Monday, July 29, 2019

Prof. Kabudi awa mgeni rasmi siku ya Taifa la Misri

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akitoa hotuba kama mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Taifa la Misri. 



Katika hotuba yake Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi alisifu ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Misri, ambapo kwa sasa Misri wanatekeleza mradi mkubwa wa Bwawa la kuzalisha Umeme Nchini ambalo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alizindua mradi huo hivi karibuni.

Pamoja na mambo mengine Prof. Palamagamba John Kabudi alimweleza Balozi kuwa Tanzania inatambua mchango wa Misri kwenye sekta mbalimbali zikiwemo Afya, Elimu na Biashara. Hafla hiyo imefanyika tarehe 29 Julai, 2019 jijini Dar es Salaam 


Juu na Chini ni sehemu ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini na Viongzoi wa Dini wakimsikiliza Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo kwenye picha) kwenye maadhimisho ya siku ya Taifa la Misri
Juu na chini ni sehemu nyingine ya wageni waalikwa wakimsikiliza kwa makini Mhe. Balozi Abouelwafa (hayupo pichani).


Sehemu ya maafisa kutoka Ubalozi wa Misri nchini nao wakimsikiliza kwa makini Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani)
Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akiendelea kuhutubia
Balozi wa Misri hapa nchini Mhe. Mohamed Gaber Abouelwafa naye akihutubia kwenye maadhimisho hayo.    


Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (wa pili kutoka kushoto) pamoja na Balozi wa Misri hapa nchini Mhe. Mohamed Gaber Abouelwafa na Mkewe wakikata keki iliyoandaliwa kwenye hafla hiyo.











No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.