Wednesday, June 13, 2018

Waziri afanya mazungumzo na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akimkaribisha Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Maziwa Makuu Mhe. Said Djinnit alipomtembelea Wizarani terehe 13 Juni 2018, Dar es Salaam. Anayeshuhudia kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, Bw. Alvaro Rodriguez.

Mjumbe huyo alifika Wizarani kwa lengo la kuzungumzia hali ya usalama na amani katika nchi za Maziwa Makuu.Aidha, mjumbe huyo alimuomba Mhe. Waziri kufikisha shukrani zake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kwa mchango mkubwa wa Tanzania katika kusaidia kutunza amani ya nchi za Maziwa Makuu.

 Mhe. Waziri Mahiga akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Mhe.Djinnit.
Mkutano ukiendelea, wanaoshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Bw. Salvatory Mbilinyi(wa kwanza kulia kwa Waziri), Bw. Ally Ubwa Afisa Mambo ya Nje na Bw. Magabilo Murobi Katibu wa Waziri na kushoto ni Ujumbe wa Mhe. Djinnit alioongozana nao.

Tuesday, June 12, 2018

Naibu Katibu Mkuu afanya mazungumzo na Mabalozi wa Uturuki, Algeria, Kuwait na Palestina.

Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhan M. Mwinyi( wa kwanza kushoto) akiwasikiliza Mabalozi wa Uturuki, Palestina, Algeria na Kuwait ( hawapo pichani) walipomtembelea Wizarani tarehe 12 Juni,2018,Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Bw. Suleiman Saleh na Mwisho ni Afisa Mambo ya Nje Bw. Fidelis Odiro wakifuatilia mazungumzo hayo. 
Pamoja na mambo mengine mazungumzo hayo yalijikita katika kujadili namna ya kuendelea kuboresha mahusiano yaliyopo kati ya Tanzania na nchi hizo. Pia walizungumzia kuhusu azimio la Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wa Palestine.
Balozi wa Algeria Mhe. Saad Belabeb(wa kwanza kushoto), Balozi wa Kuwait nchini Mhe.Jasem Ibrahim Al Najem, Balozi wa Palestine nchini Mhe.Hazem Shabat na mwisho ni Balozi wa Uturuki nchini Mhe.Ali Davutaglu wakimsikiliza Balozi Mwinyi (hayuko pichani) katika mazungumzo hayo.

Wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo.

Balozi Chana pamoja na Balozi Mboweto wawasilisha Hati za Utambulisho.

Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Pindi Chana akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Sudan ya Kusini Mhe. Salvar Kiir mara baada ya kuwasilisha Hati za utambulisho. Balozi Chana mwenye makaazi jijini Nairobi nchini Kenya pia anaiwakilisha Tanzania nchini Sudani Kusini.  


Balozi Mteule wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidini Ally Mboweto, alikabidhi Hati za Utambulisho kwa Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Nigeria Mhe. Muhammadu Buhari. Hafla hiyo ilifanyika katika Ikulu ya nchi hiyo Jijini Abuja na kuhudhuriwa na Mkewa Mhe. Balozi Hajat Ashura Ally Mboweto, Maafisa wa Ubalozi na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Nigeria.
Balozi Muhidin Ally Mboweto akisindikizwa na Mkuu wa Itifaki kuelekea eneo la gwaride.
Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidin Ally Mboweto akipigiwa wimbo wa Taifa na tayari kwa ukaguzi wa gwaride.
Ukaguzi wa gwaride
Balozi Mboweto akisaini kitabu cha wageni alipowasili Ikulu ya Nigeria tayari kwa kukabidhi Hati za Utambulisho kwenye taifa hilo.
Rais wa Shirikisho la  Jamhuri ya Nigeria Mhe. Muhammadu Buhari akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Muhidin Ally Mboweto kama Balozi wa Tanzania nchini Nigeria.
Mhe. Buhari akizungumza na Balozi Mboweto mara baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho. 






Monday, June 11, 2018

Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje akutana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya UN nchini

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda (kulia) akizungumza na  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, Bw. Alvaro Rodriguez alipofika Wizarani tarehe 11 Juni, 2018 kwa ajili ya kuzungumzia masuala mbalimbali kuhusu ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na Serikali ya Tanzania pamoja na utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG's) hapa nchini. Kwa upande wake, Prof. Mkenda alipongeza Mpango wa One UN unaotekelezwa na Ofisi za Umoja wa Mataifa hapa nchini kwa vile unarahisisha utekelezaji wa majukumu na kushukuru ushirikiano mzuri uliopo kati ya Umoja wa Mataifa na Tanzania hususan katika program za kupunguza umaskini na maendeleo endelevu.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimatifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Celestine Mushy akiwa na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Eva Ng'itu wakifuatilia mazungumzo kati ya Prof. Mkenda na Bw. Rodriguez hawapo pichani
Bw. Rodriguez nae akimweleza jambo Prof. Mkenda
Mazungumzo yakiendelea
Picha ya pamoja


Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje akutana na Mwakilishi Mkazi wa WFP nchini

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda (kulia) akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini, Bw. Michael Dunford alipofika Wizarani kwa ajili ya kuzungumzia masuala mbalimbali kuhusu utekelezaji wa majukumu unaofanywa na Shirika hilo hapa nchini. Pamoja na mambo mengine Mwakilishi huyo aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mkubwa anaopata katika kutekeleza majukumu yake. Shirika la WFP hapa nchini linajishughulisha katika kusaidia miradi mbalimbali ya kilimo katika kuwajengea uwezo wakulima wadogo, lishe na kusaidia upatikanaji wa soko kwa wakulima wadogo.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimatifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Celestine Mushy kwa pamoja na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Eva Ng'itu wakifuatilia mazungumzo kati ya Prof. Mkenda na Bw. Dunford hawapo pichani
Bw. Dunford akifafanua jambo kwa Prof. Mkenda wakati wa mazungumzo yao
Mazungumzo yakiendelea
Prof. Mkenda akiagana na Bw. Dunford mara baada ya mazungumzo kati yao

Friday, June 8, 2018

Mzigo wa kwanza wa Muhogo mkavu kutoka Tanzania waingia China.

 

 Kufuatia hatua ya kusainiwa Mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na China kuruhusu bidhaa za Muhogo mkavu kutoka Tanzania kuingia katika soko la china, mzigo wa kwanza wa kontena nne(4) za muhogo mkavu kutoka Tanzania zimeingia China wiki hii kupitia Bandari ya Qingdao. Tukio hili la Kihistoria linafungua ukurasa mpya wa zao la muhogo kuwa miongoni mwa mazao ya biashara, hivyo Serikali inawahimiza Watanzania kuchangamkia fursa hii.
 Sehemu ya magunia yenye muhogo huo kutoka Tanzania yakipakuliwa.


Sehemu ya Muhogo huo.


Thursday, June 7, 2018

Naibu Katibu Mkuu akutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Poland nchini



 Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhan M. Mwinyi, akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Poland nchini Mhe. Krzysztof Buzalski alipomtembelea Wizarani tarehe 07 Juni,2018, Dar es Salaam, 

Mazungumzo hayo pamoja na mambo mengine yalijikita katika kuboresha mahusiano yaliyopo kati ya Tanzania na Poland. Balozi Mwinyi alisema Poland ni kati ya nchi ambazo Mahusiano yake yameleta manufaa katika nyanja mbalimbali za uchumi hapa nchini, hasa katika eneo la kuendeleza kilimo cha kisasa. Itakumbukwa hivi karibuni nchi ya Poland  imetoa mkopo wenye masharti nafuu kwa ajili ya ujenzi wa maghala yanayotumia teknologia ya kisasa kuhifadhi nafaka katika Mikoa mitano(5) hapa nchini.

Naye Balozi Buzalski alisema Poland inafurahishwa na Juhudi za Serikali ya awamu ya tano(5) ya Kujenga Tanzania ya Viwanda na amesema kilimo ni kati ya eneo muhimu ambalo litasaidia Tanzania kufikia adhma hiyo kwa haraka ndio maana wameamua kuongeza nguvu kwenye eneo hili nyeti. 
Ili kuwajengea uwezo Watanzania Poland imefungua tena fursa za masomo nchini humo katika maeneo mbalimbali hivyo Watanzania wanashauriwa kuchangamkia fursa hizo zitakapotangazwa

Aidha, Balozi Buzalski pia amesema eneo lingine muhimu ni katika sekta ya utalii ambapo hadi sasa watalii kutoka Poland wameongezeka maradufu ambapo jumla ya watalii 12,000 kutoka Poland wanatembelea Tanzania kwa Mwaka na kati ya hao Watalii 10,000 wanaenda Zanzibar.
 
 Mkutano ukiendelea, wanofuatilia kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Europe na Amerika Bi Mona Mahecha na kushoto ni Naibu Balozi wa Poland Bi.Awelina Lubieniecka.

 
 Balozi Mwinyi akiagana na mgeni wake Balozi Buzalski baada ya mazungumzo.


Tuesday, June 5, 2018

Wizara ya Ulinzi ya Tanzania yasaini Mkataba wa Makubaliano na Serikali ya Israel

