Friday, February 5, 2016

JOB OPPORTUNITIES-INTERNATIONAL TELECOMMUNICATION UNION (ITU)


JOB OPPORTUNITIES WITHIN THE INTERNATIONAL TELECOMMUNICATION UNION (ITU)

The Ministry of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation has received an advert on various job opportunities from the International Telecommunication Union (ITU) for qualified individuals, particularly women to apply. 

The vacancies and application deadline are as follows:-

    i.        1. Information Systems Engineer-Deadline: 18 March 2016;

  ii.        2. Technical Support Officer-Deadline: 15 March 2016;

iii.     3. Head, Least Developed Countries Division-Deadline: 14 March 2016; and

iv.        4. Head, Area Office, Moscow-Deadline: 14 March 2016

For further details on the above mentioned vacancies including application procedures can be accessed at http://www.itu.int/employment/Recruitment/index.html.

“The Ministry encourages qualified Tanzanians to apply”.

Issued by: The Ministry of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation, Dar es Salaam.
05th February, 2015

Thursday, February 4, 2016

Kaimu Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje akutana na Balozi wa India kuhusu kudhalilishwa kwa Mtanzania nchini India

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi (kulia) akizungumza na Balozi wa India hapa nchini, Mhe. Sandeep Arya alipomwita Wizarani kufuatia taarifa za kushambuliwa na kudhalilishwa kwa mwanafunzi wa kike kutoka Tanzania na kundi la watu nchini India. Katika mazungumzo yao Balozi Mwinyi alisema Serikali ya Tanzania imesikitishwa  na inalaani vikali kitendo hicho. Pia alimtaka kufikisha ujumbe kwa Serikali yake ya kuchukua hatua kali kwa wote watakaopatikana na hatia ya tukio hilo na kuwahakikishia ulinzi Watanzania waliopo nchini India.Mazungumzo yalifanyika tarehe 04 Februari, 2016.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga kwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Mwinyi na Balozi Arya (hawapo pichani)
Mazungumzo yakiendelea.

Serikali ya Tanzania yalaani kudhalilishwa kwa mwanafunzi nchini India

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali juu ya kitendo cha kushambuliwa na kudhalilishwa kwa mwanafunzi wa kike wa Kitanzania nchini India. Hatua hizo ni pamoja na kikao chake na Balozi wa India hapa nchini, Mhe. Sandeep Arya ambapo Serikali ilimtaka Balozi huyo kufikisha ujumbe nchini kwake wa kuwahakikishia ulinzi raia wa Tanzania waliopo India na kuwachukulia hatua za kisheria wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo. Mkutano ulifanyika Wizarani tarehe 04 Februari, 2016
Sehemu ya Waandishi wa Habari waliohudhuria Mkutano huo.


Sehemu nyingine ya Waandishi wa Habari
Mkutano ukiendelea
Wanahabari wakiwa kazini

==================================================

Serikali ya Tanzania imesikitishwa na inalaani vikali kitendo cha udhalilishwaji alichofanyiwa mwanafunzi wa kike wa Kitanzania na Kundi la watu katika jimbo la Bangalore nchini India.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi alipokutana na Wandishi wa Habari kwa ajili ya kuwaeleza hatua zilizochukuliwa na Serikali kufuatia kitendo hicho cha kudhalilishwa kwa mwanafunzi wa Kitanzania nchini India.

Balozi Mwinyi alisema kuwa, hatua zilizochukuliwa ni pamoja na Ubalozi wa Tanzania nchini India kuiandikia Serikali ya nchi hiyo kuomba maelezo kamili kuhusu tukio hilo pamoja na kuitaka Serikali ya India kuwachukulia hatua za kisheria watu wote waliohusika pamoja na kuimarisha usalama katika maeneo wanayoishi wanafunzi wa Kitanzania.

Aidha, Balozi Mwinyi alieleza kuwa amemwita Balozi wa India hapa nchini, Mhe. Sandeep Arya na kumweleza masikitiko ya Serikali ya Tanzania kufuatia kitendo hicho cha kushambuliwa na kudhalilishwa kwa mwanafunzi wa kike kutoka Tanzania.

