Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akisoma hotuba ya bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2018/2019 bungeni jijini Dodoma. Mapema leo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepisha kiasi cha Shilingi
Bilioni Mia Moja Sabini na Saba, Milioni Sita na Mia Mbili Thelathini na Mbili
Elfu. Kati
ya fedha hizo Shilingi Bilioni Mia Moja Sitini na Sita, Milioni Mia Sita na
Sita, na Mia Mbili Thelathini na Mbili Elfu ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida, na Shilingi Bilioni Kumi na Milioni Mia Nne ni kwa ajili ya bajeti ya
maendeleo.
Pro. Adolf F. Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,(wa kwanza kushoto) akifuatilia uwasilishwaji wa hotuba ya bajeti ya Wizara. Wa pili kutoka kushoto, ni Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhani Mwinyi akifuatilia hotuba.
Sehemu ya Watendaji wa Wizara wakifuatilia hotuba ya bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2018/2019 iliyowasilishwa na kupishwa bungeni jijini Dodoma
Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga akijibu maswali bungeni mara baada ya kuwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2018/2019
Mhe. Dkt. Susan Kolimba Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kushoto), akifuatilia hotuba ya bajeti bungeni jijini Dodoma
Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akifafanua jambo mara baada ya kuwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara.
Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akisalimiana na Dkt. Stergomena Tax Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) walipokutana katika viunga vya Bunge jijini Dodoma mara baada kuwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara.
Mhe. Waziri Mahiga akijadili jambo na Mhe. Zitto Kabwe Mbunge wa Kigoma Mjini katika viunga vya Bunge jijini Dodoma mara baada ya kupitishwa kwa hotuba ya bajeti ya Wizara
Mhe. Waziri Mahiga na Mhe. Naibu Waziri Kolimba wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Waheshimiwa Mabalozi na Watendaji wa Wizara waliohudhuria tukio la uwasilishwaji wa bajeti ya Wizara bungeni jijini Dodoma
HOTUBA YA MHESHIMIWA BALOZI DKT. AUGUSTINE PHILIP MAHIGA
(MB), WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI AKIWASILISHA
BUNGENI MAKADIRIO YA BAJETI YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA
2018/2019
ORODHA
YA VIFUPISHO
AF
Adaptation
Fund
AfDB
African Development Bank
AfCFTA
African Continental Free Trade
Area
AGOA
African Growth and Opportunity
Act
AICC
Arusha
International Conference Centre
AMISOM
African Union Mission to Somalia
APRM
African Peer Review Mechanism
BBC
British Broadcasting Corporation
CGTN
China Global Television Network
COMESA
Common Market for Eastern and
Southern Africa
COP
Conference of Parties
DW
Deutsche Welle
EAC
East African Community
EPA
Economic Partnership Agreement
FAO
Food and Agriculture
Organization
FIB
Force Intervention Brigade
FOCAC
Forum on China-Africa
Cooperation
ii
GCF
Green Climate Fund
GEF
Global Environment Facility
GIZ
The Deutsche Gesellschaft für
Internationale Zusammenarbeit
GmbH
GPEDC
Global Partnership for Effective
Development Cooperation
IAEA
International Atomic Energy
Agency
IGAD
Intergovernmental Authority on
Development
ILO
International Labour
Organization
IMF
International Monetary Fund
IOM
International
Organization for Migration
IORA
Indian Ocean Rim Association
JNICC
Julius
Nyerere International Convention
Centre
KCB
Kenya Commercial Bank
KOICA
Korea International Cooperation
Agency
LDCF
Least Developed Countries Fund
iii
MINUSCAUnited Nations Multidimensional
Integrated
Stabilisation
Mission in the Central African Republic
MK-ICCMt. Kilimanjaro International
Convention
Centre
MONUSCOUnited Nations Organisation
Stabilisation
Mission
in the Democratic Republic of the Congo
NPTNon – Proliferation Treaty
PSPFPublic Sector Pension Fund
RFIRadio France International
RMBRenminbi
SADCSouthern African Development
Community
