Ubalozi
wa Tanzania nchini Ubelgiji umepata soko kubwa la maharage machanga ya kijani yanayojulikana
kama haricots vertz(green thin beans) nchini Ubelgiji. Soko hilo limepatikana
baada ya Balozi wa Tanzania nchini humo, Mhe. Jestas Abuok Nyamanga kufanya mazungumzo
na uongozi wa juu wa kampuni ya
CBG-Charlier-Brabo Group inayonunua maharage hayo kutoka sehemu mbalimbali duniani
na kuyauza katika supermarkets kubwa za Carrefour, Delhaize na Aldi za nchini Ubelgiji,
Luxembourg na nchi nyingine za Ulaya.
Katika
mazungumzo hayo yaliyofanyika tarehe 3 Machi 2020, kampuni hiyo ipo tayari kununua
containers kati ya 180-200 za maharage hayo kila mwaka kutoka Tanzania.
Kupatikana
kwa soko la maharage hayo nchini Ubelgiji ni habari njema kwa wakulima wa
Tanzania na wafanyabiashara wa mazao ya kilimo hususan wa aina hiyo ya maharage
ambayo tayari Tanzania inayauza nchini Uholanzi.
Kampuni
hiyo pia imeonesha utayari wa kununua aina nyingine ya maharage ijulikanayo kama
red kidney beans na chickpea kwa kiwango cha containers 8
kila mwaka katika hatua za mwanzo.
Ubalozi
wa Tanzania unatoa wito kwa Watanzania kuchangamkia upatikanaji wa soko hilo jipya
nchini Ubelgiji kwa kuwasiliana na kampuni hiyo kupitia tovuti yao ya www.cbg.be au kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki kwa maelekezo zaidi.
Maharage aina ya haricots vertz(green thin beans) yaliyopata soko nchini Ubelgiji. |
Balozi akiangalia bidhaa aina ya nanasi zilizokatwa na kuifadhiwa katika kopo na kampuni hiyo ambazo pia zinaweza kuagizwa kutoka Tanzania |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.