Thursday, August 13, 2015

Waziri Membe afungua Kongamano la Pili la Diaspora nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaina Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Pili la Watanzania waishio nje (Diaspora) ambalo limebeba kaulimbiu isemayo "Tanzanian Diaspora and SMEs in Partnership for Development and Job-Creation".  Kongamno hilo la siku mbili limefanyika katika Hoteli ya Serena  Jijini Dar es Salaam 


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (Kulia) pamoja na Balozi wa Umoja wa Ulaya Mhe. Filiberto Sebregondi (kushoto) wakimsikiliza Waziri Bernard Membe (hayupo pichani).
Juu na Chini ni Waziri Membe akiendelea kuzungumza na Wanadiaspora na wadau mbalimbali walioudhuria Kongamano hilo 
Sehemu ya washiriki wa kongamano hilo wakiwemo Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine (wa kwanza kushoto), akifuatiwa na Mkurugenzi Idara ya Asia na Australasia pamoja na washiriki wengine wakifuatilia hotuba kutoka kwa  Mhe. Membe (hayupo pichani)
Sehemu nyingine ya washiriki wa Kongamano wakisikiliza kwa makini hotuba iliyotolewa na Mhe. Membe (hayupo pichani).
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Bw. Assah Mwambene (kulia) kwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Elibariki Maleko (wa kwanza kushoto), Kaimu Mkurugenzi Idara ya Afrika, Bi. Zuhura Bundala (wa pili kutoka kushoto), Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Itifaki, Bw. James Bwana (wa tatu kutoka kushoto) nao wakimsikiliza Waziri Membe alipo kuwa akitoa Hotuba kwa niaba ya Rais  Jakaya Kikwete.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula naye akizungumza katika Kongamano hilo.
Juu na chini ni washiriki katika Kongamano hilo wakimsikiliza Mhe. Balozi Mulamula (hayupo pichani). 
Mke wa wa Waziri Membe, Bi. Dorcas Membe (katikati) kwa pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Uswisi, Mhe. Modest Mero (kulia) nao wakifuatilia ufunguzi wa Kongamano la Diaspora. 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora, Bi. Rosemary Jairo naye akizungumza katika kongamano la Diaspora wakati wa ufunguzi wa Diaspora. 
Msanii wa kizazi kipya Bw. Peter Msechu akiwaongoza mgeni rasmi, Mhe. Membe, meza kuu na washiriki wengine wa kongamano kuimba  Wimbo wa Taifa kabla ya ufunguzi rasmi wa Kongamano.
Maafisa Mambo ya Nje nao wakiimba wimbo wa Taifa.
Sehemu ya washiriki katika Kongamano la Diaspora  nao wakiimba wimbo wa taifa 
Waziri Membe na Bi Dorcas Membe wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la Diaspora mara baada ya shughuli ya ufunguzi kukamilika.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Benard Membe akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula (wa kwanza kulia), Balozi wa Umoja wa Ulaya, Mhe. Sebregond (wa pili kutoka kulia), Mwakilishi wa Baraza la wa Wakilishi Zanzibar, Ali Mzee Ali (wapili kutoka kushoto), Kaimu Mkurugenzi Idara ya Diaspora, Bi Rosemary Jairo (wa kwanza kushoto) na Mwakilishi wa (DICOTA) Bw. Abdul Majid. 
Mhe. Membe pamoja na wageni katika mezaa kuu wakiwa katika picha ya pamoja na Watanzania waishio Ughaibuni

Picha na Reginald Philip


============================================

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete ametoa rai kwa Watanzania wanaoishi ughaibuni (Diaspora) kushirikiana kwa karibu  na Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo (SME’s) ili kuchangia maendeleo ya nchi na hatimaye kuiwezesha Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Katika hotuba yake ya ufunguzi wa Kongamano la Pili la Watanzania waishio ughaibuni (Diaspora) lililofanyika leo kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam , iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe, Rais Kikwete amesema kuwa Serikali yake imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara (SME’s) inashamiri ili kuchangia maendeleo ya nchi na kukuza ajira kwa wananchi wa Tanzania wakiwemo vijana na kuwahimiza Diaspora kushirikiana na sekta hiyo ili kuleta tija.

Rais Kikwete amesema kuwa, lengo la kongamano hili la pili  ni kuwahimiza Watanzania waishio ughaibuni kuuangana na  Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo (SME’s) kwa ajili ya kuleta maendeleo nchini na kutengeza ajira.

“Napongeza kaulimbiu ya kongamano hili la mwaka huu ambayo inahimiza SME’s kufanya kazi kwa pamoja na Wanadiaspora kwa ajili ya kuiletea nchi yetu maendeleo na pia kutengeneza ajira kwa wananchi”, alisema Rais Kikwete.


