Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Wilbert Ibuge na Balozi Nguyen Doanh wa
Vietnam wakiagana walipomaliza mazungumzo yao Ofisini jijini Dodoma .
|
Katibu
Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi
Col. Wilbert A. Ibuge leo tarehe 26 Machi, 2020 amekutana na kufanya mazungumzo
na Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Nguyen Kim Doanh katika ofisi za Wizara,
Makao Makuu, Jijini Dodoma.
Balozi
Doanh alikuja jijini Dodoma kufuatia wito wa Balozi Ibuge na kufanya mazungumzo
yaliyohusu mambo mbalimbali kuhusu mahusiano baina ya Tanzania na Vietnam, likiwemo
suala la uwekezaji wa Vietnam nchini kupitia Kampuni ya simu ya Halotel.
Katika
mazungumzo yao, viongozi hao wamekubaliana kuendelea kuimarisha mahusiano
baina ya Nchi mbili hizo, ikiwemo uendelevu wa mawasiliano ya Kidiplomasia
ambapo mahusiano ya Tanzania na Vietnam yamefikisha miaka 55 mwaka huu huku fursa za uwekezaji nchini zikiendelea
kuimarishwa na hivyo kuiwezesha Serikali ya Vietnam ambayo ni mmiliki wa
Kampuni ya Simu ya mkononi ya Halotel kuwekeza nchini na kuendesha shughuli zake.
Balozi Ibuge
pia alimjulisha Mhe. Balozi Doanh kuwa Serikali ya Tanzania kupitia Wizara
itaendelea kuhimiza uwekezaji kutoka Vietnam na kusisitiza uwekezaji huo
kuzingatia sheria za nchi, kwa lengo la kuwepo tija kwa pande zote
zinazohusika.
Kufuatia
kikao hicho, Mhe. Balozi Doanh aliahidi kuendelea kuyasisitiza makampuni ya
Vietnam Nchini ikiwemo kampuni ya Halotel kuzingatia Sheria, Taratibu na Kanuni
zilizowekwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuhakikisha
pande zote mbili zinanufaika.