Monday, January 20, 2020

WIZARA YAWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI KWA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA JIJINI DODOMA



Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (aliyevaa miwani) akiwasilisha taarifa ya utendaji wa Wizara kwa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma, kulia ni Naibu Katibu Mkuu wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhan Mwinyi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (aliyevaa miwani) akiwasilisha taarifa ya utendaji wa Wizara kwa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) Mhe. Mussa Azzan Zungu  (kushoto) akisikiliza taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliyokuwa ikiwasilishwa na Mhe. Dkt. Ndumbaro.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) Mhe. Mussa Azzan Zungu na baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo wakisikiliza taarifa ya Wizara iliyokuwa ikiwasilishwa na mhe. Dkt. Ndumbaro
====================================================================================================

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imewasilisha taarifa ya utendaji kazi wake kwa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na kusema Serikali ina mpango wa kujenga bandari ndogo katika ziwa Tanganyika mpakani mwa Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema hayo alipowasilisha taarifa  taarifa ya Utekelezaji wa Wizara ya mwezi Juni hadi Desemba 2019 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.

“Mhe. Mwenyekiti, ili kunufaika kiuchumi kupitia DRC, tumepanga kujenga bandari ndogo katika Ziwa Tanganyika na kufungua Ubalozi mdogo katika mji wa Lubumbashi, mji huu uko umbali wa kilomita 3000 kutoka jijini Kinshasa,” alisema Dkt. Ndumbaro.

Amesema ujenzi wa bandari ndogo eneo la mpakani katika Ziwa Tanganyika kutawezesha bidhaa zinazozalishwa Tanzania kwenda nchini humo kiurahisi kuliko ilivyo sasa ambapo wafanyabiashara wanapitisha biashara zao nchini Zambia hadi kufika nchini DRC.

Aidha amesema Serikali inachukua hatua mbalimbali katika maeneo ya mpaka na nchi hiyo ikiwemo  kuhakikisha amani na usalama vinaimarishwa ili wananchi wa pande zote mbili wafanye biashara bila hofu yoyote.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Mussa Azzan Zungu imekutana na Menejimenti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dodoma na kupata taarifa mbalimbali za utendaji wa Wizara.

Mhe. Zungu amesisitiza umuhimu wa Tanzania kushirikiana na DRC katika kuhakikisha amani na usalama vinaimarika hata baada ya Jeshi la Kulinda Amani la Umoja wa Mataifa (MONUSCO) kumaliza muda wake nchini humo.

Sunday, January 19, 2020

TANZANIA YAWASILISHA SALAM ZA RAMBI RAMBI NA PONGEZI - OMAN

Mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwasilisha Salam za rambirambi kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman Mhe. Yusuf bin Alawi kufuatia kifo cha Sultan wa Oman - Sultan Qaboos bin Said Al Said pia Salaam za pongezi kwa kiongozi mpya wa Oman Mtukufu Haitham bin Tariq bin Taimur Al Said, Muscat,Oman


Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman Mhe. Yusuf bin Alawi akizungumza mara baada ya kupokea salam za rambirambi kufuatia kifo cha Sultan wa Oman - Sultan Qaboos bin Said Al Said pia Salaam za pongezi kwa kiongozi mpya wa Oman Mtukufu Haitham bin Tariq bin Taimur Al Said, Muscat,Oman

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman Mhe. Yusuf bin Alawi,mara baada ya  kuwasilisha salam za rambirambi kufuatia kifo cha Sultan wa Oman - Sultan Qaboos bin Said Al Said pia Salaam za pongezi kwa kiongozi mpya wa Oman Mtukufu Haitham bin Tariq bin Taimur Al Said, Muscat,Oman. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Oman Balozi Abdallah Abasi Kilima.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman Mhe. Yusuf bin Alawi,mara baada ya  kuwasilisha salam za rambirambi kufuatia kifo cha Sultan wa Oman - Sultan Qaboos bin Said Al Said pia Salaam za pongezi kwa kiongozi mpya wa Oman Mtukufu Haitham bin Tariq bin Taimur Al Said, Muscat,Oman.

