Thursday, September 11, 2014

Balozi Mushy akutana na Wawakilishi wa Nchi za G4 nchini Tanzania

Balozi Celestine Mushy, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiongea jambo wakati alipokutana na wawakilishi wa nchi za G4 hapa nchini ambazo ni India, Brazil, Ujerumani na Japan. Mwingine katika picha ni Bibi Ramla Khamis, Afisa katika Wizara ya Mambo ya Nje. Balozi Mushy na wawakilishi hao walijadili masuala ya mabadiliko katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambapo alisisitiza msimamo wa bara la Afrika wa kupatiwa nafasi mbili za ujumbe wa kudumu zenye kura ya turufu katika Baraza hilo pamoja na nafasi tano za ujumbe usio wa kudumu.

Wawakilishi wa nchi za G4 nchini wakimsikiliza kwa makini Balozi Mushy hayupo pichani. kutoka kulia ni Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Debnath Shaw; Naibu Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. John Reyels; Afisa wa Ubalozi wa Ujerumani nchini Tanzania; Naibu Balozi wa Brazil nchini Tanzania, Mhe. Pedro Martins; Afisa wa Ubalozi wa Japan nchini Tanzania, Bibi Noriko Tanaka.  

Mazungumzo yakiendelea baina ya Balozi Mushy na Wawakilishi wa nchi za G4 nchini Tanzania

Picha ya Pamoja baina ya Balozi Mushy (watatu kutoka kulia) na Wawakilishi wa Nchi za G4.


Picha na Anthony Guninita



No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.