Mkuu wa Tawi la Usalama na Utambuzi Jeshini Brigedia Jenerali, Nicodemus Elias Mwangela pamoja na Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa kwenye masuala ya Ulinzi katika Wizara ya Ulinzi ya Israel, Brigedia  Jenerali Mstaafu, Michael Ben-Baruch wakiwekeana saini katika Mkataba wa Makubaliano ya pamoja ya Ulinzi kati ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa la Tanzania na Wizara ya Ulinzi ya Taifa la Israel, tukio hilo limehudhuriwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa la Tanzania, Mhe. Hussein Mwinyi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi Dkt. Florens Turuka, Balozi wa Israel nchini Kenya awakilisha pia Tanzania, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Bw. Suleiman Salehe pamoja na viongozi wa Jeshi la Kujenga Taifa la Tanzania.Tukio hilo limefanyika katika ukumbi wa Mikutano uliopo Makao Makuu ya Jeshi 
Brigedia Jenerali Nicodemus Elias Mwangela (kulia) pamoja na Brigedia Jenarali Mstaafu Michael Ben-Baruch wakibadilishana mikataba hiyo mara baada ya kumaliza zoezi la kuwekeana saini.
Brigedia Jenerali Nicodemus Elias Mwangela akimkabidhi Brigedia Jenerali Michael Ben- Baruch zawadi ya Nembo ya Jeshi la Kujenga Taifa la JWTZ
Brigedia Jenerali Nicodemus Elias Mwangela (wa sita kulia) pamoja na Brigedia Jenerali Mstaafu, Michael Ben- Baruch (wa saba kutoka kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Tanzania na Israel pamoja na Balozi wa Israel nchini Kenya ambaye anawakilisha Tanzania.



Saturday, June 2, 2018

Umoja wa Mataifa wawatunukia Watanzania medali ya walinda amani

Mhe.Balozi Modest J. Mero (katikati) Mwakilishi wa Kudumu wa  Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, akionesha medali aliyoipokea kutoka Umoja wa Mataifa kwa niaba ya Watanzania walioshiriki katika shughuli za ulinzi wa amani.
Muonekano wa medali

Mhe.Balozi Modest J. Mero (katikati) Mwakilishi wa Kudumu wa  Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa akiwa katika picha mara baada ya kupokea medali


Friday, June 1, 2018

Katibu Mkuu afanya ziara katika Kituo cha Kutoa Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha Namanga


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Adolf Mkenda, akizungumza na wajumbe (hawapo pichani)  waliohudhuria kikao baina yake, watendaji wa Kituo hicho na wafanyabiasha wanaozunguka eneo hilo kabla ya kuanza kwa ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya kituo.

Pro. Mkenda katika ziara hiyo aliambatana na Dkt.Susan Koech Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Maendeleo ya Ushoroba wa Kati kutoka nchini Kenya.

Wawili hao kwa pamoja sambamba na kutembelea maeneo mbalimbali ya kituo hicho katika pande zote mbili za Tanzania na Kenya walipata fursa ya kuongea na watendaji wanaohudumu katika kituo hicho.

Lengo la ziara hii ilikuwa nikuangalia ufanisi wa kituo hicho katika kusaidia kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na watu kutika pande zote mbili za Tanzania na Kenya hivyo
 kurahisisha shughuli za biashara.

 Vilevile ziara hii ililenga kubaini changamoto mbalimbali zinazokikabili kituo hicho na kupelekea kushindwa kutoa huduma kwa ufanisi kwa wananchi wanaotumia kituo hicho.

Aidha Makatibu Wakuu hao wamezipongeza M
amlaka na Taasisi zote zilizopo katika kituo hicho kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuhudumia wananchi. 

Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kulia) akiwa na  Dkt.Susan Koech Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Maendeleo ya Ushoroba wa Kati kutoka nchini Kenya (kushoto), kenye kikao cha wadau kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa OSBP ya Namanga 
Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (watatu kushoto), akisikiliza maelekezo kutoka kwa mmoja wa maafisa wanaohudumu katika Kituo hicho

Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kulia) akiwa nana Katibu Katawala wa Halmashauri ya Longido Bw.Toba Nguvila (kushoto) na Mwenyeketi wa Wafanyabiasha Namanga  (katikati) wakiwa katika ziara za kutembelea kituo cha  OSBD 

Mhe.Dkt. Pindi Chana Balozi wa Tanzania nchini Kenya akizungumza katika Kikao

Katibu Katawala wa Halmashauri ya Longido Bw.Toba Nguvila akizugumza wakati wa kikao

Mmoja wa Maafisa wanaohudumu katika OSBP ya Namanga akitoa mada kwa makatibu wakuu na wajumbe wengine wa mkutano juu ya utendaji wa kituo hicho

Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  akizungumza na wajumbe wakati wa kikao

Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Namanga akizungumza wakati wa kikao

Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akizungumza na mmoja wa maafisa wanaohudumu katika Kituo hicho


Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiwa na  Dkt.Susan Koech Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Maendeleo ya Ushoroba wa Kati kutoka nchini Kenya katika ziara ya kutemebelea OSBP Namanga
Bw.Edwin Iwato Meneja Msaidizi Mkoa,Forodha Arusha akitoa neno la kuwakaribisha Makatibu Wakuu na Wajumbe wengine waliofika kwenye ziara katika Kituo cha OSBP Namanga

Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na  Dkt.Susan Koech Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Maendeleo ya Ushoroba wa Kati kutoka nchini Kenya wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe waliombatana nao kwenye ziara