Monday, July 29, 2019

Prof. Kabudi awa mgeni rasmi siku ya Taifa la Misri

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akitoa hotuba kama mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Taifa la Misri. 



Katika hotuba yake Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi alisifu ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Misri, ambapo kwa sasa Misri wanatekeleza mradi mkubwa wa Bwawa la kuzalisha Umeme Nchini ambalo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alizindua mradi huo hivi karibuni.

Pamoja na mambo mengine Prof. Palamagamba John Kabudi alimweleza Balozi kuwa Tanzania inatambua mchango wa Misri kwenye sekta mbalimbali zikiwemo Afya, Elimu na Biashara. Hafla hiyo imefanyika tarehe 29 Julai, 2019 jijini Dar es Salaam 


Juu na Chini ni sehemu ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini na Viongzoi wa Dini wakimsikiliza Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo kwenye picha) kwenye maadhimisho ya siku ya Taifa la Misri
Juu na chini ni sehemu nyingine ya wageni waalikwa wakimsikiliza kwa makini Mhe. Balozi Abouelwafa (hayupo pichani).


Sehemu ya maafisa kutoka Ubalozi wa Misri nchini nao wakimsikiliza kwa makini Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani)
Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akiendelea kuhutubia
Balozi wa Misri hapa nchini Mhe. Mohamed Gaber Abouelwafa naye akihutubia kwenye maadhimisho hayo.    


Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (wa pili kutoka kushoto) pamoja na Balozi wa Misri hapa nchini Mhe. Mohamed Gaber Abouelwafa na Mkewe wakikata keki iliyoandaliwa kwenye hafla hiyo.











Wednesday, July 24, 2019

Elewa Kuhusu SADC




Wadau waipongeza Serikali maandalizi ya Mkutano wa SADC

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Lugha Bashungwa amekutana na kufanya mazungumzo na Wadau mbalimbali kutoka Sekta binafsi na Serikali ikiwa ni muendelezo wa maandalizi ya Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe.

Katika kikao hicho wadau waliahidi kutoa ushirikiano unaohitajika ili kufanikisha maandalizi ya mkutano huo.


 
 Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam tarehe 24 Julai, 2019.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akieleza hatua ziizofikiwa katika maandalizi ya Mkutano wa 39 wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaotarajiwa kufanyika nchini mwezi Agosti 2019.  
Wadau wa Sekta binafsi na Serikali wakimsikiliza kwa makini, Dkt. Mnyepe (hayupo pichani) alipokuwa akiongea.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Bwana Laurean Bwanakunu akichangia jambo katika kikao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya sekta binafsi Tanzania (TPSF), Bw. Godfrey Simbeye akizungumza 
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Lugha Bashungwa (kulia) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe wakiwasikiliza wadau walipokuwa wakizungumza kwenye kikao hicho.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Agness Kayola (wa kwanza kushoto), Kaimu Mkurugenzi Kitengo cha Sheria wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Caroline Chipeta wakiwa kwenye mkutano uliowakutanisha Sekta Binafsi na Serikali
Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya SportPesa, Bw. Abbas Tarimba naye akichangia mada katika kikao hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bw. Albert Jonkergouw naye akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Juu na chini sehemu ya wadau kutoka Sekta Binafsi wakichangia mada kwenye Mkutano huo. 

Dkt. Mnyepe akiendelea kuzungumza kwenye Mkutano huo.