Wednesday, March 18, 2020

WAZIRI MKUU MHE. KASSIM MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA MAWAZIRI WA SADC

Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akifungua Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika uliofanyika kwa njia ya video kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Machi 2020.

Mhe. Waziri Mkuu akitoa salamu kwa Nchi Wanachama wa SADC ambao ni wajumbe wa Mkutano huo unaoongozwa na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa jumuiya hiyo.
Pamoja na salamu hizo za ufunguzi Mhe. Waziri Mkuu alipongeza jitihada zinazofanywa na Nchi Wanachama katika kukabiliana na majanga mbalimbali ikiwemo la ugonjwa wa virusi vya CORONA ambao umewezesha nchi wanachama kushirikiana kutafuta namna bora ya kuendelea na shughuli za utekelezaji kwa ustawi wa kanda na watu wake.

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC, Mhe. Palamagamba John Kabudi akitoa hotuba ya utangulizi kumkaribisha Waziri Mkuu ili aweze kufungua mkutano wa wa Baraza hilo uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jinini Dar es Salaam.

Katibu Mtendaji wa Sekretariet ya SADC, Dkt. Stergomena Tax akitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa majukumu ya jumuiya hiyo wakati wa hafla fupi ya ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC.

Wajumbe wa Mkutano huo ambao ni Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na viongozi wengine waandamizi wakifuatilia hafla ya ufunguzi. 


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.