Sunday, October 11, 2015

Silaha za maangamizi zisiishie mikononi mwa makundi ya kihalifu –Tanzania

Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzani katika Umoja wa Mataifa,  Balozi Tuvako Manongi, akichangia majadiliano kuhusu upokonyaji wa silaha na usalama wa kimataifa  mwishoni mwa wiki, ambapo ametoa wito wa jumuiya   ya kimataifa  kushirikiana katika kuhakikisha kuwa silaha za maangamizi haziishii mikononi mwa makundi ya kihalifu.


Na Mwandishi Maalum, New York

TANZANIA imetoa  wito Kwa    Jumuiya ya Kimataifa wa kuhakikisha  inashirikiana  kuhakikisha kwamba silaha za maangamizi  zikiwamo za nyukilia  haziiangukii  mikono ya  makundi ya kihalifu.

Wito huo  umetelewa mwishoni mwa wiki na  Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika  Umoja wa Mataifa,  Balozi Tuvako Manongi,wakati wa Mkutano kuhusu masuala ya   uponyaji wa silaha na  usalama wa kimataifa.

Katika  mkutakno  huo  wazungumzaji wengi walieleza wasiwasi wa  kuwapo kwa  ushirikiano wa karibu kati ya nchi ambazo zina  silaha za nyukilia na zile ambazo hazina, lakini huku zile ambazo zinamiliki silaha hizo zikiendelea kuziboresha na kujilimbikizia.

 “Ni jambo la kusikitisha, badala ya   kuzipungua silaha hizi na hatimaye kuzitokomeza kabisa,  nchi zinazolimiki silaha za nyukilia zinaendelea na kasi ya kuziboresha , kuzifufua na  kujilimbikiza”. Akasema  Balozi Manongi.

Akabainisha kuwa  mbaya Zaidi hata zile  nchi ambazo hazina silaha hizo nazo sasa zinatafuta kila maarifa ya kuwa nazo. Jambao  ambalo  amesema  ni  tishio kwa usalama wa mwanadamu.

Amesisitiza  kuwa ingawa ni  miongo saba imekwisha kupita lakini madhara ya matukio  ya Hiroshima na Nagasaki bado  yanaendelea na yapo  hai  miongoni mwetu.

Balozi  Manongi akaongeza kuwa ni muhimu basi utokomezaji wa  silaha za  nyukilia na teknolojia inayoambatana nazo likaendelea kupewa  kipaumbele pamoja na kuwa na mikataba ya kisheria itakayosimamia  jambo hilo.

Akasema  kutoka na  ongezeko la  ulimbikizaji wa silaha za nyukilia,  Jumuia ya kimataifa inawajibu wa kushirikiana kuhakikisha kwamba silaha hizo na nyingine za maangamizi haziangukii mikononi mwa  makundi ya kigaidi na  kihalifu.

Pamoja na ukweli kwamba silaha za nyukili na zingine za maangamizi  bado ni tishio kubwa kwa uhai wa mwanadamu. Balozi Manongi akasema kwa nchi zinazoendelea  tatizo la usaambaji na matumizi holela ya silaha ndogo na nyepesi  zinaendelea kuwa janga kubwa kwa ustawi na maendeleo ya bara hili  na  kwingineko.

Akimnukuu  Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa  Kofi Annan kwamba  madhara yatokanayo na  matumizi  holela ya silaha  ndogo na nyepesi yameendelea kuwa makubwa sana   na madhara yake  ni makubwa  pengine  kuzidi   mabomu ya atomic yaliyoiangamizia  Hiroshima na  Nagasaki.

Akizungumzia zidi kuhusu matumizi holela ya silaha ndogo na nyepesi,   Mwakilishi huyo wa Tanzania  anasema  mirindimo ya risasi  na   hata  matumizi ya silaha kali zikiwamo za maangamizi,  haiwezi  au haitamhakikishia   mwananchi   maisha yenye hadhi, utu, ustawi na maendeleo.

Akasema kuna uhusiano  mkubwa baina ya  Amani, usalama na utekelezaji wa Malengo ya maendeleo endelevu y (Agenda 2030) malengo yanayojikita katika kumaliza  umaskini pasipo kumwacha yoyote nyuma pamoja na kuilinda sayari dunia.