Aidha, alisema kuwa Kongamano hili ni moja ya jitihada zinazofanywa na Serikali yake katika kuhakikisha Watanzania wanaoishi ughaibuni (Diaspora) wanaunganishwa na kunufaika na sekta  mbalimbali za hapa nchini ikiwemo hiyo ya SME’s  ambayo inachangia asilimia 35 ya pato la taifa.

Mhe. Rais, aliongeza kuwa dhamira ya  serikali  ni kuweka mazingira mazuri Diaspora ili waweze kuja kuwekeza nyumbani na kwamba jitihada hizo ni pamoja na kuifanyia maboresho Sekta ya SME’s kupitia Mpango wa Kurasimisha Rasilimali za Wanyonge Tanzania (MKURABITA)  ili  wafanyabiashara wadogo wapate uwezo wa kufanya biashara rasmi ikiwemo kuwawezesha kufanya biashara nje kwa kushirikiana na  Watanzania wanaoishi ughaibuni  (Diaspora) ambao watasaidia upatikanaji wa  masoko kwa bidhaa  na kuhamasisha wawekezaji wa nje kuja nchini.

Vilevile aliwahimiza Diaspora kuendelea kutoa mchango wao kwa maendeleo ya nchi ikiwemo ujuzi, elimu, mitaji, huduma na kujenga nyumbani kupitia miradi mbalimbali inayotolewa na mashirika ya nyumba likiwemo Shirika la nyumba la Taifa (NHC).

Kwa upande wake, Mhe. Waziri Membe alisema kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ilianzisha Idara ya Diaspora mwaka 2009 kwa lengo la kuwatambua Watanzania wanaoishi ughaibuni na kuwahamasisha kuchangia maendeleo ya nchi kwa kutumia mitaji, ujuzi na elimu wanayoipata wakiwa nje ya nchi.  Aidha, akitoa maoni yake kuhusu suala la uraia wa nchi mbili (Dual Citizenship) Mhe. Membe alisema kuwa bado ana imani kuwa suala hilo litaendelea kujadiliwa ili kuwawezesha Wanadiaspora kuleta  maendeleo ya kweli  nchini.

Awali, akimkaribisha Waziri Membe kuzungumza, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula amesema kuwa dhumuni la kongamano la pili la Diaspora  ambalo limeratibiwa na Wizara kwa  kushirikiana na Ofisi ya Rais-Zanzibar na Ofisi ya Waziri Mkuu ni kuhimiza na kuendelea kutambua mchango wao katika ukuaji wa uchumi nchini na kuwaunganisha Diaspora na Sekta ya Viwanda Vidogo na biashara Ndogo (SME’s).

Kongamano hilo la  siku mbili, linawahusisha Watanzania wanaoishi ughaibuni, wadau mbalimbali kutoka sekta za umma na binafsi na wawakilishi kutoka mikoani.

-Mwisho-



Wednesday, August 12, 2015

Simple Hope Foundation wamtembelea Balozi Mulamula Wizara ya Mambo ya Nje

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Bi. Pamela A. Schwalbach, mmoja wa waanzilishi wa Shirika la (Simple Hope East Africa) linalo fanya kazi za kijamii na  wakina mama wa Kabila la Hadzabe, Mkoani Manyara.  
Bi. Pamela (katikati) na Bi Karen J. Puhl (Kushoto)  wakiwa kwenye mazungumzo na Katibu Mkuu Mambo ya Nje ambapo alipata wasaa wa kupokea taarifa ya kazi za shirika hilo lisilo la kiserikali la Marekani, Jimbo la Wisconsin. 
Katibu Mkuu Balozi Liberata Mulamula (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Bi. Pamela A. Schwalbach (wa pili kushoto), Bi. Karen J. Puhl (wa pili kulia), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Bi. Mindi Kasiga (wa kwanza kulia) na Afisa Mambo ya Nje Bi. Felista Rugambwa (wa kwanza kushoto)



Picha na Reginald Philip

Tuesday, August 11, 2015

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


UTEUZI NA UHAMISHO WA MABALOZI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Joseph B. Masikitiko kuwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Kabla ya uteuzi huo Ndugu Masikitiko alikuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo (TBS).

Aidha, Rais Kikwete amefanya uteuzi wa Balozi mmoja na kuwabadilishia vituo vya kazi Mabalozi wawili kama ifuatavyo:

(i)   Lt. Gen. Charles L. Makakala, ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe. Kabla ya uteuzi huo Lt. Gen. Makakala alikuwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (National Defence College).
(ii) Balozi Wilson Masilingi aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi amehamishwa kwenda kuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Liberata Mulamula aliyeteuliwa hivi karibuni kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa. Atakuwa pia anaiwakilisha Tanzania nchini Mexico
(iii)                Balozi Irene Kasyanju aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi kushika nafasi inayoachwa wazi na Balozi Wilson Masilingi.
Taarifa iliyotolewa leo, Jumanne, Agosti 11, 2015 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue mjini Dar es Salaam inasema kuwa Uteuzi na uhamisho huu unaanzia tarehe 07 Agosti, 2015.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.


