Balozi wa Tanzania nchini Komoro, Mhe. Balozi Sylvester Mabumba akitoa hotuba yake kwenye ufunguzi wa
mkutano wa wafanyabiashara (hawapo pichani) wa Tanzania na Komoro, katika hotuba yake aliwahakikishia wafanyabiashara kutoka Tanzania kuwa Ubalozi unaendelea kufanya kazi kwa bidii katika kuratibu shughuli za biashara baina ya Tanzania na Komoro, pamoja na kuwashauri wafanyabiashara hao kufika Ubalozini pindi watakapo kabiliwa na changamoto za aina yoyote ile.
Katika Mkutano huo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Biashara wa Komoro Mhe. Mohamed M'saidie, ambapo aliambata na Rais wa Chamber of Commerce ya
Comoro, Ndg. Ahmed Bazi, Rais wa Chamber of Commerce wa Anjouan, Ndg. Soyad
Mohamed, Rais wa Chamber of Commerce ya Ngazidja, Ndg. Soibroi Eddine Mohamed
Balozi wa Sudan, Mhe. Issam Muhi El Dine Khalili na Kaimu Balozi kutoka Ubalozi
wa Afrika Kusini Bi. Chwane Nomcebo Valentia Mthethwa.
Aidha, washiriki kutoka Tanzania walipata fursa ya kuonesha, kuuza na kutangaza bidhaa zao. Sambamba na hilo washiriki waliweza pia
kufanya majadiliano ya kibishara (B2B) na kuweza kuingia makubaliano ya kufanya biashara
na Wakomoro.
Sekta ambazo zimeonekana kuchangamkiwa zaidi ni sekta ya
ufugaji wa kuku, mayai, bidhaa za mboga mboga na biashara ya nyama ya Ng’ombe.
Mkutano huo umefanyika katika Hoteli ya Retaj nje kigodo ya mji wa Moroni.
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.