Friday, August 14, 2015

Kongamano la Diaspora na Wajasiriamali likiendelea kwa siku ya pili jijini Dar es Salaam



Chukwu-Emeka Chikezie akiongoza moja ya mdahalo katika kongamano la Diaspora, Balozi wa Marekani nchini Mhe. Mark Childress kwa pamoja na Bw. Ali Mufuruki, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maafisa Watendaji Wakuu nchini, Bw. Richard Miles, Mwakilishi wa Umoja wa Wafanyabiashara wa Marekani nchini na Dkt. Silencer Mapuranga, Mchumi kutoka ITC.
Balozi wa Marekani nchini, mhe. Childress akichangia mada kuhusu mabadiliko ya kiuchumi Tanzania wakati wa Kongamano la Diaspora.
Bw. Miles nae akichangia wakati wa mjadala kuhusu mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania na namna ya kuwashirikisha wafanyabiashara wadogo na wakati katika maendeleo ya nchi.
Balozi Mulamula akizungumza wakati wa mjadala huo 
Balozi wa China nchini, Mhe. Lu Youqing akiwasilisha mada kuhusu Mapinduzi ya Viwanda nchini na wajibu wa Diaspora katika ukuaji wa SME's
Balozi Lu akiwasilisha mada yake
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula kwa pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Uswisi, Mhe. Modest Mero wakimsikiliza Balozi wa China nchini (hayupo pichani) wakati akiwasilisha mada
Washiriki wakifuatilia mada kutoka kwa Balozi wa China
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Mhe. Hemed Mgaza akiwa na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Diplomasia, Dkt. Bernard Achiula wakisikiliza kwa makini uwasilishwaji wa mada wakati wa kongamano la Pili la Diaspora.
Mada zikitolewa
Maafisa Mambo ya Nje wakijadili jambo 
Timu ya Waandishi wa kumbukumbu za mkutano kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakinukuu taarifa mbalimbali wakati wa Kongamano la Diaspora ili kuweka kumbukumbu za tukio hilo sawasawa
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Rosemary Jairo akizungumza wakati wa kongamano hilo
Mada zikiendelea kutolewa wakati wa kongamano hilo 
Washiriki wa kongamano 


Picha na Reginald Philip

Rais Kikwete ashiriki hafla ya chakula cha jioni kuhitimisha Kongamano la Pili la Diaspora



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
 Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Watanzania waishio Ughaibuni (Diaspora) hawapo pichani wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa ajili ya kuhitimisha Kongamano la Pili la Diaspora katika Hotel ya Serena Jijini Dar es Salaam
Mhe. Rais akisisitizia jambo kwa Watanzania waishio Nje 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora, Bi. Rosemary Jairo akimsikiliza Rais Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na Diaspora wakati wa hafla ya chakula cha jioni.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Balozi Irene Kasyanju (kulia) akiwa na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Afrika Bi. Zuhura Bundala (kushoto).
Sehemu ya wageni waliohudhuria hafla hilo wakimsikiliza Mhe. Rais Kikwete (hayupo pichani).
 
Rais Kikwete akiendelea na hotuba yake
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula naye akizungumza wakati wa hafla hiyo ya chakula cha jioni.
Balozi Mulamula akiendelea kuzungumza

Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.
Wana Diaspora kutoka nchi mbalimbali na Tanzania  wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa maalum kwa ajili ya kufunga Kongamano la pili la Diaspora. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mirisho Kikwete (kushoto) akimkabidhi cheti cha kutambua mchango wa NHC kwenye masuala ya Diaspora Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa Bwa. Nehemia Mchechu (Kulia)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mirisho Kikwete (kushoto) akimkabidhi cheti Mkurugenzi Mtendaji kutoka Kampuni ya Huawei nchini Bw. Sung

Balozi wa China nchini, Mhe. Lu akizungumza na mdau walipo hudhuria hafla ya chakula cha jioni kwa ajili ya kuhitimisha Kongamano la Pili la Diaspora nchini 
Afisa Mambo ya Nje, Bw. Mugendi Zoka akibadilishana mawazo na Watanzania waishio Nje waliohudhuria hafla ya chakula cha jioni
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akizungumza  na Mkurugenzi Kitengo cha Sheria, Balozi Irene Kasyanju (kulia), na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Afrika Bi. Zuhura Bundala

Mkurugenzi Msaidizi, Bw. James Bwana (kulia),  akibadilishana Mawazo na Afisa Mambo ya Nje Bw. Hassan Mwamweta (kushoto).
Rais Kikwete (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora, Bi. Rosemary Jairo (kushoto) na kulia ni Mtoto wa Bi. Rosemary Jairo 
Rais Kikwete (mwenye tai nyekundu) akiwa katika Picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na Watanzania waishio Nje.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Kamati iliyoandaa Kongamano hilo.