SDGsSustainable Development
Goals
TAZARATanzania-Zambia Railway Authority
TBCTanzania Broadcasting Corporation
TEHAMATeknolojia ya Habari na
Mawasiliano
TICTanzania Investment Centre
TMEATrademark East Africa
UKIMWIUpungufu wa Kinga Mwilini
iv
UNAMID
United
Nations African Union Mission in Darfur
UNDP
United Nations Development Progamme
UNDAP
United
Nations Development Assistance Plan
UNEP
United Nations Environment Progamme
UNESCO
United
Nations Educational Scientific and Cultural Organization
UNFPA
United Nations Population Fund
UN-HABITAT
United
Nations Human Settlement Programme
UNHCR
United
Nations High Commission for Refugees
UNICEF
United
Nations Children’s Emergency Fund
UN-ICTR
United
Nations International Criminal Tribunal for Rwanda
UNIDO
United
Nations Industrial Development Organization
UNIFIL
United Nations Interim Force in Lebanon
UNISFA
United
Nations Interim Security Force for Abyei
v
UNMISSUnited Nations Mission in the
Republic
of South Sudan
UTTUnit Trust of Tanzania
VoAVoice of America
WHOWorld Health Organization
WTOWorld Trade Organization
WWFWorld Wildlife Fund
vi
UTANGULIZI
1.Mheshimiwa Spika, baada ya Mwenyekiti wa Kamatiya
Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuwasilisha Taarifa ya
Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara, naomba sasa kutoa hoja kwamba Bunge
lako Tukufu likubali kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa mpango na
bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa mwaka
wa fedha 2017/18. Aidha, naomba Bunge lako Tukufu lijadili na kupitisha Mpango
na Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2018/19.
2.Mheshimiwa Spika, awali ya yote napendakumshukuru
Mwenyezi Mungu, mwingi wa fadhila na rehema, kwa
kutujalia afya njema na kutuwezesha kukutana tena katika Bunge lako Tukufu, kujadili Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya
Wizara yangu.
3.Mheshimiwa Spika, naungana na wenzanguwalionitangulia
kuwashukuru na kuwapongeza watoa hoja waliozungumza kabla yangu, hususan Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mheshimiwa Dkt. Philip Isdory
Mpango (Mb), Waziri wa Fedha na Mipango ambao kwa hakika hotuba zao sio tu
zimezungumzia mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano, bali pia zimetoa dira
katika mustakabali wa taifa letu kwa kuainisha masuala muhimu ya kitaifa,
kikanda na kimataifa ambayo baadhi yake yanagusa majukumu ya Wizara yangu.
1
4.Mheshimiwa Spika, naomba pia nitumie fursa hiikutoa
shukrani zangu kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama
chini ya uongozi wa Mhe. Mussa Azan Zungu (Mb) na Makamu wake Mhe. Salum Mwinyi
Rehani (Mb). Kamati hii imetoa mchango mkubwa na imekuwa muhimili muhimu katika
kuiwezesha Wizara yangu kutekeleza majukumu yake kwa kutoa ushauri kuhusu
masuala mbalimbali ya kiutendaji.
5.Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee naombanitumie
nafasi hii kuwashukuru Mheshimiwa Dkt. Susan Alphonce Kolimba (Mb), Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki; Prof. Adolf Faustine
Mkenda, Katibu Mkuu; Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi, Naibu Katibu Mkuu;
mabalozi wa Tanzania nje ya nchi; Wakuu wa Idara na Vitengo; watumishi wa
Wizara; na taasisi zilizo chini ya Wizara yangu kwa kujituma na kutekeleza
majukumu yao kwa weledi na kufanikisha kwa kiwango cha juu utekelezaji wa
bajeti ya mwaka wa fedha 2017/18, pamoja na kuandaa Bajeti ya Wizara ya mwaka
wa fedha 2018/19.
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani ambaye anawakilisha pia na Vatican, Mhe. Dkt. Abdallah Saleh Possi, akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Baba Mtakatifu Papa Francis, Vatican tarehe 17 Mei 2018.
Kabla ya kuwasilisha Hati za Utambulisho, Balozi Dkt. Possi alipata fursa ya kukutana na viongozi muhimu wa Vatican, wakiwemo Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu Mkuu wa Mambo ya Nchi za Nje na ushirikiano wa kimataifa, Askofu Mkuu Angelo Becciu, Katibu Mkuu Msaidizi wa Vatican.
