Mhe. Balozi Luvanda akiwa katika meza moja na viongozi mbalimbali wakati wa maadhimisho ya miaka 63 tangu kuanzishwa kwa Shiriko la AALCO |
Wageni waalikwa wakiwa kwenye maadhimisho |
Mhe. Balozi Luvanda akiwa katika meza moja na viongozi mbalimbali wakati wa maadhimisho ya miaka 63 tangu kuanzishwa kwa Shiriko la AALCO |
Wageni waalikwa wakiwa kwenye maadhimisho |
Mhe. Hassan Simba Yahaya Balozi wa Tanzania nchini Zambia akihutubia adhira iliyojitokeza kwenye hafla fupi ya kukabidhi mbegu za korosho jimbo la Mongu, Zambia tarehe 16 Novemba, 2019 |
Waziri wa Jimbo la Mongu, Zambia Mhe. Richard Kapita
akihutubia hadhira iliyojitokeza kwenye hafla ya mapokezi ya mbegu za korosho |
Picha ya pamoja baada ya hafla ya kukabidhi mbegu za korosho |
Shemu ya wananchi wa Mongu, Zambia waliojitokeza kwenye hafla ya mapokezi ya mbegu za korosho |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) nae akiungumza wakati wa Mkutano kati ya Mhe. Waziri na Watumishi wa Wizara. |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akizungumza jambo wakati wa Mkutano kati ya Waziri na Watumishi wa Wizara. |
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi akichangia hoja wakati wa mkutano kati ya Waziri na Watumishi wa Wizara |
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bw. Issa Ng'imba akitoa neno kwa Watumishi wakati wa mkutano kati yao na Mhe. Waziri |
Sehemu ya Wakurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwasikiliza viongozi wa Wizara wakati wa Mkutano kati ya Waziri na Watumishi |
Sehemu nyingine ya Wakurugenzi |
Wakurugenzi wakifuatilia hotuba |
Watumishi wa Wizara wakinukuu mazungumzo kati yao na Mhe. Waziri |
Mkutano ukiendelea |
Wakurugenzi wengine wakifuatilia mkutano |
Watumishi wa Wizara wakiwa kwenye mkutano kati yao na Mhe. Waziri |
Sehemu nyingine ya Watumishi wa Wizara kwenye mkutano |
Pichani ni Watumishi wa Wizara wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mhe. Waziri (hayupo pichani) alipozungumza nao |
Sehemu nyingine ya Watumishi |
Balozi Mteule, Bw. Jestus Nyamanga akiwa amesimama ili kupokea pongezi kutoka kwa Mhe. Prof. Kabudi (hayupo pichani) kwa niaba ya Watumishi wa Wizara kufuatia kuteuliwa kwake kwenye wadhifa wa Balozi hivi karibuni |
Mtumishi mpya wa Wizara akijitambulisha |
Mhe. Waziri Kabudi na meza kuu wakiwaongoza Watumishi wa Wizara (hawapo pichani) kuimba wimbo wa ….Tuna imani na Mhe. Rais |
Watumishi wa Wizara wakiimba wimbo huo kwa furaha
|
Na Mwandishi wetu,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki imeikabidhi TAKUKURU jalada la kulifanyia uchunguzi upotevu wa
fedha katika Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Mnyepe amekabidhi
jalada hilo kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John
Mbungo katika ofisi ndogo za Wizara jijiji Dar es Salaam.
Hatua hiyo
imekuja kutokana na jitihada za Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais
Dkt. John Pombe Magufuli za kupambana na kuzuia rushwa pamoja na matumizi
mabaya ya fedha za uma.
Uchunguzi huo
unafanyika baada ya kubainika upotevu/matumizi mabaya ya fedha katika Ubalozi
wa Tanzania nchini Ethiopia.
Kuhusu kiwango
cha fedha kilichopotea Katibu Mkuu, Dkt. Mnyepe, amesema kitajulikana mara
baada ya Takukuru kukamilisha uchunguzi huo wa jalada walililokabidhiwa.
|
Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dkt. Faraji Mnyepe
akimkabidhi Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo jalada la upotevu wa fedha katika Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia leo
jijini Dar es Salaam
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akifungua mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje pamoja na Mawaziri wa Ulinzi na vyombo vya ulinzi na usalama (double Troika) ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) Jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto wake ni Katibu Mtendaji wa SADC, Dkt. Stergomena Tax na anayefuatia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Mnyepe. |
Baadhi ya wajumbe wa Double Troika wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) wakiwa katika mkutano Jijini Dar es Salaam
|
Na Mwandishi
Wetu
Taasisi
ya Uongozi yatakiwa kuhakikisha kuwa inaendelea na maradi wa kuweka kumbukumbu sahihi
za viongozi na taifa kwa kuandika vitabu na machapisho mbalimbali yanayowahusu viongozi
nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla.