11 Agosti, 2015

Monday, August 10, 2015

Katibu Mkuu amuaga rasmi Balozi wa Finland aliyemaliza muda wa kazi nchini

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Libarata Mulamula akizungumza mbele ya Mabalozi na Wageni waalikwa wakati wa hafla fupi ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Wizara kwa ajili ya kumuaga rasmi Balozi wa Finland aliyemaliza muda wa kazi nchini, Mhe. Sinikka Antila. Katika hotuba yake Balozi Mulamula alimshukuru Balozi Antila kwa mchango wake wa  kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Finland. Hafla hiyo ilifanyika kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Balozi Mulamula akiendelea kuzungumza.
Balozi Antila (Wa kwanza Kulia), Balozi wa Demokrasia ya Kongo nchini Balozi Juma Mpango (Wa pili Kutoka kulia), Balozi wa Uingereza Mhe. Dianna Melrose (Wa tatu kutoka kulia), Balozi wa Rwanda nchini Mhe. Eugene Segore Kayihura (Wa tatu kutoka kushoto), Balozi wa Ujerumani nchini Mhe. Egon Kochanke (Wa pili kutoka kulia) na Balozi wa Canada nchini Mhe. Alexandre Leveque wakimsikiliza Balozi Mulamula hayupo pichani 
Sehemu ya Wageni walioudhuria hafla hiyo wakimsikiliza Balozi Mulamula (hayupo pichani).
Balozi Antila akizungumza wakati wa hafla hiyo ambapo aliishukuru Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Serikali kwa ujumla kwa ushirikiano alioupata katika kipindi chote alichokuwepo nchini.
Katibu Mkuu Mhe. Balozi Mulamula (Wa kwanza kushoto) kwa pamoja na, Mkurugenzi Idara ya Amerika na Ulaya Balozi Joseph Sokoine (Wa pili kutoka kushoto), Balozi wa Umoja wa Ulaya Mhe. Filiberto Sebregond (Wa pili kutoka kulia) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Bwa. Alvaro Rodriguez  wakimsikiliza Balozi Antila (hayupo pichani).
Balozi Antila akiendelea Kuzungumza
Balozi Mulamula na Balozi Antila wakitakiana afya njema kwa kugonganisha Glasi
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Mambo ya Nje Bi. Mindi Kasiga ambaye alikuwa mshereheshaji wakati wa hafla hiyo akizungumza.
Balozi Mulamula akimkabidhi zawadi ya picha ya Mlango wa Zenji Balozi Antila.
Wageni waliohudhuria Hafla hiyo wakifurahia kwa kupiga makofi wakati Balozi Mulamula akimkabidhi Balozi Antila zawadi ya picha (Hawapo pichani).  
Balozi Mulamula (Wa pili kulia), Balozi Mpango (Wa kwanza kushoto), Balozi Antila (Wa pili kutoka kushoto), na Balozi Sokoine wakiwa katika picha ya pamoja.
Balozi Mulamula na Balozi Antila wakiwa katika Picha ya Pamoja na wageni walioudhuria hafla hiyo.

Picha na Reginald Philip

Mkurugenzi wa Ushirikano wa Kimataifa awashauri vijana kufanya kazi na Mashirika ya Kimataifa

Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akitoa mada katika  Kongamano la Vijana. Wakati wa kongamano hilo Balozi Mushy amewashauri vijana kufanya kazi na Taasisi za Umoja wa Mataifa ili kujipatia uzoefu wa kujielezea ikiwa ni pamoja na kujiamini. Kongamano hilo lilifanyika katika Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es Salaam
Mwakilishi Mkazi wa UNFPA Tanzania Dkt. Natalia Kanem (Wa pili kutoka kulia), Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Vijana Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi (wa kwanza kulia) wakimsikiliza Balozi Mushy (Hayupo pichani) wakati akiwasilisha Mada.
Juu na Chini ni picha ya Vijana waliohudhuria Kongamano hilo wakimsikiliza Balozi Mushy (hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha mada.
Balozi Mushy akimwelezea jambo Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi katika Kongamano la Vijana
Balozi Mushy (Katikati mwenye suti nyeusi) alipokuwa akiwasilisha mada ambapo pia alitaka kujua ni vijana wangapi wamejiandikisha kupiga kura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba 2015, huku ikionekana idadi kubwa ya vijana waliohudhuria Kongamano hilo wamejiandikisha

Picha na Reginald Philip