Wednesday, September 10, 2014

Mhe. Rais Kikwete apokea Hati za Utambulisho za Balozi mpya wa Norway nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Hati za Utambulisho za Balozi wa Norway  nchini  Mhe. Hanne Maria Kaarstad. Hafla hiyo fupi ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 09 Septemba, 2014.
Balozi Kaarstad akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) mara baada ya kuwasilisha Hati zake za utambulisho kwa Mhe. Rais.
Balozi Kaarstad akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine.
Mhe. Rais Kikwete akizungumza na Balozi Kaarstaad mara baada ya kupokea Hati za Utambulisho za Balozi huyo, Ikulu.
Mhe. Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Balozi Kaarstaad.
Mhe. Rais Kikwete pamoja na Balozi Kaarstaad katika picha ya pamoja na Maafisa kutoka Ubalozi wa Norway.
Balozi Kaarstad akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya  kuwasilisha hati zake za utambulisho kwa Mhe. Rais.
Balozi Kaarstad akisikiliza Wimbo wa Taifa lake mara baada ya kuwasili Ikulu. Wengine katika picha ni Balozi Mohammed Maharage Juma (kulia), Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki na Mnikulu, Bw. Shaaban Gurumo.
Maafisa kutoka Ubalozi wa Norway wakisikiliza wimbo wa taifa lao.
Bendi ya Polisi ikipiga wimbo wa taifa la Norway kwa heshima ya Balozi wake (hayupo pichani). 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.