|
Balozi wa Tanzania, The Hague, Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju akitoa maelezo kwa mgeni aliyetembelea Banda la Tanzania wakati wa Tamasha maarufu kama Embassy Festival lililofanyika hivi karibuni. Tamasha hilo huandaliwa na Manispaa ya The Hague kwa kushirikiana na Balozi za
nchi mbalimbali zenye Ofisi zake The Hague kwa lengo la kutangaza tamaduni za nchi hizo.
|
|
Balozi
Irene Kasyanju (mwenye fulana kulia) pamoja na Mkuu wa Utawala katika Ubalozi wa Tanzania nchini
Uholanzi, Bibi
Naomi Zegezege Mpemba (wa pili kushoto) wakitoa maelezo kuhusu Tanzania kwa wageni
waliotembelea
Banda la Tanzania, huku Bw. Denis Baraka (wa kwanza kushoto) ambaye ni Mtanzania na mdau wa shughuli za utalii ambaye kwa sasa anasoma nchini Ujerumani na ambaye
kutokana na kupenda kutangaza utalii wa Nchi yake alisafiri kutoka Kiel,
Ujerumani kuja Uholanzi kuungana na Ubalozi pamoja na Watanzania wengine kwenye
Embassy Festival.
|
|
Mwonekano
wa Banda la Tanzania na wageni waliotembelea.
|
|
Balozi
Irene Kasyanju (wa tatu kushoto) akiwa na walishiriki wa maonesho ya mavazi pamoja na baadhi ya
wafanyakazi wa Ubalozi wakiwa wamevaa fulana za kuitangaza Tanzania ambao ni
Bw. Issa Lupatu, Mwambata Fedha wa Ubalozi (wa pili kulia aliyevaa miwani) na
Bw. John Appolo Kilasara,Katibu wa Chama cha Watanzania wanaoishi Uholanzi
(Tanzanians in the Netherlands – TANE) ambaye pia ni mwanafunzi katika Chuo
Kikuu cha ISS nchini Uholanzi
|
|
Balozi
Irene Kasyanju akiwa na Bi. Bahia Kihondo, Mtanzania aliyeandaa maonesho ya
mavazi
pamoja na watoto ambao walifungua
maonyesho hayo kwa kusoma shairi fupi kwa lugha ya Kidachi na Kiswahili.
|
|
Watazamaji
wa maonesho ya mavazi yaliyotangaza utamaduni wa Mtanzania walikusanyika kwa
wingi
kutazama maonesho hayo
|
|
Mwonekano
wa Banda la Tanzania kwa sehemu ya ndani, likiwa limefurika Diaspora waliofika
kulitembelea
na kupata fursa ya kuzungumza na mmoja wa wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania
Uholanzi, Bi Linda Mkony (aliyevaa koti katikati) na Bw. Denis Baraka, wakiwa pia
wamevaa
na fulana maalum za kuitangaza Tanzania |
|
Washiriki
wakionesha vazi lenye michoro ya wanyama “animal prints” wanaopatikana kwenye mbuga za Tanzania
kwa
mtindo wa kisasa
|
|
Maonesho
ya mavazi yakiendelea– vazi la khanga.
|
Washiriki
wa maonyesho ya mavazi wakiwa katika vazi la Kimasaai.
====================================================================================================
UBALOZI
WA TANZANIA, UHOLANZI WASHIRIKI KWA MAFANIKIO
TAMASHA
LIJULIKANALO KAMA “EMBASSY FESTIVAL –
THE HAGUE”
Ubalozi wa Tanzania The Hague, Uholanzi
umeshiriki katika Tamasha maarufu la Embassy
Festival lililofanyika mwezi Septemba, 2019. Tamasha hili huandaliwa na Manispaa
ya The Hague kwa kushirikiana na
Balozi za nchi mbalimbali zenye Ofisi zake nchini humo kwa lengo la kutangaza utamaduni
wa nchi hizo.
Kama ilivyokuwa kwa balozi nyingine, Ubalozi
wa Tanzania ulikuwa na banda lake kwa ajili ya kuonesha utamaduni wa Tanzania.
Kwa kushirikiana na Watanzania wanaoishi Uholanzi (Diaspora), Ubalozi ulitumia fursa
hiyo kutangaza utamaduni pamoja na vivutio vya utalii zikiwemo mbuga za wanyama.
Ubalozi uliandaa maonesho ya mavazi (fashion
show) kwa kuonesha vazi la Kimasai (shuka na shanga, n.k.), pamoja na khanga. Aidha,
Ubalozi uliandaa maonesho ya mavazi na vitambaa vyenye animal prints za Simba, Chui (The big five), Twiga na Pundamilia na
kuvionesha kwa mtindo wa kisasa na hivyo kuvutia watu wengi.
Diaspora wajasiriamali walipata
fursa ya kuuza bidhaa zao mbali mbali za asili kama vile khanga, chai, kahawa
ya Tanzania, shanga, hereni, viatu na bangili. Watu wengi waliotembelea Banda
la Tanzania walifurahia korosho, chai na kahawa vyote kutoka Tanzania
vilivyokuwa vimeandaliwa mahsusi kwa ajili yao.
Ubalozi umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuitangazaTanzania
kupitia tamasha hilo ambapo idadi kubwa ya watu walishiriki na kuchukua vipeperushi
vya kutangaza utalii wa nchi.