UJUMBE MAALUM WA RAIS DKT MAGUFULI WAWASILI MUSCAT - OMAN

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa na Mshauri Maalum wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman Dkt. Salim bin Nassir Al Ismaili. Prof. Kabudi yuko Muscat - Oman kwa ajili ya kuwasilisha ujumbe maalum wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kufuatia kifo cha Sultan wa Oman, Sultan Qaboos  Bin Said Al Said aliyefariki Januari 10, 2020, pia kuwasilisha Salam za pongezi kwa Sultan Mpya wa Oman Mtukufu Haitham bin Tariq bin Taimur Al Said

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamgamba John Kabudi (Mb) akiwa na Mshauri Maalum wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman Dkt. Salim bin Nassir Al Ismaili. Prof. Kabudi yuko Muscat - Oman. Kushoto ni Balozi wa Tanzania Nchini Oman Balozi Abdallah Abasi Kilima.

Saturday, January 18, 2020

TANZANIA YATANGAZA UTALII UHOLANZI

Ubalozi wa Tanzania nchini Uholanzi na wadau wengine; Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro (NCAA) pamoja na makampuni binafsi kama vile, Sea-Cliff Resort & Spa Ltd, Natures Land Safari’s & Rentals na Mbalageti Safari wanashiriki Maonesho ya Kimataifa ya Utalii (Holiday Fair 2020) yanayofanyika katika mji wa Utretch, Uholanzi kuanzia tarehe 16 hadi 19 Januari 2020.

Hii ni fursa nyingine muhimu kwa Tanzania kujitangaza na kuzidi kuvutia wadau zaidi katika Sekta ya Utalii, kuja kutembelea na kufanya biashara na Tanzania. Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Irene F. M. Kasyanju tayari amekutana na wadau wote waliofika Uholanzi, kuhakikisha kuwa Tanzania inanufaika ipasavyo na maonesho hayo.

Maonesho hayo ambayo kwa lugha ya kidachi yanajulikana kama “Vakantiebeurs 2020” hufanyika mwezi Januari kila mwaka na yanahudhuriwa na mataifa mbalimbali duniani kwa lengo la kutangaza na kuuza vivutio vya Utalii na Burudani 
Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju (wa pili kushoto) akiwa na baadhi ya wawakilishi wa taasisi za Tanzania wanaoshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Utalii nchini Uholanzi. Kutoka kushoto ni Bw. Michael Christian Makombe kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Bibi Alistidia Karaze kutoka Bodi ya Utalii Tanzania na Bw. Gerald Mono kutoka TANAPA. 
Balozi Irene Kasyanju ( wa pili kulia) akiwa na wawakilishi wa TTB na Kampuni ya MAKASA Safaris kutoka Moshi, Kilimanjaro.

Balozi Irene Kasyanju akipokea zawadi ya Kalenda za 2020 kutoka kwa Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania kwenye Maonesho hayo, Bibi Alistidia Karaze ambaye ni Afisa Mkuu wa Utafiti na Maendeleo kutoka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

Balozi Kasyanju akiwa na wawakilishi kutoka Hifadhi ya Ngorongoro, TTB, TANAPA; pamoja na Kampuni binafsi yaani, Nature’s Land Safaris & Rentals;  na Mbalageti Safari zote kutoka Mwanza, Tanzania na Sea-cliff ya Dar es Salaam.

Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi akiwa na Balozi wa Uganda nchini humo Mhe. Miriam Blaak ambaye alitembelea  kwenye Banda la Tanzania.
Mandhari ya Banda la Tanzania likionesha wateja mbalimbali wanavyolitembelea. Wateja wanaotembelea licha ya kujionea vivutio vya utalii, wanaonjeshwa pia vyakula vitamu vya Tanzania kama vile vitumbua na mandazi.