Tuesday, March 29, 2016
Thursday, March 24, 2016
Tanzania na Saudia zasaini mkataba wa ushirikiano katika masuala ya uchumi na uwekezaji
Rais Magufuli akizungumza na Waziri Adel Al Jubair (kushoto) |
Waziri Mahiga na Waziri Al Jubair wakibadilishana mkataba mara baada ya kusainiwa |
Mhe. Rais Magufuli akiagana na Waziri Al Jubair |
Waziri Al Jubair akiagana na Waziri Mahiga mara baada ya kumaliza mazungumzo na Mhe. Rais Magufuli na zoezi la uwekaji saini kukamilika. |
Picha na Reginald Philip
Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje yaitaka Wizara kusimamia Sera ya Diplomasia ya Uchumi
Waziri Mahiga, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dkt Susan Kolimba (Mb.) na Katibu Mkuu wa Wizara, Balozi Aziz Mlima wakifuatilia kikao hichoambapo
kamati ilipokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa
Wizara. Sambamba na hilo Wajumbe wa kamati hiyo wameitaka wizara kuweka
mikakati na kuongeza jitihata zaidi katika kuhakikisha inazitangaza fursa za biashara na uwekezaji zilizopo nchini.
Sehemu ya Waheshimiwa Wabunge ambao ni wajumbe wa kamati hiyo wakifuatilia mazungumzo.
Sehemu nyingine ya Waheshimiwa Wabunge.
Sehemu ya Wakurugenzi na Maafisa wa Wizara wakifuatilia kikao.
Sehemu nyingine ya Wakurugenzi na Maafisa kutoka Wizarani wakifuatilia kikao
Wednesday, March 23, 2016
Waziri Mahiga azungumza na Kundi la Mabalozi wa Afrika waliopo nchini
Mhe. Dkt. Mahiga alizungumza na Kiongozi wa Mabalozi hao ambaye pia ni Balozi wa Zimbabwe nchini, Mhe. Edzai Chimonyo |
Waziri Mahiga akisalimiana na Balozi wa Kenya nchini Mhe. Chirau Ali Mwakwere wakati wa mkutano wake na Kundi la Mabalozi wa Afrika. Kulia ni Balozi wa DRC, Mhe.Jean Pierre Tshampanga Mutamba. |
Waziri Mahiga akisalimiana na Balozi wa Rwanda nchini Mhe. Eugene Kayihura wakati wa mkutano wake na Kundi la Mabalozi wa Afrika. |
Waziri Mahiga akisalimiana na Kaimu Balozi wa Burundi nchini, Bw. Prefere Ndayishimiye |
Dkt. Mahiga akisalimiana na Mwakilishi wa Ubalozi wa Angola nchini, Bw. Joel Cumbo |
Tuesday, March 22, 2016
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje afanya ziara Chuo cha Diplomasia
Naibu Waziri akiangalia vitabu vilivyopo kwenye Maktaba ya Chuo hicho |
Naibu Waziri akiwaeleza jambo uongozi wa chuo hicho. |
Naibu Waziri akikagua Darasa la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Chuo cha Diplomasia |
Dkt. Suzana Kolimba akizungumza na uongozi wa Chuo cha Diplomasia mara baada ya kumaliza kuzungukia eneo la Chuo cha Diplomasia |
Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia naye akizungumza wakati Naibu Waziri alipotembelea Chuo hicho |
Naye Mkurugenzi wa Taaluma, Dkt. Watengere Kitojo akielezea jambo wakati wa mazungumzo na Naibu Waziri |
Mkuu wa Kitengo cha Uhasibu Chuoni hapo Dkt. Charles Bekon akionesha Mpango Mkakati wa Chuo cha Diplomasia ikiwemo mfano wa michoro ya majengo ya Chuo. |
Naibu Waziri Dkt. Susan Kolimba akitazama sampuli ya michoro ya majengo yanayotarajiwa kujengwa Chuoni hapo |
Dkt. Susan akisalimiana na Wakufunzi wa Chuo cha Diplomasia mara baada ya kuwasili Chuoni hapo. |
Picha na Reginald Philip
=========================================================================================================
Naibu Waziri Dkt. Kolimba aeleza nia ya Wizara katika kuendeleza Chuo cha Diplomasia
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa imejipanga kuhakikisha Chuo cha Diplomasia kinaboresha huduma zake za utoaji elimu na mafunzo ya masuala ya Diplomasia ili kukidhi mahitaji ya Watanzania katika taaluma hiyo.
Hayo yalibainishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Kolimba alipofanya ziara katika Chuo hicho kilichopo Kurasini Jijini Dar es Salaam ambacho ni moja ya Taasisi zilizo chini ya Wizara.
Mhe. Kolimba alisema kwamba Chuo cha Diplomasia ambacho kilianzishwa kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania na Msumbiji ni miongoni mwa vyuo vilivyojipatia sifa kubwa ndani na nje ya nchi kwa kutoa mafunzo katika masuala ya Diplomasia na hivyo Wizara haina budi kuhakikisha inaendelea kukiboresha ili kuhakikisha kinakidhi viwango vya kitaifa na kimataifa.
Mhe. Dkt. Susan alisema kuwa, miongoni mwa masuala yanayotakiwa kufanyiwa kazi katika maboresho hayo ni pamoja na miundombinu ya Chuo kwa maana ya kuongeza majengo, vifaa vya kisasa vya kufundishia, maabara za kisasa za lugha, maktaba na kuongeza Wakufunzi.
Aidha, Mhe. Kolimba aliueleza Uongozi wa Chuo hicho kuwa ni vema vipaumbele katika kukiletea chuo maendeleo vikaainishwa ikiwa ni pamoja na kuonyesha mikakati ya kila changamoto ili kupata suluhisho la haraka la changamoto hizo.
“Ninawapongeza kwa kazi nzuri mnayofanya na tunaahidi kuwa pamoja nanyi wakati wote ili kuhakikisha Chuo chetu kinafikia viwango vinavyostahili” alisema Mhe. Kolimba.
Vilevile alieleza kuwa ni vema Chuo kikaimarisha ushirikiano na Vyuo vingine vya ndani na nje kwa kuainisha maeneo muhimu ya ushirikiano yenye faida kwa pande zote. Pia alikitaka Chuo kuwa na mikakati itakayokiwezesha Chuo hicho kuweza kujiendesha kibiashara kama vyuo vingine nchini na kuacha utegemezi mkubwa katika bajeti ya Serikali.
Awali akimkaribisha Naibu Waziri Chuoni hapo, Mkurugenzi wa Chuo hicho, Balozi Mohammed Maundi alisema kuwa Chuo hicho kinaendelea kuboresha maeneo mbalimbali ya Chuo hicho ikiwemo kuanzishwa kwa Kozi ya Shahada mwaka 2015 na tayari chuo kimepata michoro ya majengo kwa Chuo kipya wanachotarajia kukijenga na sasa kinachohitajika ni fedha ili kukamilisha mpango huo ambao kwa kiasi kikubwa utamaliza changamoto zinazokikabili Chuo.
Chuo cha Diplomasia (CFR) ni chuo kilichoanzishwa kwa ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania na Msumbiji mwaka 1978. Chuo kimekuwa kikitoa elimu katika ngazi ya Cheti, Diploma, Shahada na Shahada ya Juu.
-Mwisho-
Subscribe to:
Posts (Atom)