ameahidi kumuomba Rais wa Hospitali kufanya ziara nchini Tanzania mwezi ujao ili kuona na uongozi husika na kuanza mazungumzo ya kuanzisha Hospitali kama hiyo. Ameeleza kuwa Tanzania na Iran na nchi marafiki wa siku nyingi, na hivyo Iran inafarijika sana kuwa karibu na Tanzania kimahusiano.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.