Akasema  itakuwa   vigumu kuyatekeleza malengo  mapya ya maendeleo   kama kiwango cha gharama za kujilimbikiza silaha kitaendelea ambapo inakadiriwa kuwa  mataifa hasa yale makubwa  yanatumia Zaidi ya dola za  kimarekani trillion 1.7 kwa mwaka  kwa matumizi ya silaha.

Akasema  matumizi ya kiasi hicho cha fedha kujilimbikizia silaha katika maghara mbalimbali duniani   huku mamilioni ya watu wakiendelea kuishi katika umaskini  uliopindukia, na maelfu ya watoto wakiathirika kwa utapia mlo na wengine wakipoteza maisha kwa kukosa  chakula na huduma nyingine za msingi ni jambo lisilo kubalika.

Saturday, October 10, 2015

Rais Kikwete azindua Kiwanda cha Saruji kikubwa Afrika Mashariki na Kati.

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kiwanda cha Saruji kikubwa Afrika Mashariki na Kati cha Dangote Industries Limited kilichopo katika Kijiji cha Mgao Mkoani Mtwara, Tanzania. Kulia kwa Rais ni Mmiliki wa Kiwanda hicho, Alhaji Aliko Dangote na kushoto ni Mwakilishi wa Serikali ya Nigeria, Mallam Nasir Ahmad El-Rufai, Gavana wa Jimbo la Kaduna. Wengine ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete pamoja na wafanyibiashara kutoka nchini Nigeria nao wakishuhudia uzinduzi huo uliofanyika tarehe 10 Oktoba 2015.
Mheshimiwa Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiweka saini kwenye kitabu cha wageni, muda mfupi baada ya kuzindua kiwanda hicho.
Mmiliki wa Kiwanda hicho, Alhaj Aliko Dangote, akifafanua jambo kwa Mheshimiwa Rais juu ya namna kiwanda hicho kinavyofanya kazi ya uzalishaji  wa saruji
Mheshimiwa Rais akipewa maelezo na mmoja wa wataalamu ya namna kiwanda hicho kinavyofanya uzalishaji wa saruji. 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akizungumza na Wafanyibiashara wa Tanzania na Nigeria pamoja na Wananchi waliojitokeza katika kushuhudia ufunguzi wa Kiwanda hicho cha pili kwa ukubwa Barani Afrika na cha kwanza kwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya Mheshimiwa Rais Kikwete kuzindua kiwanda hicho.
Moja ya sehemu ya muonekano wa kiwanda hicho cha Dangote Industries Limited Tanzania. 
Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete akizungumza jambo na mmiliki wa Kiwanda hicho, AlhajI Aliko Dangote.
Picha ya Pamoja.
=====================================
PICHA NA: Reuben Mchome.


Balozi Mulamula atembelea Ubalozi wa Tanzania, Washington DC


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na watumishi wa Ubalozi wa Tanzania Washington DC mara baada ya kuwasili Ubalozini

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akisaini kitabu cha wageni Ubalozini Washington DC.
Katibu Mkuu akiwa katika kikao na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania, Washington DC

Katibu Mkuu akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania Washington



Friday, October 9, 2015

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI



Taarifa zaidi ya Mahujaji kutoka Tanzania huko Saudi Arabia

Idadi ya mahujaji wa Tanzania waliopoteza maisha katika tukio la kukanyagana lililotokea eneo la Mina, Makkah tarehe 24 Septemba, 2015  imeongezeka kutoka 11 na kufikia 12 hadi sasa. Idadi hiyo imeongezeka kufuatia Bi. Aluiya Sharrif Saleh Abdallha kugundulika kuwa ni miongoni mwa mahujaji waliofariki dunia katika tukio hilo. Bi. Abdallah alienda Makkah kufanya ibada ya hijjah kupitia kikundi cha TCDO.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam
09 Oktoba, 2015

Thursday, October 8, 2015

Kaimu Katibu Mkuu azungumza na waandishi wa Habari kuhusu Wiki ya Umoja wa Mataifa

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Simba Yahaya (wa pili kutoka kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa. Pamoja kwenye picha ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez (wa kwanza kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bi.Mindi Kasiga (wa pili kulia). Mwingine ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Celestine Mushy (wa kwanza kulia) 
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez, naye akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani). 
Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Maafisa wa Umoja wa Mataifa nao wakifuatilia mkutano huo pamoja na waandishi wa Habari (hawapo pichani)
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bi.Mindi Kasiga (kulia) akiwafafanulia jambo waandishi wa habari (hawapo pichani).
Mkutano ukiendelea.

