|
Mhe. Balozi Masilingi akisalimiana na Bi. Mariam Mkama, Mtumishi wa Ubalozi, kitengo cha Visa |
|
Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi akizungumza na Mkuu wa Kitengo cha
Visa na huduma za Uhamiaji na wafanyakazi wa kitengo hicho na watumishi
wengine. Kulia ni Bi. Swahiba H. Mndeme, Mkuu wa Utawala na Fedha,
Ubalozini. |
|
Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi (kulia) akipolewa na Bw. Abass
Missana, Mkuu wa Kitengo cha Visa na huduma za Uhamiaji ubalozini hapo. |
|
Mhe. Balozi Masilingi akisalimiana na mmoja wa wateja wa Visa aliyefika Ubalozini kupata huduma hiyo |
|
Mhe. Balozi Masilingi akizungumza na Bw. Arnold NzuaMtemi Nzali wa
Las Vegas, Nevada aliyefika Ubalozini kupata huduma ya Pasipoti | | | | | | | | |
=================================
Katika kutekeleza agizo la Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli,
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Ubalozi wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania, Washington D.C umeendelea kufanya kazi na kutoa
huduma za Visa na Pasipoti kama sehemu ya maadhimisho ya sikukuu hiyo.
Pamoja
na kazi zingine za Ubalozi kuendelea kama kawaida, Mhe. Balozi Wilson
M.Masilingi alitembelea kitengo cha Visa na huduma za Uhamiaji na
kufanya mazungumzo mafupi na Mkuu wa Kitengo hicho Bw. Abbas A. Missana,
Afisa Mambo ya Nje Mwandamizi, (Minister Plenipotentiary). Bw. Missana
alimweleza Mhe. Balozi kuwa kumekuwa na ongezeko la wageni wanaokuja
Ubalozini kuchukua Visa, mara baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe
25 Oktoba, 2015 kumalizika salama.
Hapo awali, kabla ya uchaguzi idadi ya wageni waliokuwa wanafika Ubalozini kuomba Visa ilipungua kwa kiasi kikubwa.
Mhe.
Balozi aliwapongeza Wafanyakazi wa Ubalozi kwa kuitikia wito wa “Uhuru
na Kazi” kwa hamasa kubwa, jambo linalodhihirisha uzalendo na kuheshimu
miongozo sahihi toka kwa Mkuu wa Nchi na wasaidizi wake.
Aidha, aliwataka Watumishi wa Ubalozi kuendelea kuboresha huduma kwa wateja ili kulinda heshima ya nchi yetu.