Wito huo
umetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli leo jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akizindua kitabu cha maisha
ya binafsi ya Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. Benjamini William Mkapa kiitwacho
'My Life, My Purpose'.
"Napenda
kutumia fursa hii, kumpongeza Rais Mstaafu, Mzee Mkapa kwa kuandika kitabu hiki
na kwa mchango wake mkubwa alioutoa na anaoendelea kuutoa kwa taifa letu pia
naipongeza Taasisi ya Uongozi kwa kuratibu zoezi zima la uandishi wa kitabu
hiki kwa kuwa na mambo mengi mazuri" Alisema Rais Magufuli.
Mhe. Rais
aliongeza kuwa kama alivyoeleza Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Prof.
Joseph Semboja kuwa jukumu la taasisi hii ni kuwaanda, kuwaimarisha na
kuwaendeleza vingozi….bila shaka kuratibu na kuchapisha machapisho mbalimbali
ni sehemu ya jukumu hilo hasa barani Afrika.
"Wito
wangu kwenu Taasisi ya Uongozi muangalie jinsi ya kutafsiri kitabu hiki kwa
lugha ya Kiswahili…..naomba kusisitiza viongozi wastaafu wengine waandike
vitabu ili kutoa chachu kwa vijana wetu ambao watakuwa viongozi wa baadae
kujifunza mambo mbalimbali, tusiishie tu kwa viongozi wastaafu katika ngazi ya
Urais bali hata viongozi wengine," Amesema Rais Magufuli.
Rais
Magufuli ameongeza kuwa nitafurahi kusoma kitabu cha Maalim Seif, …….nitafurahi
kusoma kitabu cha mzee Warioba…… nitafurahi kusoma kitabu cha Spika Job Ndugai kuwa
nae amezaliwa kongwa.
Uzinduzi
wa kitabu cha maisha binafsi ya Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. William
Benjamin Mkapa kijulikanacho kwa jina la "My Life, My Purpose" ulihudhuriwa
na Rais wa Mstaafu wa awamu ya pili, Mhe. Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa
awamu ya Tatu Mhe. Benjamini William Mkapa na Rais wa awamu ya Nne Mhe. Jakaya
Mrisho Kikwete pamoja na Rais wa Zanzibar, Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed
Shein.
Mbali na
kuzindua kitabu hicho, pia leo ilikuwa ni siku muhimu kwa Rais Mstaafu wa awamu
ya Tatu, kwani leo alikuwa akisheherekea kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa
akiwa ametimiza miaka 81 ya kuzaliwa.
Viongozi mbalimbali
waandamizi wa Serikali waliohudhuria uzinduzi wa kitabu hicho ni pamoja na Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi John Kijazi, Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai na Balozi wa Finland Nchini Tanzania
Riita Swan
Wengine ni
Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba, Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Elimu na
Sayansi, Prof. Joyce Ndalichako, Mabalozi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba
na Sheria, Bw. Amon Mpanju, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda,
viongozi wa vyombo vya ulinzi na Usalama, wakuu wa mikoa, viongozi wa dini,
wakuu wa taasisi mbalimbali na asasi za kiraia.
Awali
akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli, Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa alimpongeza Rais Magufuli kwa
jitihada zake za kuhakikisha kuwa taifa linajitegemea hasa katika maendeleo.
"Kujitegemea
ni muhimu sana kama nchi, na ni muhimu kwa heshima ya taifa letu" amesema
Rais Mkapa.
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli wa pili kushoto akiwa ameshika kitabu cha My Life, My Purpose katika picha ya pamoja na Rais mstaafu wa awamu ya pili, Mhe. Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. William Benjamin Mkapa na Rais wa awamu ya Nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein. |
Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. William Benjamin
Mkapa akimkabidhi nakala ya kitabu cha 'My Life, My Purpose' Rais John Pombe
Joseph Magufuli mara baada ya uzinduzi wa kitabu hicho. Rais mstaafu wa awamu
ya pili, Mhe. Ali Hassan Mwinyi na Rais mstaafu wa awamu ya Nne Mhe. Jakaya Mrisho
Kikwete.
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akizindua rasmi kitabu cha 'My Life, My Purpose' wengine ni Rais mstaafu wa Awamu ya pili, Mhe. Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. William Benjamin Mkapa na Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete. |
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitoa
hotuba yake wakati wa uzinduzi wa kitabu cha 'My Life, My Purpose' chenye
historia ya maisha binafsi ya Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa
|
Balozi wa Finland Nchini Tanzania Riita Swan akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa kitabu cha 'My Life, My Purpose' chenye historia ya maisha binafsi ya Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa |
Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. William Benjamin Mkapa akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli wakati alipowasili ukumbini kwa ajili ya uzinduzi wa kitabu cha 'My Life, My Purpose'. Kushoto ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Elimu na Sayansi, Prof. Joyce Ndalichako, Mabalozi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Amon Mpanju. Wengine kushoto ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na Mke wa Rais Mkapa, mama Anna Mkapa. |