Tuesday, May 28, 2019

RAIS MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA AFRIKA KUSINI MHE. CYRIL RAMAPHOSA KATIKA IKULU YA PRETORIA NCHINI AFRIKA KUSINI IKIWA NI SIKU MOJA MARA BAADA YA KUAPISHWA NA KABLA YA KUTEUA BARAZA LAKE LA MAWAZIRI MEI 26, 2019


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Pretoria nchini Afrika Kusini leo Mei 26, 2019 ikiwa ni siku moja  baada  ya kuapishwa  kuwa Rais wa Nchi hiyo na kabla hajateua Baraza lake la Mawaziri.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Pretoria nchini Afrika Kusini leo Mei 26, 2019 ikiwa ni siku moja baada  ya kuapishwa  kuwa Rais wa Nchi hiyo na kabla hajateua Baraza lake la Mawaziri. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpa zawadi ya picha ya wanyama Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa baada ya kuwasili katika Ikulu ya Pretoria nchini Afrika Kusini  leo Mei 26, 2019 ikiwa ni siku moja baada  ya kuapishwa  kuwa Rais wa Nchi hiyo na kabla hajateua Baraza lake la Mawaziri.  

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi zawadi ya Kamusi ya Kiswahili na Kingereza pamoja na Vitabu vya Kiswahili Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa kwa ajili ya kujifunza lugha hio ya Kiswahili leo Mei 26, 2019 ikiwa ni siku moja baada  ya kuapishwa  kuwa Rais wa Nchi hiyo na kabla hajateua Baraza lake la Mawaziri. 
Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa akisikiliza maelezo yaliokuwa yakitolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi kuhusu vitabu hivyo vya Kiswahili leo Mei 26, 2019 ikiwa ni siku moja baada  ya kuapishwa  kuwa Rais wa Nchi hiyo na kabla hajateua Baraza lake la Mawaziri.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa mara baada ya mazungumzo yao katika Ikulu ya Pretoria nchini Afrika Kusini leo Mei 26, 2019 ikiwa ni siku moja baada  ya kuapishwa  kuwa Rais wa Nchi hiyo na kabla hajateua Baraza lake la Mawaziri. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mwenyeji wake Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa wakati akizungumza na wanahabari Pretoria nchini Afrika Kusini leo Mei 26, 2019 ikiwa ni siku moja baada  ya kuapishwa  kuwa Rais wa Nchi hiyo na kabla hajateua Baraza lake la Mawaziri. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mwenyeji wake Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa wakifurahia jambo katika mazungumzo yao Pretoria nchini Afrika Kusini leo Mei 26, 2019 ikiwa ni siku moja baada  ya kuapishwa  kuwa Rais wa Nchi hiyo na kabla hajateua Baraza lake la Mawaziri. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa mara baada ya kumaliza mazungumzo yao leo Mei 26, 2019 ikiwa ni siku moja baada  ya kuapishwa  kuwa Rais wa Nchi hiyo na kabla hajateua Baraza lake la Mawaziri.














Makamu wa Rais ashiriki sherehe za uapisho za Rais wa Comoro



Dodoma, 28 Mei 2019

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 

Makamu wa Rais ashiriki sherehe za uapisho za Rais wa Comoro

Kufuatia Mwaliko kutoka Serikali ya Comoro, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan aliongoza ujumbe wa Tanzania katika sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Muungano wa Visiwa vya Comoro, Mhe. Azali Assouman zilizofanyika Moroni, terehe 26 Mei 2019.

Sherehe hizo zinafuatia ushindi alioupata Mhe. Azali katika Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo uliofanyika tarehe 24 Machi  2019.

Mara baada ya Sherehe za Uapisho, Mhe. Makamu wa Rais alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Mhe. Azali ambapo katika mazungumzo hayo, Mhe. Makamu wa Rais aliishukuru Serikali na Wananchi wa Comoro kwa mwaliko na mapokezi mazuri.

Aidha, aliwasilisha salamu za pongezi kutoka kwa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumhakikishia kuendeleza uhusiano na ushirikiano wa kihistoria baina ya nchi hizi mbili.

Kwa upande wake, Mhe. Azali alielezea furaha yake kwa ujio wa Mhe. Makamu wa Rais na kueleza kwamba hiyo ni ishara ya udugu na uhusiano mzuri baina ya Tanzania na Comoro.

