Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) amekutana na
kufanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Balozi Sarah Cooke,
Balozi wa Norway nchini Mhe. Balozi Elisabeth Jacobsen pamoja na Balozi wa
Korea nchini Mhe. Balozi CHO tae-ick.
Dkt. Ndumbaro amekutana na mabalozi
hao leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na
mambo mengine wamejadili masuala ya kuongeza ushirikiano wa kidiplomasia pamoja
na mikakati ya kujikinga na kupambana na homa ya virusi vya corona.
Pia, Mabalozi hao waliishukuru Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Kushirikiana na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika –SADC
kwa maamuzi yake ya busara kupitia mawaziri wa Afya ya kuamua vikao vyote
vinavyoendelea kufanyika kwa njia ya mtandao yaani (Video Conference) ikiwa ni
hatua mathubuti ya kukabiliana na maambukizi
ya Ugonjwa huo.
Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akiongea na Balozi
wa Uingereza nchini Mhe. Balozi Sarah Cooke pamoja na Balozi wa Norway nchini
Mhe. Balozi Elisabeth Jacobsen
Balozi wa Norway nchini Mhe. Balozi
Elisabeth Jacobsen akimuuliza jambo Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro. Kushoto kwake ni Balozi
wa Uingereza nchini Mhe. Balozi Sarah Cooke.
Balozi wa Korea nchini Mhe.
Balozi CHO tae-ick akiongea na Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro
Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akimfafanulia jambo Balozi wa Korea nchini Mhe. Balozi CHO tae-ick |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.