Friday, July 19, 2019

Wizara ya Mambo ya Nje yamuaga Balozi wa Switzerland na Denmark waliyomaliza muda wa kazi nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akimkabidhi Balozi wa Switzerland Mhe. Florence  Tinguely Mattli zawadi ya picha ya kuchora ya  Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro kama kumbukumbu yake ya vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akimkabidhi Balozi Jensen zawadi ya picha iliyochorwa  Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro kama kumbukumbu yake ya vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na Wizara kwa ajili ya kumuaga Balozi wa Denmark Mhe. Einar Hebogard Jensen na Balozi wa Switzerland Mhe. Florence  Tinguely Mattli hapa nchini ambao wamemaliza muda wao wa kazi. Hafla hiyo ilifanyika kwenye Hoteli ya Hyatty Regency Jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Balozi wa Denmark Mhe. Einar Hebogard Jensen (wa pili kutoka kulia), Balozi wa Switzerland Mhe. Florence  Tinguely Mattli (wa pili kutoka kushoto), Balozi wa Uingereza Mhe. Sarah Cooke na Kaimu Balozi wa Marekani Bi. Inmi Petterson kwa pamoja wakimsikiliza kwa makini Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani)
Balozi wa Italy Mhe. Roberto Mengoni (wa kwanza kushoto) na Katibu wa Waziri Bw. Charles Mbando wakimsikiliza kwa makini Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani)
Switzerland Mhe. Florence  Tinguely Mattli naye alitoa neno la shukrani kwa ushirikiano alioupata wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yake akiwa hapa nchini. ambapo ameahidi kuendelea kushirikiana na kuitangaza vyema Tanzania 
Balozi wa Denmark Mhe. Einar Hebogard Jensen naye alishukuru kwa ushirikiano alioupata wakati wote katika kutekeleza majukumu yake akiwa hapa nchini. Hata hivyo hakusita kumpongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihada zake za kupambana na Rushwa pamoja na kujenga miundombinu mizuri hapa nchini.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (katikati), kiongozi wa Mabalozi nchini Tanzania Mhe. Dkt. Ahamada El Badaoul Mohamed (wakwanza kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Jestas Nyamanga wakiwasikiliza Balozi wa Sweden na Denmark (hawapo pichani) walipokuwa wakizungumza.
Kiongozi wa Mabalozi nchini Tanzania Mhe. Dkt. Ahamada El Badaoul Mohamed naye akizungumza neno wakati wa hafla ya kuwaaga Mabalozi wa Switzerland na Denmark (hawapo pichani)  







No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.