Katika mazungumzo yao, Balozi Arya alieleza bayana kuwa Serikali ya India imesikitishwa na tukio hilo la udhalilishaji na kwamba Serikali imeahidi kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika kutekeleza uovu huo.
 Alisema kuwa Waziri Mkuu wa Jimbo la Bangalore aliongea na umma kuelezea masikitiko yake kuhusu uovu huo na kuahidi kuwa mamlaka za jimbo hilo zitaimarisha usalama katika maeneo yote wanayoishi wanafunzi wa Tanzania na raia wengine kutoka nje.

Balozi Arya aliihakikishia Serikali ya Tanzania kuwa India inaheshimu ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na nchi yake, hivyo itashughulikia suala hilo kwa ukamilifu na hadi wakati huu tayari watu watano wanashikiliwa na vyombo vya usalama wakituhumiwa kuhusika na tukio hilo.

Sanjari na taarifa hiyo, Balozi Mwinyi aliwaomba Watanzania kutohusisha tukio hili la uhalifu na ajali ya Mtanzania, Bw. Christian Benjamin Mlyansi iliyotokea nchini India jana usiku na kusababisha kifo chake. Alisema kuwa Bw. Mlyansi alipata ajali ya kawaida alipokuwa anaendesha pikipiki ambapo ilipoteza mwelekeo na kugonga ukingo wa kati wa barabara. 

-Mwisho-







Balozi Mwinyi akutana na Katibu Mtendaji wa ALAT

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Ramadhani Mwinyi akiwa katika mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania (Association of Local Authorities of Tanzania-ALAT), Bw. Abraham Shamumoyo. Katika mazungumzo hayo, Bw. Shamumoyo alitoa taarifa fupi kuhusu muundo na utendaji kazi wa ALAT. Aidha, Bw. Shamumoyo alitoa taarifa za awali kuwa Jumuiya hiyo kwa upande wa Kanda ya Mashariki mwa Afrika inakusudia kutuma maombi Serikalini ili makao makuu yake yawe Tanzania.
Mazungumzo yakiaendelea, wengine katika picha, kutoka kulia ni Bw. Elisha Suku na Balozi Baraka Luvanda ambao ni maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje. Pembeni kwa Bw. Shamumoyo ni maafisa wa ALAT.

Wednesday, February 3, 2016

Dkt. Mahiga aapa kuwa Mbunge

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika  Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dkt.  Augustine Mahiga akiapa  Bungeni mjini Dodoma Februari 2, 2016.


Monday, February 1, 2016

Kampuni Binafsi za Tanzania zashiriki Maenesho ya Utalii nchini Uholanzi


Mhe. Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju akiwa katika ya pamoja na Bi. Selma Kamm-Melai (kulia) na Bw. Yohannes Ngomi- Kamm (wa pili kutoka kulia) Wawakilishi wa Kampuni ya Utalii ya MAKASA SAFARIS iliyopo Moshi, Tanzania walioshiriki katika Maonesho ya Utalii ya Holiday Fair 2016 (Vakatiebeurs 2016) yaliyofanyika hivi karibuni mjini Utrecht.  Kushoto ni Bi. Agnes Kiama Tengia, Afisa Ubalozi.

Baadhi ya Makampuni binafsi ya Utalii nchini Tanzania yalishiriki katika Maonesho hayo maarufu yanayofanyika kila mwaka katika miji ya Amsterdam, Utrecht na Maastricht, Uholanzi ambapo huvutia maelfu ya washiriki kutoka nchi mbalimbali duniani. Maonesho ya Vakantiebeurs hutoa fursa kwa nchi kujitangaza hususan katika sekta ya utalii. Ubalozi wa Tanzania ulihudhuria Maonesho hayo na kukutana na Wawakilishi wa baadhi ya Makampuni hayo binafsi kutoka Tanzania.


Watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uholanzi wakiwa katika picha ya pamoja na Bw. Kassim Abdallah, Mwakilishi wa Kampuni ya BOBBY TOURS kutoka Arusha Tanzania aliyeshiriki katika Maonesho ya Vakantiebeurs 2016 yaliyofanyika katika miji ya Amsterdam na Utrecht, Uholanzi hivi karibuni. Kutoka kulia ni Bi. Flora Williams, Bw. Peter Mihyona Bi. Agnes K. Tengia.


Mhe. Balozi Irene F.Kasyanju akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa Kampuni ya KILIDOVE ya Arusha, Tanzania walioshiriki katika Maonesho ya Vakatiebeurs 2016 yaliyofanyika mjini Utrecht hivi karibuni.