Picha na Reginald Philip.

Waziri Membe atembelea mabanda ya maonesho wakati wa Kongamano la Diaspora

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (kushoto) akipata maelezo kuhusu na matumizi ya Gesi Asilia, Miradi na manufaa yake kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Bw. James Mataragio (kulia) alipotembelea banda la shirika hilo wakati wa Kongamano la Watanzania waishio Ughaibuni (Diaspora) 


Waziri Membe akionyeshwa na Bw. Mataragio eneo bomba la gesi asilia lilipopita kwenye Mchoro wa Ramani ya Tanzania uliopo mbele yao.
Waziri Wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa katika picha ya pamoja na Bibi Dorcas Membe (kushoto), Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Bw. James Mataragio (Kulia), Kaimu Mkurugenzi Idara ya Diaspora, Bi Rosemary Jairo (wa pili kutoka kulia) na Watumishi kutoka katika shirika hilo.
Waziri Membe na Mkewe Mama Dorcas wakipata maelezo juu ya matumizi ya radio calls kutoka kwa  Bw. Sunji wa Kampuni ya Huawei nchini alipotembelea banda la Kampuni ya hiyo wakati wa Kongamano la Diaspora.
Waziri Membe (wa kwanza kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) nchini, Bi. Matilda Nyallu. Kushoto kwa Mhe. Membe ni Balozi Mulamula, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Balozi Mulamula (katikati) akielezea jambo kwa Waziri Membe (kushoto).
Waziri Membe akisalimiana na mmoja wa  Washiriki wa Kongamano la Pili la Diaspora,Bw. William Malecela. Kulia ni Balozi Mulamula na katikati ni Bi. Suzani Mzee kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Bi. Rosemary Jairo (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Itifaki, Bw. James Bwana (wa pili kutoka kushoto)na Maafisa Mambo ya Nje Bw. Batholomeo Jungu ( kulia) na Bw. Amosi Tengu ( kushoto). 

Picha na Reginald Philip

Thursday, August 13, 2015

Waziri Membe afungua Kongamano la Pili la Diaspora nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaina Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Pili la Watanzania waishio nje (Diaspora) ambalo limebeba kaulimbiu isemayo "Tanzanian Diaspora and SMEs in Partnership for Development and Job-Creation".  Kongamno hilo la siku mbili limefanyika katika Hoteli ya Serena  Jijini Dar es Salaam 


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (Kulia) pamoja na Balozi wa Umoja wa Ulaya Mhe. Filiberto Sebregondi (kushoto) wakimsikiliza Waziri Bernard Membe (hayupo pichani).
Juu na Chini ni Waziri Membe akiendelea kuzungumza na Wanadiaspora na wadau mbalimbali walioudhuria Kongamano hilo 
Sehemu ya washiriki wa kongamano hilo wakiwemo Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine (wa kwanza kushoto), akifuatiwa na Mkurugenzi Idara ya Asia na Australasia pamoja na washiriki wengine wakifuatilia hotuba kutoka kwa  Mhe. Membe (hayupo pichani)
Sehemu nyingine ya washiriki wa Kongamano wakisikiliza kwa makini hotuba iliyotolewa na Mhe. Membe (hayupo pichani).
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Bw. Assah Mwambene (kulia) kwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Elibariki Maleko (wa kwanza kushoto), Kaimu Mkurugenzi Idara ya Afrika, Bi. Zuhura Bundala (wa pili kutoka kushoto), Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Itifaki, Bw. James Bwana (wa tatu kutoka kushoto) nao wakimsikiliza Waziri Membe alipo kuwa akitoa Hotuba kwa niaba ya Rais  Jakaya Kikwete.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula naye akizungumza katika Kongamano hilo.
Juu na chini ni washiriki katika Kongamano hilo wakimsikiliza Mhe. Balozi Mulamula (hayupo pichani). 
Mke wa wa Waziri Membe, Bi. Dorcas Membe (katikati) kwa pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Uswisi, Mhe. Modest Mero (kulia) nao wakifuatilia ufunguzi wa Kongamano la Diaspora. 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora, Bi. Rosemary Jairo naye akizungumza katika kongamano la Diaspora wakati wa ufunguzi wa Diaspora. 
Msanii wa kizazi kipya Bw. Peter Msechu akiwaongoza mgeni rasmi, Mhe. Membe, meza kuu na washiriki wengine wa kongamano kuimba  Wimbo wa Taifa kabla ya ufunguzi rasmi wa Kongamano.
Maafisa Mambo ya Nje nao wakiimba wimbo wa Taifa.
Sehemu ya washiriki katika Kongamano la Diaspora  nao wakiimba wimbo wa taifa 
Waziri Membe na Bi Dorcas Membe wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la Diaspora mara baada ya shughuli ya ufunguzi kukamilika.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Benard Membe akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula (wa kwanza kulia), Balozi wa Umoja wa Ulaya, Mhe. Sebregond (wa pili kutoka kulia), Mwakilishi wa Baraza la wa Wakilishi Zanzibar, Ali Mzee Ali (wapili kutoka kushoto), Kaimu Mkurugenzi Idara ya Diaspora, Bi Rosemary Jairo (wa kwanza kushoto) na Mwakilishi wa (DICOTA) Bw. Abdul Majid. 
Mhe. Membe pamoja na wageni katika mezaa kuu wakiwa katika picha ya pamoja na Watanzania waishio Ughaibuni