Mabalozi wengine waliowasilisha Hati za Utambulisho ni pamoja na Balozi Ahmad Naseem Warraich kutoka Pakistan, Balozi Risto Piipponen kutoka Finland, Balozi Lundeg Purevsuren kutoka Mongolia, Balozi Retšelisitsoe Calvin Masenyetse kutoka Lesotho, Balozi Karsten Vagn Nielsen kutoka Denmark, na Balozi Sulaiman Mohammed kutoka Ethiopia.
Baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho, Balozi Dkt. Possi alipata fursa ya kukutana na Jumuiya ya Watanzania wanaoishi Vatican. Katika kikao hicho, Dkt. Possi aliwaeleza Watanzania hao kwamba wana jukumu kubwa la kutumia.nafasi zao kuhakikisha nchi ya Tanzania inadumu katika misingi ya uadilifu, umoja, na amani ambavyo ni misingi muhimu ya maendeleo.
Balozi Dkt. Possi akisalimiana na Katibu Mkuu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin.
Balozi Dkt. Possi na Mama Balozi, Bi. Sada Mshana, katika picha ya pamoja na Baba Mtakatifu Papa Francis. Picha kwa hisani ya Vatican
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Balozi Innocent E. Shiyo (Katikati) akifunga Warsha ya siku tatu(3) ya Mafunzo ya Mfumo wa Ufuatialiaji na Tathmini wa SADC (SADC Results Based Online Monitoring and Evaluation System), mmoja wa Wakufunzi wa Warsha hiyo kutoka SADC Bi. Lerato Moleko(kulia) na wa mwisho kushoto ni Bw. Meneja Mradi kutoka GIZ Bw. Robson Chakwama.
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Wizara kwa kushirikiana na Serikali ya Ujerumani chini ya Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) na Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), yametolewa kwa Maafisa wa Serikali na Taasisi za Umma, tarehe 15 - 17 Mei,2018 katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
Hafla hiyo ikiendelea
Sehemu ya Maafisa kutoka Wizarani wakifuatilia hafla ya kufunga mafunzo hayo
Sehemu ya Washiriki wakifuatilia hafla ya kufunga mafunzo hayo
Bi. Felister Rugambwa ambaye alikuwa Mshereheshaji wa shughuli hiyo akitoa utaratibu wa shughuli.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Jestas Nyamanga akizungumza na Balozi wa Italia nchini, Mhe. Roberto Mengoni alipofika Wizarani kwa mazungumzo kuhusu ushirikiano baina ya Tanzania na Italia.
Bi. Tunsume Mwangolombe, Afisa Mambo ya Nje akinukuu mazungumzo kati ya Bw. Nyamanga na Balozi Mengoni(hawapo pichani)
VACANCY ANNOUNCEMENT FROM THE SOUTHERN
AFRICA DEVELOPMENT COMMUNITY SECRETARIAT (SADC)
The
Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation has received 50 vacant
positions from the Southern Africa Development Community Secretariat (SADC)
inviting qualified Tanzanians to apply. The vacant positions are open to all 16 member countries.
Interested Tanzanians are required to present their
application letters not later than or on 30th May 2018 through the
following address:-
Permanent Secretary,
President's Office,
Public Services Management
University of Dodoma,
P.O.Box 670,
40404 DODOMA.
Applicants may also
send their application letters through this Email address: - ps@utumishi.go.tz or shiyo27@yahoo.co.uk.
For further details
please visit the following websites: - www.sadc.int
or www.utumishi.go.tz or www.foreign.go.tz. We are sending an attachment of the stated positions with this press release.
NB: The SADC positions are highly competitive. Thus, interested candidates are advised to send their Curriculum Vitae that meets regional and international standards.
Issued by:
Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs and East African
Cooperation,
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini, Bi. Sarah Cooke kuhusu ushirikiano kati ya nchi hizi mbili. Katika mazungumzo yao walijadilikwenye ushirikiano katika sekta mbalimbali.