Picha na Reginald Philip


Katika kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 25 Oktoba 2015, Watanzania wamehimizwa kuweka mbele suala la amani kuliko kitu kingine chochote. Kauli hiyo imetolewa leo na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Simba Yahaya na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Alvaro Rodriguez kwenye mkutano wa pamoja na waandishi wa habari katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje kama sehemu ya uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa Mataifa ambapo kwa Tanzania, kilele cha maadhimisho hayo yatafanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Siku ya Jumanne tarehe 13 Oktoba 2015.



Kwa upande wake, Bw. Rodriguez alieleza kuwa wakati Umoja wa Mataifa unatimiza miaka 70 tokea kuanzishwa kwake mwaka 1945, dunia imeshuhudia kuidhinishwa kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs)  na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja huo  ambayo yanachukua nafasi ya Malengo ya Milenia (MDGs) yanayofikia kikomo mwaka huu.



“Utekelezaji wa malengo hayo ambao utaanza mwaka 2016 na kukamilika mwaka 2030, unatarajiwa kumaliza umasikini nchini Tanzania  na duniani kwa ujumla”. Bw. Rodriguez alisikika akisema. Aidha, alisema kuwa UN Tanzania itasaidia utekelezaji wa malengo hayo kupitia Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Kusaidia Maendeleo wa Awamu ya Pili (United Nations Development Assistance Plan- UNDAP II). Mpango huo pamoja na mambo mengine, unalenga kusaidia ukuaji wa uchumi shirikishi, kuhamasisha demokrasia, kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi pamoja na kuendeleza huduma za kijamii.



Hivyo, Mratibu Mkazi wa UN aliwaomba waandishi wa habari kuelimisha umma wa Tanzania kuhusu SDGs na kuwasihi kuandika habari zitakazodumisha na kuendeleza amani nchini Tanzania.

Akizungumza katika mkutano huo, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Hassan Simba Yahaya naye aliungana na Mratibu Mkazi wa UN kusisitiza umuhimu wa kutunza amani. Alisema kuwa bila ya amani hakuna kitu chochote cha maendeleo kinachoweza kufanywa. Alitoa mfano wa nchi ambazo zimetekeleza MDGs kwa mafanikio makubwa lakini nchi hizo sasa zimerudi nyuma kwa kukosa amani. 

Vilevile aliwafahamisha waandishi jinsi Tanzania ilivyoshiriki kuandaa malengo hayo ambayo yamezingatia pale yalipoishia malengo ya milenia. Amesema Serikali imeshayawekea mpango wa utekelezaji ambao umezingatia mpango wa maendelea wa miaka mitano wa Serikali.

Aliongeza kuwa lengo la 16 la Maendeleo Endelevu linalozungumza kuhusu amani ndio msingi mkubwa wa vipaumbele vya nchi ya Tanzania. 

"Nafarijika kuona kuwa wengi wenu mliohudhuria mkutano wa leo ni vijana, na hii dunia tunayoitaka kwenye malengo haya ni yenu, ni wajibu wenu kuitunza na sio kuibomoa" alisema na kuongeza kuwa utekelezaji wa SDGs una faida kubwa kwa vijana na taifa kwa ujumla.
Description: https://blogger.googleusercontent.com/img/proxy/AVvXsEifwmjYKS-gMfl_aN9z6GJdGmF04LrzwSY57xswSgnf6JIjFGu8jqWxjD6KtulC3AYA2xtAczb5j-PanN8N3O05RH8fehgpRg8sRRGHDDlPZnKuqBFYy2uJEepBKXXLBONwgygu3Nsi7rVanNtcUK2fs9uY7MR-HM_PZ-Im=s0-d-e1-ft

Wednesday, October 7, 2015

Rais Kikwete apokea hati za utambulisho wa Mabalozi

Balozi mteule wa Hispania nchini Tanzania Mhe. Felix Costales akikabidhi hati ya utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete  Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 7, 2015.
Balozi mteule wa Ubelgiji nchini Tanzania Mhe. Paul Cartier akikabidhi hati ya utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete  Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 7, 2015.
Balozi mteule wa Msumbiji nchini Tanzania Mhe. Monica Patricio Clemente akikabidhi hati ya utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam.Picha zote na Eliphace Marwa – Maelezo