Picha na Reginald Philip


============================================

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete ametoa rai kwa Watanzania wanaoishi ughaibuni (Diaspora) kushirikiana kwa karibu  na Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo (SME’s) ili kuchangia maendeleo ya nchi na hatimaye kuiwezesha Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Katika hotuba yake ya ufunguzi wa Kongamano la Pili la Watanzania waishio ughaibuni (Diaspora) lililofanyika leo kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam , iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe, Rais Kikwete amesema kuwa Serikali yake imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara (SME’s) inashamiri ili kuchangia maendeleo ya nchi na kukuza ajira kwa wananchi wa Tanzania wakiwemo vijana na kuwahimiza Diaspora kushirikiana na sekta hiyo ili kuleta tija.

Rais Kikwete amesema kuwa, lengo la kongamano hili la pili  ni kuwahimiza Watanzania waishio ughaibuni kuuangana na  Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo (SME’s) kwa ajili ya kuleta maendeleo nchini na kutengeza ajira.

“Napongeza kaulimbiu ya kongamano hili la mwaka huu ambayo inahimiza SME’s kufanya kazi kwa pamoja na Wanadiaspora kwa ajili ya kuiletea nchi yetu maendeleo na pia kutengeneza ajira kwa wananchi”, alisema Rais Kikwete.


Aidha, alisema kuwa Kongamano hili ni moja ya jitihada zinazofanywa na Serikali yake katika kuhakikisha Watanzania wanaoishi ughaibuni (Diaspora) wanaunganishwa na kunufaika na sekta  mbalimbali za hapa nchini ikiwemo hiyo ya SME’s  ambayo inachangia asilimia 35 ya pato la taifa.

Mhe. Rais, aliongeza kuwa dhamira ya  serikali  ni kuweka mazingira mazuri Diaspora ili waweze kuja kuwekeza nyumbani na kwamba jitihada hizo ni pamoja na kuifanyia maboresho Sekta ya SME’s kupitia Mpango wa Kurasimisha Rasilimali za Wanyonge Tanzania (MKURABITA)  ili  wafanyabiashara wadogo wapate uwezo wa kufanya biashara rasmi ikiwemo kuwawezesha kufanya biashara nje kwa kushirikiana na  Watanzania wanaoishi ughaibuni  (Diaspora) ambao watasaidia upatikanaji wa  masoko kwa bidhaa  na kuhamasisha wawekezaji wa nje kuja nchini.

Vilevile aliwahimiza Diaspora kuendelea kutoa mchango wao kwa maendeleo ya nchi ikiwemo ujuzi, elimu, mitaji, huduma na kujenga nyumbani kupitia miradi mbalimbali inayotolewa na mashirika ya nyumba likiwemo Shirika la nyumba la Taifa (NHC).

Kwa upande wake, Mhe. Waziri Membe alisema kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ilianzisha Idara ya Diaspora mwaka 2009 kwa lengo la kuwatambua Watanzania wanaoishi ughaibuni na kuwahamasisha kuchangia maendeleo ya nchi kwa kutumia mitaji, ujuzi na elimu wanayoipata wakiwa nje ya nchi.  Aidha, akitoa maoni yake kuhusu suala la uraia wa nchi mbili (Dual Citizenship) Mhe. Membe alisema kuwa bado ana imani kuwa suala hilo litaendelea kujadiliwa ili kuwawezesha Wanadiaspora kuleta  maendeleo ya kweli  nchini.

Awali, akimkaribisha Waziri Membe kuzungumza, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula amesema kuwa dhumuni la kongamano la pili la Diaspora  ambalo limeratibiwa na Wizara kwa  kushirikiana na Ofisi ya Rais-Zanzibar na Ofisi ya Waziri Mkuu ni kuhimiza na kuendelea kutambua mchango wao katika ukuaji wa uchumi nchini na kuwaunganisha Diaspora na Sekta ya Viwanda Vidogo na biashara Ndogo (SME’s).

Kongamano hilo la  siku mbili, linawahusisha Watanzania wanaoishi ughaibuni, wadau mbalimbali kutoka sekta za umma na binafsi na wawakilishi kutoka mikoani.

-Mwisho-