Aidha, Mhe. Rais alieleza kwamba kutokana na maendeleo makubwa yaliyofikiwa na Serikali ya Tanzania, ipo haja kwa Tanzania kuendelea kuisadia Comoro katika sekta mbalimbali.

Mwisho, aliishukuru Tanzania kwa salamu za pole kufuatia nchi hiyo kukumbwa na kimbunga Kenneth tarehe 26 Aprili 2019.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
                          
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Comoro,Mhe. Azali Assouman jijini Moroni, Comoro. Mhe. Makamu wa Rais alikwenda nchini humo kushiriki sherehe za uapisho za Rais huyo zilizofanyika tarehe 26 Mei 2019.

Thursday, May 23, 2019

Waziri Prof. Kabudi akutana na Kiongozi wa Kanisa la Othodox

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mazungumzo na Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Othodox Afrika, Papa Beatitude Theodoros II,katika ofisi ndogo za Wizara zilizoko Dar Es Salaam.
May 23,2019
Waziria wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mazungumzo na Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Othodox Afrika, Papa Beatitude Theodoros II pamoja na ujumbe alioambatana nao,katika ofisi ndogo za Wizara zilizoko Dar Es Salaam.
May 23,2019
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Othodox Afrika, Papa Beatitude Theodoros II katika Ofisi ndogo za Wizara zilizoko Dar Es Salaam,May 23,2019


Tuesday, May 21, 2019

Waziri Kabudi akutana na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Uingereza (DFID)

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Uingereza (DFID) Bi. Jane Edmondson alipomtembelea na baadhi ya wajumbe wake katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam Mei 21, 2019
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akimwelezea jambo Bi. Jane Edmondson pamoja na ujumbe alioambatana nao
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Uingereza (DFID) Bi. Jane Edmondson
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Uingereza (DFID) Bi. Jane Edmondson  (wa pili kutoka kushoto) pamoja na wajumbe alioambatana nao, wa kwanza kushoto ni Afisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Tunsume Mwangolombe





Call for Applications for the 2019/2020 Academic Year at the Pan African University

Dodoma. 21st May 2019

PRESS RELEASE

Call for Applications for the 2019/2020 Academic Year at the Pan African University
                                                                                                                 The Pan African University an initiative of the Heads of State and Government of the African Union is inviting young, qualified, talented and enterprising Tanzanians to apply for Masters or PhD degree programmes at any of the four Pan African University Institutes listed below:

  • Pan African University Institute for Basic Sciences Technology and Innovation (PAUST) at Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology (JKUAT) Kenya;

  • Pan African University Institute for Life and Earth Science including Health and Agriculture (PAULESI), at the University of Ibadan (UI), Nigeria;

  • Pan African University Institute for Governance, Humanities and Social Science (PAUGHSS), at the University of Yaoundé II and the University of Buea, Cameroon; and


  • Pan African University Institute for Water Energy Sciences-including climate change (PAUWES), at the University of Tlemcen, Algeria.


Interested candidates should visit the following links for enquiries and more details: - https://www.au-pau.org/submission and pau.scholarships@africa-union.org.

 

The call for applications is open from May 14, 2019 to June 27, 2019.


Issued by;
Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation

Waziri Kabudi akutana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza hapa nchini Mhe. Sarah Cooke alipomtembelea katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam Mei 20, 2019
Maafisa Ubalozi wa Uingereza hapa nchini wakisikiliza mazungumzo kati ya Prof. Palamagamba John Kabudi na Balozi Sarah Cooke (hawapo pichani)
Mazungumzo yakiendelea



Waziri Kabudi akutana na Balozi wa Iran nchini Tanzania

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akimuelezea jambo Balozi wa Iran hapa nchini Mhe. Mousa Farhang alipomtembelea katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam Mei 20, 2019
Maafisa Ubalozi wa Irani hapa nchini wakisikiliza mazungumzo kati ya Prof. Palamagamba John Kabudi na Balozi Mousa Farhang (hawapo pichani)
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mazungumzo kati ya Prof. Palamagamba John Kabudi na Balozi Mousa Farhang (hawapo pichani), katikati ni Mkurugenzi Kitengo cha Habari na Mawasiliano Bw. Emmanuel Buhohela, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati Bw. Ayubu Mndeme (wa kwanza kushoto) na Katibu wa Waziri Bw. Murobi Magabilo
Mazungumzo yakiendelea.